Mtoa mada umeandika kihisia sana na mahaba ya kutosha, kwanza rekebisha baada ya Dar ni Mwanza then Arusha kisha Dodoma
Nasema hivi kwa sababu Dodoma inakua ndio inajengwa ila haina hadhi hiyo unayoipa lkn pia unaikosea heshima nchi yetu kimataifa haiwezekani jiji la pili baada ya Dar (kwa maelezo yako) iwe Dodoma mji ambao usafiri mkuu ni bajaji,
Tusiifananishe Dom this time na miji kama Mwanza na Arusha, lkn pia kuondoa utata kati ya Mwanza na Arusha ipi ni the second after Dar
Serikari inagawa wilaya na halmashauri (manispaa) kufuatana na ukubwa wa eneo na mahitaji wa watu kuopata huduma za kiserikali, lkn pia kuirahisishia serikali kuihudumia jamii, yaani kupunguza mzigo wa serikali kuwafikia watu
Mfano Manyara ni mkoa uliotokana na Arusha ilikuwa ni kazi sana kwa viongozi wa mkoa wa Arusha kutatua changamoto za mkoa mzima ikabidi waupunguze ili sehemu ingine iwe na viongozi wao pia
Mwanza ina manispaa 2 za Ilemela na Nyamagana ambazo pia ni wilaya zipo eneo moja la mji, Arusha ina manispaa 1 na wilaya moja ya Arusha the same kwa Dom pia
Mwanza inafanya mchakato wa kuitangaza Kisesa kuwa wilaya na itakuwa na wilaya 3 ndani ya eneo moja wakati hiyo miji mingine yote ina wilaya moja moja na zinahudumika
Arusha sio mji wa serikali ila uwepo wa makao makuu ya EAC imerahisisha jumuia kujenga majengo ambayo yanapendezesha mji, Dodoma inajengwa na serikali 70% ya majengo marefu ya Dodoma mmiliki ni serikali Mwanza 86% ya majengo ni sekta binafsi (hii inatosha kusema kibiashara Mwanza haina mpinzani)
Nimekuwepo Dom vipindi tofauti tofauti ni mji naufahamu vizuri ni mji unaokua, tusiiweke tayari fikiria sehemu kama Kisasa, Makulu, Kikuyu ni mitaa mikubwa ila haina route za daladala ni mwendo wa bajaji, Sehemu kama Iyumbu na Michese unaweza kaa saa nzima na zaidi bila kupata daldala zinazoenda maeneo hayo Dom inakua lkn Mwanza na Arusha pia hazijasimama, Mwanza ujenzi wa daraja la Busisi-Kigongo unaendelea, soko kuu ambalo ni kubwa kuliko yote nchini linakamilika mwaka huu, ujenzi wa meli kubwa kuliko zote ukanda wa maziwa makuu upo mwishoni kabisa, meli ambayo itaiunganisha nchi yetu na EAC five star hotel mbili soon zitaanza kutumika (NSSF 5 Star hotel na Kapri 5 star hotel) trust me hivi vitu vitaiamsha sana Mwanza, kibiashara Dom inamisi vitu vingi sana hakuna maduka makubwa ukiwa Dom kuna bidhaa bado ili kuipata ni lazima uifuate Dar
Kwenye population hapa ndio bado kabisa nenda Dodoma kipindi bunge halipo lkn pia vyuo vimefunga utashangaa asilimia kubwa nyumba za Dodoma wanaishi watu sio zaidi ya 4-6 nyumba moja na kuna nyumba zingine zimejengwa hazina watu kabisa tembea Mkonze, Chidachi, Kisasa, Iyumbu kuna nyumba nyingi sana zimekamilika lkn hawaishi watu, watu walijenga kwaajili ya kupangisha
Mwanza nyumba yako kukosa mpangaji utake wewe, vile vile kwa Arusha
Mwanza hakuna sehemu ya mji Daladala hazifiki the same to Arusha