Dodoma, Mbeya, Mwanza na Tanga sio majiji; zirudishwe kuwa halmashauri au manispaa

Hata mjinga huwacheka wajinga wenzie siyo tu kwasababu ya kufurahisha nafisi yake Bali kwa kutojua kiasi Cha ujinga wake yeye mwenyewe.
 
Ukitoka isanga unaenda iganzo njia ya chunya.
Wewe nae unatafutiza tu, sasa ukitoka Isanga vijiji vya milimani huko kuelekea chunya unavihesabia? Mbeya ni pazuri sana, mzunguko wa hela upo, system ya usafiri wa uma ni nzuri,

population kubwa kuna toto kali za kinyakusya black beauty halafu zina mizigo, mazao bei chee mahindi mengi na mchele wenye ubora na viazi vya kutosha, ndizi na maparachichi ni kama ya bure tu, hali ya hewa nzuri ya baridi safi kabisa.

Ukitaka kufaidi maisha kaishi Mbeya, huku Dsm mnateseka tu!

Au nasema uwongo Beesmom ?
 
No way .wew unataka tu battle na uchokozi Kwa mwanza...Hilo unalojua then maoni yako binafsi usilazimishe wengine waamini kama wew
 
Yaani msanii anapokelewa na raisi jamani duu yaani nchi za kiafrika
Michael Jackson kwa hadhi yake hata waziri haruhusiwi kumpokea. Unashangaa kupokewa na raisi, uingereza alipokelewa na malkia.

Uarabuni wafalme ndio walimpokea. Huyu jamaa alikuwa na nyota kali kuliko msanii yoyote aliyewahi kutokea Duniani hapa.

Akipanda stejini akijikuna tu watu wanashangalia na wengine wanapoteza fahamu na kuzima kabisa.

Acha kabisa ingekuwa ni miaka hii huyu jamaa sijui angekuwa na power ya aina gani imagine huo moto wake ni miaka ya 90 kurudi nyuma technology haikuwa kama hii leo.

Naomba nisiseme mengi sana maana nikikumbuka miaka ile namna tulikuwa tunavurugwa jamaa akitoa nyimbo. Nyimbo ikiwekwa kwenye redio unasikia shoti mwili mzima unatamani ucheze kama yeye unashindwa u abakia kuwa bwege tu umeuduwaa hujui la kufanya.

MUNGU amrehemu popote alipo i hope in the next life atarudi tena zaidi ya alivyokuja katika this life. Dah....

Michael Jackson yule mwamba acha tu aiseeeee.

Ngoja nipige kale kaukelele kake nijisikie vizuri kidogo.
... Hi Hiiiiiiiiii Shaaamonaaaa.... U ain't bad.... [emoji30]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana nae aendelee kulegeza mbupu huko na joto la kuzidi
 
Iganzo ni ndani ya mnachoita jiji na kuna watu wengi kama mchanga. Gharama za maisha ni kweli ziko chini sana lakini mbeya hakuna hadhi yoyote, maeneo mengi ni makazi holela.

Mzunguko wa fedha pale mbeya upo lakini ni ule wa hela ndogondogo. Maisha mbeya ni local sana, nimekaa miaka 16 pale.
 
ni kweli mkuu siku bby wangu alirudi akakuta imejengwa flyover alicheka sana akasema siyo flyover nnayoijua,umeongea ukweli
 
Tatizo kubwa la dar na miji mingi ya Tanzania Hamna public park, pedestrian walk watu wanashare na boda boda hivi hao watu wa ardhi ni kazi ipi wanafanya na kwanin wanalipwa mshahara
 
Kama vigezo vyako ni nyumba kutapakaa kama takataka na miundombinu hatarishi, basi hatuna jiji hata moja Tanzania
nami nakazia kwa vigezo vyake basi hatuna jiji hata moja Tanzania ya Tozo,
 
hata kama una usafiri binafsi foleni za magari unakaa hadi unasinzia,
Mbeya kuna foleni ya kijinga sana kuanzia ilomba mpaka mafiati.. yaani main road ya kuingia kwenye hicho kitu mnaita jiji ni single lane.. kilometer karibu tano ni foleni tupu.
 
Mbeya kuna foleni ya kijinga sana kuanzia ilomba mpaka mafiati.. yaani main road ya kuingia kwenye hicho kitu mnaita jiji ni single lane.. kilometer karibu tano ni foleni tupu.
Sasa si hapo tu, utalinganisha na dar kila kona foleni?
 
Jamaa yangu alikaa Bangkok miaka mitatu. Aliporudi bongo ndani ya dk 20 za kwanza akasema, "Kaka, mimi hapa ni nyumbani ila Michael Jackson hakukosea, tulimuona ana nyodo na mbwembwe ila kiuhalisia home pana harufu flani hivi, hewa flani nzito sana."

Mtoa mada ameshindwa kutofautisha vitu flani vichache. Kwa mawazo aliyonayo, akiishi mahali kama Tokyo, Paris and the alikes, hakuna nchi Afrika ataona ina hadhi ya kua na jiji hata moja.
 
Mtoa mada ameshindwa kutofautisha vitu flani vichache. Kwa mawazo aliyonayo, akiishi mahali kama Tokyo, Paris and the alikes, hakuna nchi Afrika ataona ina hadhi ya kua na jiji hata moja
Bangkok Thailand hawana cha kujivunia maana hata wao kuna harufu fulani ipo kila mahali nadhani inachangiwa na vyakula vyao. Nimekaa pale 2014 na nikagundua ile nchi imewekeza sana kwenye sekta ya misosi maana hata malls zao unakuta floor nne kati ya kumi ni biashara ya misosi. Ila ofcourse miundombinu yao ni next level. Kuna mpaka red tarmac roads ukiwa unatokea Suvarnabhumi airport na treni na boat kibao za mjini.

Nimekaa Switzerland ambako mpaka watu kutoka US wanapashangaa kwa uzuri na standard. Dubai pale nimekaa na ndio sehemu nimeona kuna maghorofa mengi sana mapya na ya kisasa. Ofcourse kwa international standards tz hamna jiji lolote. Ndio maana tunafananisha kwa hapa tz pekeake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…