DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa na fahamu na sasa anapelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
======
Taarifa zote za uhakika tutakuwa tunazitoa kila baada ya muda mfupi...
Picha HELKOPITA iliyombeba Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ikiwa angani kuelekea Nairobi
View attachment 583481
Isije ikalipuliwa nayo maana hali si shwari sasa
MUNGU amponye kamanda
 
Alichosema Lissu chumba cha habari

Alichosema Lissu.jpg

Kwa ufupi
Licha ya kushambuliwa kwa risasi, Tundu Lissu amewahi kusema kuwa katika siku za karibuni hakuwahi kutishiwa maisha, bali miaka 20 iliyopita.

Dar es Salaam. Machi 27, Lissu alitembelea chumba cha habari Mwananchi na moja ya maswali tuliyomuuliza ni “Kwa misukosuko mbalimbali ya kisiasa unayokumbana huna hofu juu ya maisha yako?”

Jibu: Ni kweli watu wana hasira na mimi, lakini hawajawahi kunitishia maisha. Kabla sijawa mbaya kiasi hiki, miaka 20 iliyopita nilipokuwa mwanaharakati kwenye Chama cha wanasheria wa mazingira (LEAT) pale nilikutana na vitisho. Nilianzisha ugomvi na mfanyabiashara anaitwa Reginald Nolan, huyu aliuzia nchi vifaa vya kijeshi na katika kulipa deni lake, Serikali ya Mkapa ikampatia ekari 20,000 ajenge mabwawa ya kufuga kamba. Tulianza kupambana naye, hapo ndipo tulikuwa tunakuta bahasha za vitisho chini ya mlango katika ofisi zetu pale Kariakoo. Lakini hatukunyamaza. Tulimvuruga yule jamaa akakimbia na baada ya hapo sijawahi kutishwa.

Lakini najua watakuwa wanajiuliza, unamuanzaje yule jamaa, useme nyamaza tutakuua, useme nyamaza tutakufunga, unaanzaje? Lakini kwa siasa za namna yangu, kwa sababu kuna watu wanakuchukia kwelikweli, huwezi kuwa salama na usipotegemea kusumbuliwa utapata shock (mshtuko).

Yote haya yanayonipata sijawahi kushangaa, sijawahi kukosa usingizi. Hata nikilala Central Police (Kituo Kikuu Polisi) huwa napata usingizi na ninakoroma kwelikweli. Nikishapata mto wangu, naunganisha chupa tatu za maji nazifunga kwa shati nalala kama kawaida.

Lakini nikisema sikosi usingizi sina maana kuwa napafurahia, hapana. Kule si mahali pazuri hata kidogo. Ni pabaya kwelikweli. Si pazuri hasa kama huna kosa. Nasema kama huna kosa maana najua kesi zangu zote za uchochezi kuwa sina kosa lolote, sheria ileile ninayodaiwa kuivunja imenipa uhuru wa kuzungumza, kuikosoa Serikali na kumkosoa Rais.
chanzo.Alichosema Lissu chumba cha habari
 
siraha zote zimilikiwazo na watu zimesajiliwa na idadi ya risasi kwa kila siraha
 
Hivi watu wasiojulikana ni pamoja na walioingia clouds wakamkata mtama sudy na kwisa. Na wengine niwale walimnyooshea bunduki nape hadharani??. Watu wasiojulikana hivi huwa wanakaa wapi? Hata mimi sijulikani
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

View attachment 583477


REUTERS Wanaripoti hivi:

By Fumbuka Ngw‘anakilala

DAR ES SALAAM, Sept 7 (Reuters) - Tanzanian opposition lawmaker Tundu Lissu, a fierce critic of President John Magufuli’s government, was shot and wounded by unknown assailants at his residence in the administrative capital Dodoma on Thursday, his party said.

“Lissu has suffered multiple gunshot wounds and is being treated at the main public hospital in Dodoma,” Tumaini Makene, spokesman for the main opposition CHADEMA party, said.

CHADEMA said in a separate statement the incident took place at his Dodoma residence on Thursday afternoon.

“We strongly condemn this attack and are closely monitoring his condition,” the statement said.

Lissu, who is also the president of the Tanganyika Law Society and opposition chief whip in parliament, has previously been arrested by police on several occasions and charged with incitement.

He was arrested in July and later released after having called Magufuli a “dictator”.

The motive of the shooting is unclear. Tanzania police’s spokesman was not immediately available for comment.

DW (Kiswahili)

2 hrs ·
HABARI ZA HIVI PUNDE: Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana. Amelazwa katika hospitali kuu ya DODOMA - Kwa mengi zaidi kuhusu kisa hicho, JIUNGE NASI kwenye Dunia Yetu Leo Jioni

Al-Jazeera Wanaripoti hivi:
Tanzania: Opposition MP Tundu Lissu wounded by gunmen
Top opposition figure suffers multiple gunshot wounds by unknown attackers at his residence in Dodoma
409a300def804e93b6ee6cb811960aa4_18.jpg

A prominent opposition member of parliament in Tanzania has been shot and "seriously wounded" by unknown attackers at his residence in the administrative capital, Dodoma, according to officials.

Tundu Lissu underwent emergency surgery after being shot in the abdomen on Thursday. James Kiologwe, a doctor at Dodoma regional hospital, said he was in stable condition.

"[Tundu] Lissu has suffered multiple gunshot wounds," Tumaini Makene, spokesman for the main opposition CHADEMA party, said shortly after the incident.

"We strongly condemn this attack and are closely monitoring his condition."

Mwigulu Nchemba, Tanzania's home affairs minister, confirmed the incident and Lissu's condition, adding that the government would issue a statement after receiving a medical report.

The motive of the shooting was unclear.

Fierce critic
Lissu, a fierce critic of President John Magufuli and his government, is the president of the Tanganyika Law Society.

He has previously been arrested by police on several occasions and charged with incitement.

In July, he was arrested and later released after having called Magufuli a "dictator" over alleged attacks on the opposition and the media.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa na fahamu na sasa anapelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
======
Taarifa zote za uhakika tutakuwa tunazitoa kila baada ya muda mfupi

Muhimbili dawa zimeisha?
 
Back
Top Bottom