DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Najaribu kufikiria, hivi Tundu Lissu alitaka kutolewa roho na serikali? Au watu wasioipenda serikali wameamua kumharibia Mhe. Rais hasahasa siku ya leo wakati anapewa report ya uchunguzi wa Almasi na Tanzanite?

Nafikiria kama ni kazi ya serikali, basi aliyetumwa ni bwege na hajui timing; maana ingawa tukio la jaribio la kuuwawa Tundu Lissu limetokea baada ya kupokea kwa report, thread ya Lissu kutaka kuuwawa imeshakuwa kubwa mara mbili zaidi ya hii ya Mhe. Rais.

Lakini kama waliopanga jambo hili ni wale jamaa wa madini, basi kweli wamebobea kwenye conspiracy.

Uhusika wa serikali hautatiliwa shaka, pale tu mtuhumiwa atakaposhikwa haraka.

Lakini kama serikali imehusika, sidhani kama hii inasaidia zaidi ya kuleta chuki. Kuna watu wasiokuwa sahihi watakuwa kwenye nafasi za uteuzi. Hapo Magufuli itabidi azipitie upya taasisi zake.
Mjomba unabusara sn. Hili swala lina kiza kinene sn. Nmependa sn commnt.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lolote laweza kuwa sababu za kushambuliwa Lisu...ingawa kwa akili za harakaharaka za kubeba mambo juu juu tulizajaaliwa Wa TZ tunakimbilia tu kushutumu kundi fulani.

Yeyote mwenye tofauti na Lisu, iwe ya kisiasa, kimaslahi, kifamilia n.k ni rahisi kutumia huo upenyo akiwa na uhakika kabisa wapi sehemu kubwa ya jamii itakapoelekeza shutuma zake.

Watu wenye nyenzo na utaalamu wakitaka kumpoteza mtu sidhani kama watatumia mbinu mbovu kama hiyo ya kumimina marisasi tu hovyo...bila hata uhakika kama wanampata mlengwa wao au la.

Muhimu hapa ni kumuombea tu TL abaki salama, atoke hospitali arudi aendelee kuvuta pumzi hii ya Mwenyezi Mungu kama sisi wengine humu tunaozijaza pages za JF.
Kwa vile serikali ina mkono mrefu iwakamate waharifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maombi maombi maombi jamani,huu si wakati wa kunangana,kupanda helicopter na kupelekwa Naii haimanishi kuwa tatizo limekwisha,Lissu anahitaji maombi badala ya malumbano na kejeli
 
Mwombee adui yako aishi siku nyingi. Tunakuombea Lissu japo binafsi huwa sikubaliani na wewe. Ila siombi mabaya juu yako ili Mungu atukuzwe! !
 
SAFI, APELEKWE KWA WASHUA, KUOKOA MAISHA YAKE.

KWA AINA HII YA KUVIZIANA KUTAKA KUUANA BILA SABABU ZINAZOELEWEKA ITATUCHUKUA MIAKA 500 KUFIKIA MAENDELEO YA MAJIRANI ZETU WA KENYA
Acha kuongea upumbavu kinachotakiwa nikumuombea Mungu apone inamaana hko Nairobi Hospital zote ziko tupu hazinawagonjwa kwenye mambo ya serious avheni kuleta siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mh. Lisu, Mungu atakuponya majeraha yako maana yeye ndiye Mponyanyi. Amen
 
NAJUA TU HAWA JAMAA WANAMUOGOPA HUYU WAMEMSHINDWA KISIASA SASA WANATAKA KUUA KABISA

 
Mimi ni mtanzania mzalendo sina chama ninampenda mtanzania yeyote yule bila kujali ni chama gani, dini gani, kabila gani, rangi gani, sehemu gani aliyotoka n.k.
Kwa suala hili la ndugu yetu kipenzi chetu Tundu Lisu kupigwa risasi wengi wetu wameshapeleka mawazo upande mmoja fulani hivi...... lakini kumbuku Rais wetu mpendwa ni mtu mwenye nia ya maendeleo mimi kama mzalendo mwingine yeyote nampongeza rais mpendwa kwa sababu kazi anayoifanya ya kula pande mbili ndani ya chama chake na upande wa pili pia, kila mzalendo tanzania mwenye uchungu na nchi hii lazima asifu kazi za rais mpendwa wa watanzania ndg Magufuli. Lakini kumbukeni rais ni kama binadamu mwingine awaye yote na amepania kufanya kazi ile kwa nguvu zote, kwa hiyo kwa ninavyomwelewa anataka afanye kazi bila kelele nyingi, au kama ukiona kosa sehemu basi kama mtu maarufu unaweza kumuarifu kuwa kuna kosa mahali badala ya kuongelea hadharani ili alifuatilie, najua kwa yale mambo anayoyafanya ya kuzuia siasa si kikatiba lakini vilevile sis wananchi hatutaki siasa majukwaani bali tunataka tuone matendo na bila shaka nitamuunga Rais Mkono kwa hili la kutaka kufanya kazi zaidi kuliko siasa za majukwaani.

Pili, kwa mwazo yangu kuna coicedence hapa, jinsi rais anafanya kazi ya kupamban na wanyonyaji wa uchumi wetu, wana mipango mingi sana ya kuharibu ile mipango ya rais wetu, mfano haya makinikia ya almasi kuna mabepari walikuwa wanavuna kama wako kwao vile sasa hii nguvu ya rais wanataka kuhamisha na kufuta la makinikia ili tuanzishe habari nyingine za misiba na tusahau mambo ya wizi mkubwa kwenye madini yetu, maana wanajua wakimuua mtu popular ana critical kama Mwanasharia mzalendo Tundu lisu ambaye kwa sasa habari ya mjini ni Lisu, baada ya zile Buldozer wetu na Rais wetu Magu.

Sasa basi tuwe na uvumilivu yawezeka ni watu tu wana nia ya kuhamisha hili suala la makinikia na kuanza habari za msiba ili tusahau. tushirikiane na serikali yetu tumpate huyo adui anayetaka kuifanya hii ndege yete "TANZANIA" isitakeoff yaani isianze kupaa.

Ndugu zangu niwaeleze kitu kimoja mliomo humu hakuna wazungu, au mtu kutoka nje ya tanzania anayetaka watanzania tuendelee kwa hiyo lazima tuwe wamoja katika hili, tushirikiane na serikali mpaka hao watu wapatikane.

maana kubwa ya kuandika hili ni kuwa kwa sababu tu ndug yetu tundu lisu amesumbuana na serikali basi wengine wanaweza kutumia hi nafasi kufanya uhalifu wao na wananchi wakaamini yule aliyekuwa anamsumbua ndiye aliye muua tuwe macho sana.

Nawapenda watanzania wote hayo ni mawazo yangu, tujenge nchi tuwe wazalendo badala ya kuwa washabiki

aksanteni
Kwakuwa alishatoa taarifa za matisho ilibidi serikali imuwekee ulinzi ili haya yasitokee na kwasasa ni kazi kweli kweli kuwa kuwa na mitizamo elekezi ya hali ilivyo.
 
Lakini mwenyekiti wake anaweza husika maana jamaa alikua anaunyemelea *UENYEKITI* kwa nguvu zote,unakumbuka yule alifariki kwa ajali ya gari miaka ile naye alikua anautaka *UENYEKITI* na uenyekiti ukachukua maisha yake?

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
Chacha Wang we.
 
Back
Top Bottom