DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Hizi ni figisufigisu za watu kutoka ng'ambo ,,vita ya kugombanisha Serikali na wapinzani mwisho ihamie kwa wananchi..

Imeanza rasmi.
Wenye maslahi na madini washaaanza kufanya kazi yao..kama ambavyo wanafanyaga katika nchi zenye Rasilmali..Ya Gas,Mafuta,na Madini.

Kuwagombanisha wananchi wauane wenyewe kwa wenyewe wao wakwapue mali.
Vita hii ishindwe kwa jina la Yesu.

Tumeshawabaini.
Tutasimma kwenye zamu zetu.
Eeh Mungu Mponye Tundu maadui waibie
 
hata akifa maneno yake yataishi na kila mwenye jukumu la kufanya atasimama kwenye eneo lake
 
Ukiambiwa umtaje huyo anayetaka kumuua utamtaja?that's my point mkuu!
Hivi wewe ni mzima kwel?,inshu siyo kutaja inshu ni tukio lenyewe lilivyotokea,kwa hiyo unataka kutuambia alikuwa anasalimiwa na risas,Watu wengine bhana ni hasara kwa kwel,Mtu kapigwa risas maana yake nini?,au risas ni Maj au kitu kisichoweza kuutoa uhai wa Mtu?,duuh...!,bora nguo iraruke lakini siyo kuraruka akili,kwa hiyo wewe ikitokea umepigwa risas,hao waliokupga risas walikuwa hawana lengo la kutaka kukua!,au haujui risas itakuwa,unaisikia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali impe ulinzi pamoja na kwamba ni mkosoaji mkubwa wa serikali lakini ni Mbunge wa Bunge la JMT.
Unbelievable. Shocking. Tunakuombea Kamanda upone mapemna na urudi kwa mapambano. Waliodhani wanakunyamazisha wamekosea.
 
Wakuu,

Inadaiwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!


56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES;

=======

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

Tunakuombea Mh. Lissu wewe ni mpigania haki huru
 
Karibuni kwa kuni quote humu..

Mnapenda sana kubwabwaja na kiwaga na maneno makali kwa serikali yetu na hampendi kuambiwa ukweli.. ukweli ndio huo na mamlaka waanze kuwachunguza chama cha Chadema na UKAWA.. waende pia kwa wenzake TLS.. lazima kuna wanaojua lililojiri kiundani na mpango gani haukwenda kama ulivyopangwa..

Pia kuna watu wanajua anapokea pesa za malipo ya kuharibu ya serikali nao waojiwe sababu ni wenzake..

Leo Raisi ameongelea kujua mengi pia kwa upande wa mali za Taifa na jambo hili limewaohopesha wengi wahuni, wasaliti na waliojaa tamaa.

Wengi wanajua Mkulu anayajua yote na sasa ni wanataka kutafuta kisingizio hiki kuleta haya mnayodai kuwa ni watawala wanahusika..

Tabu yenu wengi nyie hamjui kukaa na kufikiria.. mnajua kuisema vibaya serikali na hata Raisi mkipata mwanya... sasa ya huyu Lissu mnona mnaweweseka na kutaka kuonyesha mna rojo nzuri wakati tumezoea kuwasoma humu na wenzenu wengiiii.. mmejaa maneno machafu sana wengi wemu pia.

Sasa leo ripoti na uamuzi wa Raisi umewaacha hoi.. mnakuja huku kunidandia kama vile hamjaona wengine wanaosema kuwa ni mipango ya ndani.

Nasema tena mamlaka ianze na hao hao wanaohusika maishani na Lissu nae akipona ahojiwe aseme ukweli na achunguzwe kwanini majambo yake na labda kula pesa za watu wanaomtuma avuruge ya serikali..

Wote tusubiri upelelezi uanze na ukweli utoke.. tena nitafurahi kuona JPM anatoboa siri za wasaliti wa nchi yetu..

Mnajua kuwa serikali hawawezi kuwa wajinga kutenda haya mnayokuwa mnasubiri kuyaona bali wenzenu hao mnaowasjangilia ndio wanajua zaidi.. bila kusahau anavyopenda kutaka kuwa juu zaidi ya wakuu wa Chadema wanavyotaka.. muanze kuulizana nyie mnaopenda kuisingizia serikali kwanza nini kimo ndani ya chumba mlichomo wote.

Hii sasa mtauona ukweli na kukimbia ma kujionea aibu kubwaaaa... haya ya kupangwa na kutendwa na wenyewe.. ila pia labda maagizo yameenda mbali hawakuelewa ni kupiga gari tu.. wakaamua kutaka kummaliza..

Mnaonitukana hayo mtakiwa mmejifunza mlipolelewa ndipo mnaona wa hivyo.

Tunamuombea apone ili ahojiwe na mengine kutendwa juu yake ili tujue ukweli sasa...Serikali inaoenda wananchi wake wote bali upinzani wamezidi sasa na Lissu anajua kuwa anavuka mipaka na hii inaonyesha kuwa hata ile ya bomu alishushuka.. na sasa ya mwenyewe pia hii itakuwa aibu kwake na wote wahusika.

Kuna lingine... vipi ripoti.. JPM sio wa mchezo mchezo mliona na flash.. yaani yupo dakila tano mbele..

Mnaosema nalipwa kwani na nyie mnalipwa kuandika humu mnayoandika!?

Mungu ibariki Tanzania.. wabaya ma waovu wote wapatikane na kuacha kuharibu jina la nchi yetu kwa masalahi yao binafsi yaliyojaa tamaa za pesa za wasiojali nchi yetu.

N.B. kama umeniquote baada ya hawa.. basi nawe usome tu haya.. CIAO
Hapana wewe si wa kawaida... Hiyo chuki unayoionesha hapa na kum link TL na hicho unachokiita usaliti kinaku implicate kuwa upo ndani ya cycle hiyo hiyo... Maandiko yanatuambia tuwaombee watu wenye roho mbaya ili siku moja mshuhudie ukuu wake...
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Kuna tetesi siyo nzuri..! Tuwe na vifua la sivyo yaweza kuwa simanzi kuu[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom