View attachment 2604901
JESHI la Polisi nchini limesema ajali iliyotokea Aprili 26, 2023 ikimuhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dk Festo Dugange ilisababishwa na Bodaboda aliyekuwa akivuka barabara ghafla bila kuchukua tahadhari.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, ACP Martin Otieno imesema gari hilo lenye usajili wa T 454DWV aina ya Toyota Land Cruiser likiendeshwa na Naibu Waziri Dugange lilipoteza mwelekeo na kugonga kigo ya barabara ya Iyumbu maeneo ya St Peter Clever na kupinduka.
“Kulikuwa na mtu moja tu (dereva) kwenye gari hilo ambaye ni Naibu Waziri. Alivunjika kidole gumba cha mkono wa kulia na kupata majeraha katika mkono huo,” amesema Kamanda Martin.
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amemjulia hali Dk Ndugage ambaye amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Doodma.