Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Na huo wingi wa watu ndio turufu ya kupanua mji! Mipango miji ya Mwanza ukiiangalia kwa kupitia milimani utaona haijapangwa lakini sasa hivi kwenye tambarare za Mwanza mji unapangwa unapangika. Tembelea Malimbe, Nyegezi, njia ya airport ukiwa unaelekea Kayenze, angalia kote huko Buswelu, Nyamhongolo, Kisesa n.k. huwezi kukuta slums tena! Lami kote huko zinamea! SGR pale mjini iko inaendelea. Ngoja tusubiri hiyo 10 years kama Dodoma atatoboa!
 
Hapo umenipata,sasa ukiwa unapita hiyo road ya Chinangali kuelekea Wajenzi,kushoto kwako ndo kuna Area A na Chamwino. Siku moja utembee kwa miguu ukipata nafasi,nyumba zimepangika ila zimechoka haswaa, ni za urithi warangi wanaishi humo tangu enzi.
Nitapita siku nikija dodoma, nina list ndefu ya sehemu za kutembelea sijui kama nitamaliza
 
Na hii ndio sababu nimesema Dodoma ni modern city kuliko yeyote Tanzania. Majengo yote ni mapya na modern kwasababu maeneo yale ya wazi ndio yanajengwa, sehemu chache sana unaweza kuona slums kwa bahati mbaya.
Dar ni kama kachumbari, mijengo mibovu imechanganyika na mijengo mizuri kitu kinachoharibu view, pia hizo slums za buguruni, kipawa, buza, goms etc wafanya mpango wa total demolition of slums na kuweka modern buildings.
 
Balozi kuhamia Dodoma ni suala sio immediate linahitaji kwanza availability ya international standards kwa Dodoma kitu ambacho bado hakijafikiwa kwa Dodoma, ikiwemo International Airport and Five star hotels. Ni jambo la muda.

Lakini pia, balozi zinapaswa kuwa na budget ya kuhama.

Serikali hii ni kweli inakwamisha kuifanya dodoma capital city, Mahakama na Bunge wameweza hili isipokuwa executive. President ajaye asitokee Coastal hawa wana ubinafsi na Dodoma, bila Magu sijui ingekuwaje.

All in all, kasi ya Dodoma kukua ni kubwa sana, Mwanza hatoboi in few years, Take my word.
 
Nakuelewa hoja yako.

Pengine waliiga jina kutokana na Serene and tranquil neighbourhood not necessarily reflecting etymology ya Neno "Oyster Bay"
 
Population sio kigezo cha ubora wa mji unaweza kuwa na population kubwa lakini mipangomiji+huduma za kijamii mbovu mfano jiji la Windhoek Namibia lina population ya watu lakisita tu lakini limeizidi mbali sana Dar Es Salaam yenye wakazi zaidi ya milioni 5. Kwa kukusaidia tu mji wa Dodoma umeanza kupangiliwa tangu enzi za Nyerere/CDA hiki unachokiona kwa sasa ni mwendelezo wa master plan iliyoanza kuratibiwa tangu miaka ya 1970 sasa imagine miaka 10 ijayo itakuaje Dom,Kiukweli miji mingine inabidi ikajifunze Dom
 
Tatizo huyu Ngosha anaiona Dodoma ilivyo sasa, haioni Dodoma ya miaka 5 -10 mbele. Atashangaa!

Nakumbuka 2010-2015 ukimwambia mtu anunue ardhi dodoma anakucheka, hapo Makulu Oyster bay kwa Biteko, kulikuwa mapori na vichaka, wanachuo wa Udom walikuwa wanakataa kununua ardhi kwa laki moja.
Sasa hivi hupati ardhi hapo bila 30 million kwenda juu.
 
Masaki sioni tatizo.

Masaki ipo Kisarawe, ikaletwa mpaka Dar es salaam.

Kama ni jina tu hakuna tatizo.

Tatizo naliona kwa Oysterbay, kwa sababu hilo si jina tu, ni jina kenye maana maalum.

