Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Wakuu amani kwenu, wazungu wanamsemo wao mzuri tu kuwa "he who has a gold makes the rules" Jana wakati wa siku ya walimu rais Magufuli alipiga simu kukanusha katazo la kuendelea kwa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti kwa kile alichodai kuwa ni tangazo la kipumbavu.

Sasa kulingana na tatizo la ajira lilipo na mabadiliko ya kimfumo ya dunia, elimu ya cheti katika elimu yeti inapwaya, hivyo nature imekataa kuukubali hivyo no hero walimu wa cheti mlioko makazini na ambao mnategemea kuajiriwa mkarudi shule haraka.

The lost, kwa sasa Tallin, Estonia.
 
Taasisi ziko huru, zinapofanya vizuri always no changamoto but wanapoleta taharuki shida inakuwa kubwa ndo hapo anapoweza hitaji kupata briefing kutoka kwa Waziri au KM. Siyo kila kitu Lazmi ajue. Kinapoleta taharuki as now baba ndo anaibuka kuonyesha uwepo wake
Ndani ya ilani ya CCM imeandikwa, je Magufuli hajaiona na bado anainadi kwa nguvu zake zote!
 
duh, sometimes viongozi wetu muwe na busara.....sio sawa kusema ni tamko la KIPUMBAVU....bad, mbaya mno....na waliokaa na kuamua hayo, walishindwa kutambua ni kipindi cha kampeni.....naipenda TANZANIA....
 
duh, sometimes viongozi wetu muwe na busara.....sio sawa kusema ni tamko la KIPUMBAVU....bad, mbaya mno....na waliokaa na kuamua hayo, walishindwa kutambua ni kipindi cha kampeni.....naipenda TANZANIA....
Mpumbavu keshatumbuliwa. Huyu na familia yake hawapigi Kura.
 
Leo tarehe 5 Oktoba, katika Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani lililoandaliwa na CWT, Dodoma, Rais John Pombe Magufuli alipiga simu 'live' na kuongea na washiriki wa kongamano na pia kukanusha kufutwa kwa ualimu wa ngazi ya cheti.

Rais Magufuli amewataka walimu kupuuza taarifa hiyo na kusema kuwa tangazo hilo ni la kipumbavu na kwamba ataendelea kuwa pamoja na walimu wote.


PIA SOMA: Siku ya Mwalimu Duniani: Wizara ya Elimu yafuta rasmi mafunzo ya Ualimu wa shule ya msingi na awali ngazi ya Cheti Tanzania


Ingependeza Wizara ya elimu ikaongozwa na walimu badala ya kuongozwa na watu wasio na ualimu
 
Hivi hadi katibu mkuu wizara anatoa tamko inamaana alijitolea tuu au lilikuwa kwenye mpango linafahamika na waziri wake pamoja na baraka la baraza la kawazidi? Na kama alijitolea mwenyewe tu je kuna mangapi maamuzi yamefanyika kwa utashi tu wa mtu?

Kuwaambia watu wapuuze nadhani ni kosa kubwa lakiufundi kwenye utendaji mzima hakuna credit yoyote unayopata zaidi yakupoteza point


Hili linafanana sana na alivyofanya Mungai alipofuta masomo ya kilimo, ufundi na biashara kwenye mashule ya sekondari ati kwasababu tu ilikuwa vigumu kuwapata walimu wa kufundisha masomo hayo
 
Ipo mifano mingi inayoonesha ubingwa wa kutengeneza matatizo kisha kuyatatua ili aonekane ni mwema.

Suala la kufuta mtaala wa ualimu ngazi ya cheti si suala dogo la kuamliwa na naibu katibu mkuu bali ni la wizara nzima na serikali kwa ujumla. Sasa kitendo cha kutengua uteuzi wa Avemaria si cha kiungwana bali amekuwa kama mbuzi wa kafara.

Raisi Magufuli ulisema, "Watanzania sio wajinga" na kweli sio wajinga, tunajitambua na tunajua kutofautisha mbivu na mbichi.

Miaka mitano ya uongozi wako ndiyo tunayoitumia kukutathmini ili tukuongezee mingine au tumpe mwingine. Tukutane oktoba 28.
 
Unamwita daktari mpumbavu? jamani? unafuta kwa kauli tu? hapana si sawa! mamlaka zikanushe kwa tangazo na waweke saini kama alivyofanya Dkt Ave
 
Kuna watu niliwasikia huko kwenye siri-kali kwamba wenye shahada wafundishe kuanzia shule za msingi kuboresha elimu, leo hii bwana nanihii anakuja ku-defend elimu ya cheti kisa mke wake ni wa cheti, sasa unajiuliza kwani mke wake ndo standard ya ubora wa elimu hapa nchini.
 
Rais Magufuli amewataka walimu na watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa zinazodai kwamba serikali imefuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa shule za msingi na awali, na kwamba mafunzo hayo sasa yataanzia ngazi ya Diploma...
Sasa wale walimu 350 na wakuu wa vyuo 18 walipewa mafunzo ya nini? na walilipwa posho na nani? jamani Daktari Ave ametolewa kafara tu! huo ndio ukweli, na hapa kura za walimu hao wenye cheti ndio zinatafutwa. Ajira za kura za walimu shule ya msingi utapambanishaje mwenye degree na cheti katika shule ya msingi!
 
Huyu hapati kura yangu, ni miaka mitano sasa ninasubili mshahara Mpya, hata ile annual increment imekuwa shida. Kura yangu ni kwa Lissu tu.
Mimi mwenzio kura yangu ni kwa JPM
 
Kiki ya kijinga.Hiyo ni sera na haikutungwa na mmoja. Kuitangaza si kuwa yeye ndo mwasisi. Yale yale ya kikokotoo. Wajinga watadanganyika.
 
3222EF0D-0331-4873-A4E3-ACBB977DD062.jpeg
 
Back
Top Bottom