DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Naamini kama yule wa Nape mchana kweupe hakuwa polisi wala usalama wala usalama mpka leo hajulikani.

Wa Mvungi nayo ilipotea kimya kimya.

Majuzi hapa tukaambiwa walivaa sare za polisi lakini hawakuwa polisi sasa sijui walijuaje kama sio polisi
.
Na sasa kwa Lissu nayo najua watasema watu wasio julikana tena mchana kweupe na SMG. Hivi kuna raia wanamiliki SMG?

Tumwombee apone ila kwa hali hii tunaelekea watu kujitoa muhanga tusishangae huko mbeleni.
 
Dtiketka uwhcara....nimeikumbuka sana hii kauli ya huyu Mh.labda ndiyo anamshughulikia tutajuaje?sijamtaja mtu mimi.

sent from my Infinix S2 Pro using JamiiForums mobile app
 
Ungekwoti ulichokisoma jwa Lisu
mnatuchanganya kwa vile hatupo huko, mliopo dodoma mtujuze manake kuna memba hapa anasema Lissu kakataa yupo dar , watu washahack account ya lisu hivyo wanakanusha kwa niaba ya lisu wakati lisu mwenyewe anapigania uhai wake dodomela
 
Wakuu,

Inadaiwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!

9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow
Ndo tuende zimbabwe sasa, bado mnangoja nn??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom