Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

Ikiwa mkuu wa nchi ndio hivi walio chini yake ataweza kuwanyooshea kidole kweli.
 
1688840246783.png

Hawa wabunge wetu wamekosa sifa ya kuitwa wabunge, tangu leo waitwe MANGUNGOS. Hawa mangugos lazima washitakiwe!! Takukuru wachunguzeni, huko kujitoa ufahamu si kawaida!! wamevimbiwa hawa na "kitu kikubwa" sana!!
 
Itaingia kwenye rekodi ya kudumu. Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania 2020-2025 limeridhia kuuzwa kwa bandari zetu bure kwa waarabu wa DP World!! Nasema ni bure maana hawajaainisha manufaa yoyote tutakayopata wala hawajaainisha huyo mwarabu atawekeza kiasi gani cha pesa!! Ukisimuliwa huwezi kuamini lakini ndio ukweli wenyewe!!

Wameenda mbali zaidi wanataka kufanya marekebisho ya sheria inayozuia mgeni kumiliki ardhi ili huyo mwarabu amiliki pia ardhi ambako kuna bandari zetu!! Inatia kisirani sana!! Sultan Mangungo tutasema hakuwa na elimu, je hili bunge lililojaa wasomi tutasemaje? Lazima kuna "kitu kikubwa" wamepewa hawa!! maana si kwa kujitoa ufahamu hivyo!! hawana aibu! Wabunge mtaficha wapi sura zenu!!
 
Walichokifanya wabunge wa Tanzania kwa kuridhia bandari zetu kupewa waarabu bure, wanafanana na sultan Mangungo kukabidhi ardhi yote ya utawala wake kwa wajerumani kupitia mkataba mbovu. Kwa hiyo hawa wabunge ni sawa na Mangungo al;ichokifanya. Kwa hiyo tusiwaite wabunge tena, bali tuwaite MANGUNGOS maana wako wengi.
Tangu leo tuwaite MANGUNGOS!!
1688848341107.png
 
Uwezi kumfananisha mangungo na hawa watu. Mangungo alikuwa analikuwa anatia dole gumba uku anashangaa. Ila wabunge wanajua maana ya mkataba. Uoni kuna tofauti kubwa hapa
 
1688895309802.png

Natoa zawadi hii kwa watu wanaitetea katika mikataba mibovu iliyosaini ukiwepo wa bandari .
Weka majina yao hapa.
 
I am so proud of my fellow Tanzania on this.
Tumeamka Kwa pamoja na asilimia kubwa tunaongea lugha Moja ya kutetea rasilimali zetu. Tusiwe selfish, tufikirie vizazi vijavyo siku tukiondoka hapa duniani

Hii nchi ilikuwa inahitaji a common enemy, haiitaji chama cha siasa
 
Kitu pekee ni watz tubaki na asilimia 75 ya umiliki wa Bandari,hao dp world walete teknolojia ya kisasa ya uendeshaji wa Bandari yetu.

Nadhani itasaidia kurekebisha sintofaham inayoendelea kwa sasa.

Mungu ibariki Tanzania yetu
 
25% ni kubwa sana labda 2.5%
Kama una kampuni usingetoa 25% kama wewe ndio mwenye mali aisee 25 ujue ni robo hiyo

Imagine ni kama umewapa miguu mpaka kwenye magoti
Mimi ningewapa kiganja tu

Nina kampuni najua maana ya 25%
 
25% ni kubwa sana labda 2.5%
Kama una kampuni usingetoa 25% kama wewe ndio mwenye mali aisee 25 ujue ni robo hiyo

Imagine ni kama umewapa miguu mpaka kwenye magoti
Mimi ningewapa kiganja tu

Nina kampuni najua maana ya 25%
Afteral serikali imeshaweka trilioni moja toka world bank kwa hiyo inapaswa kuwa na zaidi ya 90%
 
Kijana Mzalendo Nkindikwa David amehoji Chama cha Mapinduzi kimepewa ridhaa na watanzania kulinda mali za nchi kwanini kimebariki nchi kuuzwa kupitia mkataba wa bandari

 
Back
Top Bottom