Population sio kigezo cha ubora wa mji unaweza kuwa na population kubwa lakini mipangomiji+huduma za kijamii mbovu mfano jiji la Windhoek Namibia lina population ya watu lakisita tu lakini limeizidi mbali sana Dar Es Salaam yenye wakazi zaidi ya milioni 5. Kwa kukusaidia tu mji wa Dodoma umeanza kupangiliwa tangu enzi za Nyerere/CDA hiki unachokiona kwa sasa ni mwendelezo wa master plan iliyoanza kuratibiwa tangu miaka ya 1970 sasa imagine miaka 10 ijayo itakuaje Dom,Kiukweli miji mingine inabidi ikajifunze DomNa huo wingi wa watu ndio turufu ya kupanua mji! Mipango miji ya Mwanza ukiiangalia kwa kupitia milimani utaona haijapangwa lakini sasa hivi kwenye tambarare za Mwanza mji unapangwa unapangika. Tembelea Malimbe, Nyegezi, njia ya airport ukiwa unaelekea Kayenze, angalia kote huko Buswelu, Nyamhongolo, Kisesa n.k. huwezi kukuta slums tena! Lami kote huko zinamea! SGR pale mjini iko inaendelea. Ngoja tusubiri hiyo 10 years kama Dodoma atatoboa!
Ukavu ni nature ya jiji lenyewe, pale ni semi desert na huwezi badili hiliDodoma Kwenye Miundo mbinu Wamejitahidi,Ila Changamoto ya Dodoma Ni kukavu Balaa
Na huo ndio ukweli mchungu Dodoma wanapendelewa sana mfano mdogo tu angalia mtandao wa barabara za lami kilasiku wanaongeza ndiomana makampuni makubwa ya ujenzi wa barabara karibia yote yamehamishia ofisi zao Dom kwasababu wana uhakika na miradi inayokuja mbeleni.State Capital City utaifananishaje na Mwanza kwa baadae mzee?
Miradi na privileges nyingi zinakuwa channelled Dodoma.
Hapana,Tanzanite Bridge Posta.
Tunajua Tanzanite ni madini yanapatikana Arusha, sasa kuna Tanzanite inachimbwa pale Selandar kwenda Agha Khan Hospital?
Upo sahihi mkuu, Dar ni kachumbari, uchafu na uzuri umewekwa eneo moja.Mtoa mada nakuunga mkono asilimia 700....
Dodoma kwa sasa ndio mji unaofuatia kwa kupangwa vyema baada ya mkongwe Tanga....
Katika jambo muhimu serikali walifanya ni kutoivunja CBD pamoja na mazongezonge yake....
Majiji mengine yameendelea sana ila kipengele kikuu ni upangaji wa mji.
Kwa kuwa mimi ni mkazi na mwenyeji wa Dar hebu nikupe mifano kadhaa...
Hizi ni sehemu zilizojitahidi kupangwa.
1. Posta ambayo ukitoka posta juu kuna osterbay chini kuna kurasini then mbagala hebu angalia hali ya kurasini ni hovyo sana licha ya kuwa mji wa serikali na upo karibu na bandari gusa mbagala ni janga makazi hayajapangwa.
2. Kariakoo ukitoka unaingia buguruni huku jangwani ni balaa.
3. Masaki ukitoka msasani hii hapa
4. Osterbay msasani hii hapa.
5. Mikocheni iliyopangwa ni mikocheni B ambayo mwenzake ni mikocheni A ambayo ukiingia kita 50 kutoka barabarani ni uchafu tupu. Ukipandisha kuelekea kawe ni balaa.
6. Sinza
7. Mbezi
8. Mbweni
yani Dar es salaam ni mji wa biashara ila kwenye kupanga mji tumefeli vibaya sana.
Tabata ni mji wa 90's lakini barabara haieleweki...
Dar ukiacha hela na biashara ni uchafu
2.
Kwaabadae Mwanza hasogelei Dodoma, wawekezaji wanaangalia Serikali inafavor eneo gani in terms of infrastructure and easy accessibility with government entities. Mwanza hana hii privilege Dodoma anayo.Kumbuka Dar na Mwanza ni Majiji ya Kibiashara. Capital city inakuwa na majengo mengi ya taasisi. Mara nyingi Majiji ya kibiashara ndiyo yanakuwa maarufu zaidi ya Capital city! Hiki ndicho kinanipa uhakika Dodoma haitakaa iipiku Mwanza au Dar. Maana kama magorofa makubwa hata Mwanza yaoo yanajengwa, vyuo vikki vinajengwa kama uyoga. Hotel ya Nyota ipo ya nssf inajengwa pale karibu na chuo cha bot
Watu wa mbeya na dodoma sijui wanashida gani... Na asilimia 99% ya wamiliki wa ghorofa ni wageni 😂Hii ni kwa waliofika mitaa ya ushuani Dodoma kwa hivi karibuni.
