Dodoma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki ibada Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska

Mitandao ni mizuri ila wengine Wanaitumia Vibaya. Tuitumie kwa Kumuogopa MUNGU. Waliokuwa wanatuma picha yangu na Mshumaa pembeni, Wengine wanasema Mzee amekata moto, Kazi ambayo MUNGU amenituma kuifanya sijaimaliza. Wakati Utakapofika nitarejea kwa Muumba wangu” Philip Mpango.
 
Utajuaje kama sio TISS!?....
 
Amesharudi kutoka nje ya nchi kikazi?😁😁😁.hivi makalu wa rais uwa hapokewi kiserikali kama rais anaporudi kutoka safari.yaani anakuwa kama mjumbe wa nyumba kumi tu.
 
Wenye gubu hawaachi maneno. Watasema hii picha ya mwaka jana!
 
Haya sasa tuendelee na mengine, maana kwa sasa tayari Dr. Philip Mpango ameshajibu kuhusu kimya chake, kwa kutokeza hadharani.

Haya twendeni tukajenge nchi, huu mjadala umeshafungwa rasmi na hakuna tena kilichobaki nyuma kwenye mjadala wa kimya chake.

Ila katika hili, tujifunze kuwa na kiasi kwa kile tunachosema mitandaoni jata kama tunaona tuna uhuru wa kusema chochote kilicho kichwani.

Ova
 
Ni yeye kweli au ni mambo ya AI
 
Your browser is not able to display this video.


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amewashukuru Watanzania kwa kumuombea huku akibainisha kuwa alikuwa nje ya nchi kwa shughuli maalumu takribani mwezi mmoja.

“Asanteni sana kwa kuniombea, yamesemwa mengi si ndio? Na wengine bado wanasema mimi ni mzuka..

“Muwe na amani nipo salama nilikwenda nje kufanya shughuli malum takribani mwezi mmoja sijapungua hata kidogo si ndio?... Wapo wengi walioumizwa na maneno ambayo hayana msingi, wale waliokuwa wanatuma picha yangu na mshumaa pembeni…. wengine walisema mzee amekata moto…muda wangu bado,”amesema Dk Mpango.

Dk Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo Desemba 10, 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
 
Tundu Lissu anahisikiaje aisee?
 
Anyamaze, dunia ya sasa haina nafasi ya uongo.
Anaweza kutajiwa hosp. Alipokuwa anatibiwa, ugonjwa hata daktari wake.

Mambo mengine kama kiongozi unayanyamazia tu.

Ameahau corona ilivyomdhalilisha?
Yaani nyie mmzushie wee, halafu eti yeye anyamaze tu. Mbona nyie hamkunyamaza. Yamewashuka kabisa, mnakuja na makasiriko. Evil people, shame on you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…