Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

Tz bhana, eti mtu kama huyu ndiye anatarajiwa ku discuss juu ya maendeleo ya Taifa ikiwemo matumizi ya new technology na Tz kuja kurusha chombo chake mwezini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ccm oyeeee oyeeeeeeeee......
 
Halafu anataka arudi jimboni na mapesa ili akawaringishie wananchi wa jimbo lake au? Ndicho wananchi walichomtuma? Shubamiti zake.
 
Aache Ubunge akajiajiri... Kench taip
 
mjinga sana h
uyo
mjinga sana huyo mbunge mbona hawatetei watumishi wa umma ambao wanaishi kwa shida na mishahara yao hata haiwafikishi mwisho wa mwezi.halafu yeye na wenzake wanataka iongezeke tena ilipwe kwa dola.afrika kusini,kenya je uchumi wao uko sawa na wa tanzania.hao ndiyo wabunge wanafiki ambao wananchi tunapaswa kuwa nao makini.wao waongezewa wengine kodi ya PAYE juu halafu wao hamna kodi wanayokatwa je huo siyo usaliti kwa wananchi?anasema wanaowashambulia ni wa mitandaoni tu lkn si wananchi,je kuna utafiti gani alioufanya kuwa wananchi wanariddhia jambo hilo.wacha nao wasage benki ili akili ziwasogee.
 

Halafu kibaya zaidi wengine ni 7 ya msukuma
 
Ni kweli kabisa. Nafasi za ukuu wa Mkoa na wilaya zingefutwa na ubunge ukawa wa kujitolea tu kama udiwani upumbavu kama huu tusingeusikia. Alaaniwe dhalim kwa kutuharibia mfumo wa utawala katika nchi yetu
 
Kama ela haitoshi abeti ataongeza kipato ila ajue sisi wengine hata tuishi miaka 200 hatutarajii kuingiza kipato anachokipata kwa mwaka mmoja tu
 
Atakuwa mutheing huyu
 
Watu wanalipwa laki sita na kodi wanalipa yy anachukua mshahara huo hata kodi halipi halafu analeta Maneno ya ajabu kabisa nashauri apimwe akili
 
Ni ombi lilioshangiliwa sana bungeni baada ya kutolewa na Mbunge wa Mbogwe akiwa amevaa suti ya ki-kongo, alisema mengi na nimeona mambo kadhaa:

1. Alishangiliwa na Bunge zima
2. Naibu spika naye aka-smile kwa wema wa mbunge
3. Mifano ya kuigwa ni nchi za Kenya na Afrika ya kusini
4. Anaomba walipwe kwa dola
5. Anaomba wabunge wasiwaogope wananchi

Wana JF hili linahitaji mjadala. Mbunge asiyewaogopa wananchi anawezaje kulisaidia taifa? Mifano ya malipo ya wabunge bila kutoa mifano ya malipo ya waalimu, madaktari, n.k anawasaidia nini wa-TZ? Binafsi nahisi ni ombi la makusudi, la kutengeza ndani ya Bunge na kumsukumia mmoja wao mwenye akili za hivyo, aseme.

Hofu yangu ni udhaifu wa rais wetu ambaye katika kutafuta support ya chama aonekane ni mwema kwa wenzake wa CCM, tutajikuta wameongezwa kimya kimya.
 
Siyo makosa yake! Alipewa ubunge bure anastahili kudai posho ziongezwe.
Hajui gharama za kupata ubunge kwenye sanduku la kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…