Naishi dsm, lakini nimeishi dodoma 5 years back, nimekaa Arusha na Mwanza pia.
Sikatai Dar ndio baba lao kwa Tz kwenye vitu vizuri hasa Makazi.
Kama umefika Dodoma hivi karibuni au hata kuangalia insta, Tiktok utaona real estate ya Dodoma inakuja kwa kasi mno hata Dar ikasome kuanzia Apartments, hotels, AirbnB etc
Hizi ni baadhi ya sehemu ambazo ukitembelea utakubaliana na mimi.
1. Itega - ianshika namba moja kwa Dodoma, wanaishi wazito huu mtaa uliopo chini ya mlima kama unaenda gereza la isanga. Sharti la kujenga ni kuanzia ghorofa moja, kiwanja kuuzwa 1 billion sio jambo la kushangazwa kutokana na value ya eneo na kumepangwa kweli kweli hiyo Mijengo Mbweni JKT akasome.
2. Njedengwa- naipa namba mbili, huu mtaa upo chini ya mlima kama unaenda iyumbu kule Udom. Kuna makazi ya watu, taasisi za umma na binafsi kama Tume ya Uchaguzi HQ. Huku kuna balaa watu wamejenga hadi unasema pesa wamepata wapi. Kwa kuongezea kuna Hotel Mbili za Nyota tano zinajengwa, ile ya Bunge la Afrika kushirikiana na Bunge Tz pamoja na ile ya NSSSF ili kuendana na kasi ya Jiji lakini kuhost diplomats, UN guests and high profile foreigners watakao kuwa dodoma msalato international airport ikikamilika.
3. Mkalama/ Makulu Oyster bay
Huu mtaa una washua balaa, kina Biteko etc wameshusha vitu na apartments zile za modern luxury zinajengwa na zingine zipo tayari.
4. Ilazo - kumenyooka huku hamna slums ni vitu fulani hivi vya kishua na barabara kiwango cha lami kwenye mitaa yake.
5. Medeli - Huku ndio kuna shopping malls, restaurants, ofisi za umma na bifnafsi na hotels za kisasa, in short panakuwa kwa kasi sana. Kiwanja kuuzwa 2 billion sio maajabu huu mtaa.
6. Kisasa- huku ni kama Sinza ya Dar, kumechangamka sana yaani ni mtaa unajitosheleza karibia kila kitu, tofauti na sinza huku hamna slums, kumepangwa vizuri barabara za mtaa almost zote zina lami.
7. Mlimwa C - huku ndio kule kwa Waziri Mkuu, chini ya mlima watu wanashusha mansion kama uyoga ndipo kuna royal village.
8. Mtumba City - kwasasa kuna modern state of art ministerial offices, ila kwa baadae patakuwa kufuru kutokana na modern hotels, restaurants and apartments ambazo zipo underway.
Sehemu zingine kuna Iyumbu, Ntyuka, Tambuka reli street etc
Dodoma Uncle magu angekuwepo sijui tungekuwa tunaongea nini.
Kwasasa ndio Jiji la tatu linalokuja kwa kasi baada ya Dar na Mwanza, hivyo Mwanza kaa tayari kushika namba tatu by 2030
Oyster Bay ni maneno mawili ya Kiingereza yenye maana maalum.Neno kuwa tusi ni suala la Context tu.
Kuna ukoo wa Wachagga unaitwa MBORO, na hawaoni shida kwasababu kila lugha/neno yana context yake. A word can have hundreds of meanings depending on context and usage.
Wewe pia hoja yako ni MFU.Hapana,
Mfano wako ni mbaya.
Kwanza hilo ni jina la daraja, daraja la Nyerere maana yake pale ndipo alipozaliwa Nyerere? Pale ni nyumbani kwa Nyerere?
Daraja la Golden Gate California linabeba sifa ya California kuwa jimbo lililochimba dhahabu sana, kama daraja la Tanzanite linavyobeba jina la Tanzania kuchimba Tanzanite sana.
Oysterbay ni sehemu iliyo baharini, yenye ghuba, yenye chaza au historia ya kuwa na chaza.
Oysterbay zipo nyingi duniani.
Kuna Oysterbay New York, US, ipo baharini.
Kuna Oysterbay Alabama, US, ipo baharini.
