Hii ni kwa waliofika mitaa ya ushuani Dodoma kwa hivi karibuni.
Naishi dsm, lakini nimeishi dodoma 5 years back, nimekaa Arusha na Mwanza pia.
Sikatai Dar ndio baba lao kwa Tz kwenye vitu vizuri hasa Makazi.
Kama umefika Dodoma hivi karibuni au hata kuangalia insta, Tiktok utaona real estate ya Dodoma inakuja kwa kasi mno hata Dar ikasome kuanzia Apartments, hotels, AirbnB etc
Hizi ni baadhi ya sehemu ambazo ukitembelea utakubaliana na mimi.
1. Itega - ianshika namba moja kwa Dodoma, wanaishi wazito huu mtaa uliopo chini ya mlima kama unaenda gereza la isanga. Sharti la kujenga ni kuanzia ghorofa moja, kiwanja kuuzwa 1 billion sio jambo la kushangazwa kutokana na value ya eneo na kumepangwa kweli kweli hiyo Mijengo Mbweni JKT akasome.
2. Njedengwa- naipa namba mbili, huu mtaa upo chini ya mlima kama unaenda iyumbu kule Udom. Kuna makazi ya watu, taasisi za umma na binafsi kama Tume ya Uchaguzi HQ. Huku kuna balaa watu wamejenga hadi unasema pesa wamepata wapi. Kwa kuongezea kuna Hotel Mbili za Nyota tano zinajengwa, ile ya Bunge la Afrika kushirikiana na Bunge Tz pamoja na ile ya NSSSF ili kuendana na kasi ya Jiji lakini kuhost diplomats, UN guests and high profile foreigners watakao kuwa dodoma msalato international airport ikikamilika.
3. Mkalama/ Makulu Oyster bay
Huu mtaa una washua balaa, kina Biteko etc wameshusha vitu na apartments zile za modern luxury zinajengwa na zingine zipo tayari.
4. Ilazo - kumenyooka huku hamna slums ni vitu fulani hivi vya kishua na barabara kiwango cha lami kwenye mitaa yake.
5. Medeli - Huku ndio kuna shopping malls, restaurants, ofisi za umma na bifnafsi na hotels za kisasa, in short panakuwa kwa kasi sana. Kiwanja kuuzwa 2 billion sio maajabu huu mtaa.
6. Kisasa- huku ni kama Sinza ya Dar, kumechangamka sana yaani ni mtaa unajitosheleza karibia kila kitu, tofauti na sinza huku hamna slums, kumepangwa vizuri barabara za mtaa almost zote zina lami.
7. Mlimwa C - huku ndio kule kwa Waziri Mkuu, chini ya mlima watu wanashusha mansion kama uyoga ndipo kuna royal village.
8. Mtumba City - kwasasa kuna modern state of art ministerial offices, ila kwa baadae patakuwa kufuru kutokana na modern hotels, restaurants and apartments ambazo zipo underway.
Sehemu zingine kuna Iyumbu, Ntyuka, Tambuka reli street etc
Dodoma Uncle magu angekuwepo sijui tungekuwa tunaongea nini.
Kwasasa ndio Jiji la tatu linalokuja kwa kasi baada ya Dar na Mwanza, hivyo Mwanza kaa tayari kushika namba tatu by 2030