Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Narudia tena, Mbowe hakustahili haya yanayotokea Bungeni, angeshauri kisha awe kimya, kuliko alivyoongea.

Labda akawaombe msamaha, watamkasirikia sana na kitatumika hicho 2025
 
HIvi hawa wabunge wamewahi kukaa Zanzibar au Pemba na waka-experience ubaguzi uliopo huko.? Au wanaongea kwa mihemko tu.? Niliwahi kutamkiwa na Mpemba nikiwa chakechake kuwa hawanitambui sababu mimi si Mpemba. Ubaguzi upo Zanzibar na Pemba
Uongo huo.
 
Narudia tena, Mbowe hakustahili haya yanayotokea Bungeni, angeshauri kisha awe kimya, kuliko alivyoongea.

Labda akawaombe msamaha, watamkasirikia sana na kitatumika hicho 2025
Kosa lake ni nini, mbona hakuna chochote kilichojibiwa juu ya hoja zake?

Hoja ya Mbowe ni kwanini bandari za Zanzibar hazijaguswa katika huo uwekezaji mnaouita mzuri?
 
Hivi Nape huwa hajui kutoa hoja kulingana na mada husika, yeye yupo kutisha watu tyuuh, ko Mbowe asiseme ukweli kisa maridhiano? Ko maridhiano yalikua ili awe kimya kwa mambo ya kitapeli km mkatabaa huu??

Afu haoni aibu anafananisha mkataba wa bomba LA mafuta na huu wa bandarii, khaaah

Hivi ana Elimu gani huyu Nape?? Mxxxiiiiieeeeeewwwww
 
Tungeambiwa kwanza kama ile IGA inayozunguka mitandaoni ni ya ukweli au uongo? Hilo la TPA kuachiwa gati chache kuziendesha hata Mbowe alilizungumzia.

Amandla...
Serikali inajichanganya sana katika hili.

Katika Clubhouse ya Msigwa, Msemaji wa serikali (Msigwa) ameikana. Hapo hapo alikuwa na CEO wa TPA, kila kifungu anachokisema na kukinukuu CEO kipo katika ile ya mtandaoni. Kifungu kwa kifungu.This was a contradiction.

Hata kama huu mkataba ni mzuri na una manufaa kwa umma na raia wengi sana wanaweza kuutetea, serikali inavyofanya usiri, usiri huo unatoa ishara kwamba kuna jambo baya.

Kwa nini mikataba hii haiwekwi wazi?

Nature abhors a vacuum, katika Information Theory tunafundishwa kwamba, usipoweka habari sahihi wazi, unaalika habari zisizo sahihi zisambae. This is PR 101, somo la awali kabisa katika PR. Kwa nini serikali inaendekeza usiri? Ni kwa sababu sisi ni washamba sana tunaendekeza usiri wa kizamani?

Au ni kweli usiri unatokana na ukweli kwamba serikali inajua kuwa mikataba ikiwekwa wazi na kukubaliwa na serikali kuwa hii ndiyo mikataba yenyewe, wananchi wataikosoa na kuonesha mapungufu?

So, huu ni ushamba, hadaa ya wezi au yote mawili pamoja?

Kama mkataba una manufaa sana kwa wananchi, kwa nini usiwekwe wazi?

Kwa nini uliwekwa kwenye tovuti ya bunge halafu ukatolewa? Bunge halijui kwamba wananchi wanaweza kuwasaidia sana wabunge kujadili mkataba?

Kwa nini Msigwa aliukataa Clubhouse? Kama huo alioukataa Msigwa si wenyewe, wenyewe uko wapi?

Wananchi wana haki ya kikatiba (ibara ya 18 (1) na (2) ) ya kujua jinsi nchi yao inavyoendeshwa. Serikali haioni kwamba inavunja katiba kwa kupitisha hii mikataba bila kuwaonesha wananchi mikataba inasemaje?
 
Kosa lake ni nini, mbona hakuna chochote kilichojibiwa juu ya hoja zake?

Hoja ya Mbowe ni kwanini bandari za Zanzibar hazijaguswa katika huo uwekezaji mnaouita mzuri?
Uzanzibar na Zanzibar
 
Si ya kupitisha hilo azimio lao?? Au nini hatima ya wao kushinda hapo Dodoma??
Kikao cha leo kilikuwa cha kuishauri serikali iende vipi itapoingia mikataba ya kiutendaji kutokana na makubaliano ya ushirikiano na maendeleo tuliokubaliana na Dubai.
 
Back
Top Bottom