DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa na fahamu na sasa anapelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
======
Taarifa zote za uhakika tutakuwa tunazitoa kila baada ya muda mfupi...
Picha HELKOPITA iliyombeba Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ikiwa angani kuelekea Nairobi
View attachment 583481
Mungu ataonekana tena katika maisha ya lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
namuombea mh Tundu lissu apone japo nilitaman kuona pale alipojeruhiwa...
 
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa na fahamu na sasa anapelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
======
Taarifa zote za uhakika tutakuwa tunazitoa kila baada ya muda mfupi...
Picha HELKOPITA iliyombeba Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ikiwa angani kuelekea Nairobi
View attachment 583481
Pole sana. Mungu atakuponya,
 
Unyama huu ni ktendo klchopangwa na lengo n kutoa uhai wake akka mungu ndo anaejua uhai wa mtu, na hao wanafk wanaoanza kutoa salam za pole n unafk mtu hao ndo wapangaj wa shambulio hilo, na mungu hakka atawaumbua. Hakka uongozi wenu hautakubalka na jamii, mtalaaniwa na mwsho wenu n mbaya,nyie endeleen na utawala wenu wa kdkteta uchwara, jiulzen gadafi yuko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwe mwema usiwe mwema mauti hayakwepeki.
 
Kwanza, sisi ni binadamu ambao hapa duniani hatutakuwepo milele na hivyo tunapita. Hapa tu safarini. Tutendeane na kusemeana yaliyo mema. Sote tu safarini.
Hatuna haja ya kusakana na kushambuliana kwa mijadala tu.

Pili,amani na utulivu tulionao kama nchi ni zao la utawala wa sheria na kusikilizana;tukosoane kwa staha na kuvumiliane wakati wa kutofautiana kwetu. Kukosoana ni afya ya kinchi kiutawala na kisiasa.

Tatu, wakosaji washughulikiwe kwa mujibu wa katiba,sheria na taratibu tulizojiwekea kama taifa. Hatuna haja ya kushughulikiana kwa namna nyinginezo.

Nne, tumtangulize Mungu katika kuilinda amani yetu kwakuwa ndicho kinachotuunganisha kama taifa na ndicho kinachotufautisha na nchi nyingine.

Tano, tuviamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kuchunguza na kushughulikia wahusika wote wa matukio ya kijinai. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko imara na vyenye weledi wa kutosha.

Sita, kila mmoja wetu ana umuhimu wake na nafasi yake katika taifa hili. Kila mmoja wetu ana wanaompenda na kumkubali na wale wasiompenda na wasiomkubali. Mchanganyiko huo ndiyo nchi yenyewe.
 
INASIKITISHA, TUMUOMBEE
Alishasema kuna jambo kama hili linaweza kumtokea - alihitaji ulinzi
 
Back
Top Bottom