Ghuba ya Chaza. Sehemu ya bahari yenye ghuba na chaza.

Sasa Arusha, Dodoma au Kigoma kunawezaje kuwa na ghuba ya chaza?
 
State Capital City utaifananishaje na Mwanza kwa baadae mzee?
Miradi na privileges nyingi zinakuwa channelled Dodoma.
 
Nakuelewa hoja yako.

Pengine waliiga jina kutokana na Serene and tranquil neighbourhood not necessarily reflecting etymology ya Neno "Oyster Bay"
Sawa,

Sasa unapoiga jina unatakiwa kujua maana ya jina, si unaigaiga tu. Utaiga matusi.

Serene and tranquility does not need to be Oysterbay. Kwani hakuna majina ya lugha ya kiasili yanayomaanisha hivyo?
 
Mtoa mada nakuunga mkono asilimia 700....

Dodoma kwa sasa ndio mji unaofuatia kwa kupangwa vyema baada ya mkongwe Tanga....

Katika jambo muhimu serikali walifanya ni kutoivunja CBD pamoja na mazongezonge yake....

Majiji mengine yameendelea sana ila kipengele kikuu ni upangaji wa mji.

Kwa kuwa mimi ni mkazi na mwenyeji wa Dar hebu nikupe mifano kadhaa...

Hizi ni sehemu zilizojitahidi kupangwa.

1. Posta ambayo ukitoka posta juu kuna osterbay chini kuna kurasini then mbagala hebu angalia hali ya kurasini ni hovyo sana licha ya kuwa mji wa serikali na upo karibu na bandari gusa mbagala ni janga makazi hayajapangwa.

2. Kariakoo ukitoka unaingia buguruni huku jangwani ni balaa.

3. Masaki ukitoka msasani hii hapa
4. Osterbay msasani hii hapa.
5. Mikocheni iliyopangwa ni mikocheni B ambayo mwenzake ni mikocheni A ambayo ukiingia kita 50 kutoka barabarani ni uchafu tupu. Ukipandisha kuelekea kawe ni balaa.

6. Sinza
7. Mbezi
8. Mbweni

yani Dar es salaam ni mji wa biashara ila kwenye kupanga mji tumefeli vibaya sana.

Tabata ni mji wa 90's lakini barabara haieleweki...

Dar ukiacha hela na biashara ni uchafu

2.
 
State Capital City utaifananishaje na Mwanza kwa baadae mzee?
Miradi na privileges nyingi zinakuwa channelled Dodoma.
Kumbuka Dar na Mwanza ni Majiji ya Kibiashara. Capital city inakuwa na majengo mengi ya taasisi. Mara nyingi Majiji ya kibiashara ndiyo yanakuwa maarufu zaidi ya Capital city! Hiki ndicho kinanipa uhakika Dodoma haitakaa iipiku Mwanza au Dar. Maana kama magorofa makubwa hata Mwanza yapo yanajengwa, vyuo vikuu vinajengwa kama uyoga. Hotel ya Nyota ipo ya nssf inajengwa pale karibu na chuo cha BOT
 
Sawa,

Sasa unapoiga jina unatakiwa kujua maana ya jina, si unaigaiga tu. Utaiga matusi.

Serene and tranquility does not need to be Oysterbay. Kwani hakuna majina ya lugha ya kiasili yanayomaanisha hivyo?
Neno kuwa tusi ni suala la Context tu.

Kuna ukoo wa Wachagga unaitwa MBORO, na hawaoni shida kwasababu kila lugha/neno yana context yake. A word can have hundreds of meanings depending on context and usage.
 
Dodoma itakuwa second largest city by 2030, huko mbeleni watakuwa wanafukuzana na Dar.
Look Johannesburg vs Pretoria and Capetown, look Lagos vs Abuja , look New York vs Washington DC, look Shanghai and Guangzhou vs Beijing. Kuna miji inakua kibiashara na mingine political and admistrative. Look kahama vs shinyanga. Dodoma inakuwa admistrative but not commercially like dar es salaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…