Duh! Wee jamaaa, Upande wa kilimo Dom unaweza ilinganisha na Mwanza?
Kwa upande wa madini ya dhahabu kanda ya ziwa ni kama misikiti Zanzibar, sehemu zote zina madini sjui kama unajua kuwa 80% ya mkoa wa Geita ni dhahabu, Sengerema kunajengwa mgodi mkubwa kuliko ule wa GGM, Mara kuna mgodi mkubwa wa North Mara, Kahama ina migodi mikubwa zaidi ya miwili, Mwadui ina almasi, Biharamulo nk sehemu zote hizo zinainufaisha Mwanza
Upande wa viwanda ikikitoa kiwanda cha magodoro QFL na kile kimoja cha zabibu Dom ina kiwanda gani kingine? Cha mbolea ni mkakati hakijaanza hata kujengwa,
Wakati Mwanza ina viwanda vya samaki vikubwa zaidi ya vinne, SBC wanafyatua soda za pepsi Mwanza, Cocacola wanafyatua soda Mwanza, Sayona pia,, sjui kama unajua Mwanza nondo hawaagizi Dar, Sjui kama unajua bia zote pia Mwanza hawaagizi Dar
Upande wa sekta binafsi Mwanza huwezi ilinganisha na Dom hata kidogo