Mambosasa Kwenye Sakata La MO Wakati Wa Utawala Wa Mzilankende Alimwambia
Wamemrudisha MO Na Hawajakamatwa Nakwambia Tanzania Siyo Ya Wajinga
Kwenye Hiyo Ajali Najua Watanzania WanAujua Ukweli Wote Muda Sana Walikuwa Wanashindwa Kusema Chochote Mpaka Walipopika Data Ndiyo Wanakuja Hadharani
USSR mbona unawaandama tena kwa hasira ndugu zako,ni baada ya fungu la pambio kufutwa au😂Watuwekee picha za tukio lao na sisi kina USSR tuweke zetu ili tujue mbivu na mbovu
Wewe ndiye mume wewe huyo mwanamke mnayesema amefariki ama mna undugu naye?We RPC ndio wa kupuuzwa kwa upotoshaji huu, hii taarifa ungemwandikia tu rais. kwanini plate namba ya hiyo gari imeondolewa kabla hata gari haijanyanyuliwa. Angalieni picha hapo kwenye tukio hakuna plate number. RPC na viongozi wako wa kitaifa nyie ni binadamu km huyo mama ambaye mmemficha na kwenda kumzika km mnyama ili kumlinda mpumbavu moja km Dugange. Dugange ni nani nchi hii mpaka serikali itumie nguvu kubwa kupotosha watanzania na kumdhalilisha mtanzania mwingine, yaani huyo mama aliyekuwa naye
Mama Rais wetu watu km hawa ndio watakupa wakati mgumu sana, watu wataichukia serikali yako. Watanzania siyo wajinga wanajua ukweli wote ndio maana walikuwa wa kwanza kutoa taarifa hii mtandaoni. We rais hushangai taarifa viongozi wako akiwepo huyo RPC walikata kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari mpaka habari ilipojulikana nchi nzima kuwa ni ya kweli na sasa anakuja RPC na taarifa za uwongo za kupotosha na yenye vitisho. Nchi hii ni ya wananchi na wana akili, Otieno asifikiri anawazidi watanzania akili kisa ana hako kacheo. Km Magufuli alifia madarakani, cheo gani haitapita? Mwe na utu.
Duh, yaani gari limeharibika vibaya hivyo sbb ya kukwepa boda eti na kugonga ukingo? Kweli? 🕵🕵🤔🤔🤔🤔🤔😏😏 Mmmhhh..!! ubongo, moyo, roho na macho yangu, vyote vimekataa, basi sawa..!!
Hujawahi kumiliki gari. Ukimiliki utagundua kuwa yale ni makaratasi tu
Na huyo mwanamke aliyekua nae ambapo inasemekana kafariki, vipi mbna hawatoi taarifa kumuhusu??Hii issue ukiitazama kwa makini naona kuna kitu serikali inaficha, na sijui wanafanya hivyo kwa manufaa ya nani.
Kama mtu kakosea awajibishwe lakini kumuacha ni sawa na kulea uozo kwa watendaji wa serikali, au labda wanasubiri atoke hospitali ndio hatua nyingine zifuate..
Vetting inashusisha Vingi mkuu ikiwemo tabia bianfsi za mtu.Vetting ya michepuko?
Tumewaachia Wanasiasa watuongoze, kila jambo wanatanguliza Siasa na kujuana.wapumbavu na wajinga sana wengi wao!!!!! pia hawana hofu kabisa PM mwenyewe ndiyo hivyo tena , ulimbukeni na ushamba unachangia pia
Ndiyo maana Siri nyingi za Nchi zinakuwa wazi kwa kwa kuwategea Viongozi Wanawake pamoja na huko kwenye Masanga yao 🙌Asilimia 95 % ya viongozi wa nchi za Kiafrika hawana maadili mazuri . Hii ni mpaka viongozi wa dini .
Ukitaka ujue hivyo fuatilia wanapokua kwenye safari au wakimbiza mwenge. Ni ama Rushwa sana , uzinzi sana, ulevi sana ,ushirikina sana,fitina sana na kujipendekeza sana.
Tuna baadhi ya viongozi wasiofaa hata kuongoza nguruwe .
View attachment 2604901
JESHI la Polisi nchini limesema ajali iliyotokea Aprili 26, 2023 ikimuhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dk Festo Dugange ilisababishwa na Bodaboda aliyekuwa akivuka barabara ghafla bila kuchukua tahadhari.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Martin Otieno imesema gari hilo lenye usajili wa T 454DWV aina ya Toyota Land Cruiser likiendeshwa na Naibu Waziri Dugange lilipoteza mwelekeo na kugonga kigo ya barabara ya Iyumbu maeneo ya St Peter Clever na kupinduka.
“Kulikuwa na mtu moja tu (dereva) kwenye gari hilo ambaye ni Naibu Waziri. Alivunjika kidole gumba cha mkono wa kulia na kupata majeraha katika mkono huo,” amesema Kamanda Martin.
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amemjulia hali Dk Ndugage ambaye amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Doodma.
Ehh.. povu lote lile kweli!?? 🤣🤣😔😔View attachment 2604901

Pia, soma: Dodoma: Naibu Waziri wa TAMISEMI Festo Dugange apata ajali akiendesha gari