Kuna Oysterbay, New South Wales, Australia, ipo baharini.
Kuna Oysterbay, Eastern Cape, South Africa, ipo baharini.
Kuna Oysterbay, Trelawny, Jamaica, ipo baharini.
Kuna Oysterbay, Rodrigues, Mauritius, ipo baharini.
Kuna Oysterbay, Northern Mariana Island, ipo baharini.
Kuna Great Oyster Bay, Tasmania, Australia, ipo baharini.
Dunia nzima wanajua Oysterbay ni sehemu iliyo baharini.
Ni huko Tanzania ushamba wenu tu.
View attachment 3632548
Kwanini uite sehemu Tanzanite wakati hakuna madini sehemu hiyo zaidi ya bahari?Oyster Bay ni maneno mawili ya Kiingereza yenye maana maalum.
Ghuba ya Chaza.
Sasa kwa nini mnalazimisha sehemu ambayo haina bahari, haina ghuba, haina chaza, kuitwa Oysterbay?
Kwani hamna majina mengine?
Majina yameisha mpaka mchafue maana ya majina ya watu kwa ushamba wenu?
Dar es Salaam pia, wenye maendeleo ni wageni, wazaramo wanajua vigodoro na shughuli. 😂Watu wa mbeya na dodoma sijui wanashida gani... Na asilimia 99% ya wamiliki wa ghorofa ni wageni 😂
Tanroads wanavyojenga barabara Dar sio kabisa! unakuta sehemu barabara ya lami kilomita kadhaa lakini hakuna sehemu ya watembea miguu wala Vyombo ya kutupa taka na pia sehemu za kupaki magari yani kumejengwa bila mpangilio wowote! Sasa Dodoma kuna jaribu kurekebisha mistake iliyofanya Dar.Dodoma ni Modern City, Dar ni old city with modern buildings and slums kitu ambacho dodoma hakipo.
Pia, Dar kunanuka sana jamani, hakujapangwa kuanzia makazi, barabara hamna hata city parks?
Nimekueleza kuwa kuna daraja la Golden Gate huko San Francisco California, linawakilisha jimbo la California kuwa jimbo lenye historia ya kuchimba dhahabu.Wewe pia hoja yako ni MFU.
Unasema jina la mahali inabidi lisadifu yaliyomo, sasa Tanzanite Bridge linasadifu eneo la hapo Posta?
Kwasababu Tanzanite ipo Arusha Mererani sio Posta.
Hakuna sehemu iliyoitwa Tanzanite, kuna daraja limeitwa Tanzanite.Kwanini uite sehemu Tanzanite wakati hakuna madini sehemu hiyo zaidi ya bahari?
Ndio maana wazaramo zikianzag story za pesa na matajiri wa dar utashangaa huwaoni au wanakaa kimya 😂Dar es Salaam pia, wenye maendeleo ni wageni, wazaramo wanajua vigodoro na shughuli. 😂
Kwasasa ni administrative, kwa mbele itakuwa ni both administrative and commercial, unajua kwanini?Look Johannesburg vs Pretoria and Capetown, look Lagos vs Abuja , look New York vs Washington DC, look Shanghai and Guangzhou vs Beijing. Kuna miji inakua kibiashara na mingine political and admistrative. Look kahama vs shinyanga. Dodoma inakuwa admistrative but not commercially like dar es salaam.
Hakuna sehemu inayoitwa Tanzanite, kuna daraja linaitwa Tanzanite.Kwanini uite sehemu Tanzanite wakati hakuna madini sehemu hiyo zaidi ya bahari?
Ni kweli Mkuu,Tanroads wanavyojenga barabara Dar sio kabisa! unakuta sehemu barabara ya lami kilomita kadhaa lakini hakuna sehemu ya watembea miguu wala Vyombo ya kutupa taka na pia sehemu za kupaki magari yani kumejengwa bila mpangilio wowote! Sasa Dodoma kuna jaribu kurekebisha mistake iliyofanya Dar.
Mimi nakueleza ipo sehemu Posta inaitwa Tanzanite, nikimwambia Boda ananipeleka, sasa wewe unapinga nini?Hakuna sehemu inayoitwa Tanzanite, kuna daraja linaitwa Tanzanite.
Ukiwa hujui hilo, huo nao ni ushamba mwingine.
Hata ikiwapo sehemu inaitwa Tanzanite si tatizo.Mimi nakueleza ipo sehemu Posta inaitwa Tanzanite, nikimwambia Boda ananipeleka, sasa wewe unapinga nini?
Daraja sio sehemu? Unaelewa sehemu ina maana gani? Pengine una myopia ya lugha.