ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Msiwaonee wivu wanakuja vizuri wameanza na mipango miji dodoma mitaa yote inapendeza funzo kwetu arusha, mwanza na hata mbeya
Kila siku Dodoma kuna mradi mpya unatangazwa na haitaishia hapa kila bajeti utaskia kuna jambo jipya Dodoma
Na Dodoma haikuwekwa mji mkuu na Magufuli ni tangu enzi za Nyerere huko
Magufuli sio mtu wa dodoma kwamba anafaidika napo
Alichokifanya nikutekeleza jambo lililopaswa kufanyika miaka 50 iliyopita akalifanya yeye na sio kuamia Dodoma tu hata Bwawa la Mwalimu Nyerere la umeme mpango ulikuwepo kwa miongo mingi ila yeye akatekeleza kwahiyo mwamba alikua mtekelezaji mzuri asiyependa mambo kucheleweshwa kwa hilo nampa kongole
Na kuamia Dodoma ni faida kubwa sana kwa nchi hamjui tu
NB: Shida moja tu ninayoiona ni serikali kurudia makosa yaleyale ya Daresalaam kulundika kila kitu Dodoma pamoja na kuwa Dodoma ni makao makuu unajengaje km220 barabara zisizo hata na mahitaji zingeweza kusubiri wakati miji mingine wanashida na km20 tu, Arusha tuna barabara inahitajika kupanuliwa ya km9 tu kuelekea airport tangu kipind cha kikwete ni danadana tu sasa hiv mipango miji wote ni Dodoma tu
Rai yangu tusiue miji mingine ili Dodoma ionekane inastawi miji mingine inaweza ikaboreshwa na Dodoma ikastawi vile vile
View: https://x.com/dailynewstz/status/1871088101524689315?t=GXkY3Vj5xQ7Sche2djeMoA&s=19