DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

CCM imetoa pole

Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole
View attachment 583477

UPDATES: 2235HRS
Ndege iliyokuja kumchukua Tundu Lissu ndo inatua Uwanja wa Dodoma. Ni ndege binafsi, imetoka Dar Es Salaam na itampeleka Mh. Lissu Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi.
6a0df0d4014896f500bc344cb3ddcb26.jpg

TunduLissu akipakiwa kwenye ndege usiku huu tayari kwa safari ya Nairobi kwa matibabu zaidi
3c38765220348b8a8712fc343f512797.jpg


*Rais wa Chama cha Mawakili Kenya(LSK), Isaac Okero amesema Lissu amelazwa Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

Lissu awasili Nairobi salama lakini Ubalozi wa Tanzania haujatoa ushirikiano

Mbowe: Hali ya Lissu ni mbaya na yupo kwenye chumba cha upasuaji

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

very sad, get well soon
 
nilishangaa sana walipong'ang'ania kutaka kumpeleka Mh Antipas hospitali ya Muhimbili...eti watuhumiwa wanamuamuliwa mhanga mahali pa kwenda kutibiwa...nchi hii ina mijitu ya ajabu sana.
 
Ngoja angalau wamalizie kuzichomoa risasi mlizomiminia, hivi hata hamna huruma kwa familia yake? Sasa Familia yake inshitaji upendo zaidi na siyo kuendelea kumtumia Tundu Lisu kama mtaji wenu!
kila mtu anajuwa wewe na wengine wengi ni mmoja wao na nakuhakikishia kwamba maisha yako yatakuwa mabaya sana milele namilele machozi ya wengi damu yake iliyomwagika ita wa hunt forever
 
Kama ingekuwa ni rahisi kihivyo basi Dunia nzima tungepitia hayo unayoyasema, mmesahau mlivyofanya pati hapa na kushangilia wana CUF walivyofariki kwa ajali au ni hiyo laana unaipata kwa sababu tu ya Tundu Lisu kupigwa Risasi? Yeye ni nani Dunia hii? Vp khs ndugu zetu waliopigwa risasi Kibiti hao sio watu!
Ha ha spin doctor kwa hio pati yenu imeingia kitumbuwa munajianika sana wauaji nyie watu wa Kibiti walivyoanza kuuwa wawa nani walisema mwanzo ccm bashite na mwenyekiti wenu simulitengeneza movie ya kibitz ika back fire mulidhani watanzania ni stunt brain kwani sasa si mumekataza vyombo vya habari visitangaze mbona mauaji yanaendelea na nyie daamu za wananchi mumegeuza mvinyo
 
si kweli..labda unazungumzia sinema..hata hvo haya maneno yako yanatokana na nini,mbona hayana uhusiano na lolote
Ki akili-ccm huwezi kujua nini kinaendeleana nini matokeo zaidi ya kuimba ulicholishwa pasi na kuwaza nje ya boksi. Kwa anaeiwaza leo hana haja na kesho.
Mchawi huwa haishii kuwaroga asiowajua
 
Kalagabaho! Kwani Chacha Wangwe aliuliwa na serikali ya ccm?
Hivi ule mgogoro wa mgodi wa Nyamongo alipouongelea bungeni alikuwa anagusa mikataba walioingia ni CDM au ilikuwa wazee wa makinikia kina msituseme?
au mnadhani sote ni akili kusahau?
 
Huyu [HASHTAG]#malisa[/HASHTAG] ameandika "GIZA KUU" katika facebook account yake, sijui anaanisha nini, presha zinapanda tu
 
Hivi ule mgogoro wa mgodi wa Nyamongo alipouongelea bungeni alikuwa anagusa mikataba walioingia ni CDM au ilikuwa wazee wa makinikia kina msituseme?
au mnadhani sote ni akili kusahau?
Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti wa chama - yakampata yaliyompata.
Zitto alipotangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama - akapigwa panga kwenye chama.
Lissu amejifanya yeye ndo Zitto kabwe (act) wa chadema - tutashangaaje kupatwa na yaliyompata ??
 
Ukristo msingi wake Ni Biblia. Ndicho kipimo tulichopewa. Hakuna sehemu tumetakiwa kuomba visasi kwenye Biblia. Nifundishe nami hiyo verse. Nafanya hivi kutimiza lile ndiko, tuonyane sisi kwa sisi. Otherwise jinsi ilivyo Roho yako ndio uhusiano wako na Mungu. Ila Kumbuka, huwezi kumpenda Mungu usiyemwona wakati unamchukia mwanadamu unayemwona

Yesu alichapa watu bakora hekaluni na kupindua meza zao waluofanya biashara hekaluni. Hicho kilikuwa kisasi? Hiii hiii hii
 
Wangwe alipotangaza kugombea uenyekiti wa chama - yakampata yaliyompata.
Zitto alipotangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama - akapigwa panga kwenye chama.
Lissu amejifanya yeye ndo Zitto kabwe (act) wa chadema - tutashangaaje kupatwa na yaliyompata ??
Ilikuwaje geti likawa wazi ili wauwaji waingia na kutoka pasina kizuizi? Hivi walinzi wa maeneo ya tukio la kupigwa risasi Mh. TL walikuwa wapi muda huo? ama silaha zilizotumika zilikuwa na viwambo vya kuzuia sauti?
 
Wale baadhi ya Mawakili waliosema hawamwelewi Lissu kwa kuitisha Mgomo wa Mawakili wakati ule kupinga kulipuliwa kwa ofisi ya Uwakili ya IMMA, sasa baada ya Lissu kushambuliwa kwa risasi wamemwelewa?

Wamekuwa jasiri, waoga ama ndiyo watarudi kule kule walikokuwa kuachia chama chao kuwa tawi la Wizara ya Sheria?

CC:

Petro E. Mselewa
 
Back
Top Bottom