Dodoma: Watu 5 wa Familia moja wauawa

Dodoma: Watu 5 wa Familia moja wauawa

Huyu kuna siku atasema ijengwe ikulu ya raisi wa machifu.mikoa miwili sasa amaimaliza.nasikia mkoa unaofata ni kagera
#chifu hangaya
#chifu chui jike manka.

Bukoba naskia watamuita ,
#chifu kokubanza
 
View attachment 2092348
Watu watano wa familia moja wameuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Chanzo: Radio One

C0339130-2F04-4C54-95C9-6D2C5B9D4163.jpeg


86B1C807-82B6-4E1B-8DA4-57E1CFF95E0F.jpeg
 
Ndugu, Amini usiamini bila Mungu kuwepo moyoni mwetu hatuwezi kuwa na upendo. Upendo ndio kila kitu, bila kuwa na moyo wa upendo watu wataelimishwa lakini chuki zitaendelea kubaki tu na mauaji yataendelea.


We Kiranga Mwitu kuna Kiranga mwenzako humu jf hajui kama kuna Mungu.🤣🤣
 
Uwezekano ni Visasi ndani ya Jamii.

Viongozi wa Kiimani hawafanyi kazi zao vya kutosha, wamewaachia Waganga wa Kienyeji kuendesha Jamii huku wao wamejikita kwenye kuhimiza UTOAJI wa sadaka.
Maovu yameletwa na viongozi wa nchi wanaoamini katika wizi, uporaji na kupuuza sheria.

Kama kiongozi anapata mamlaka kwa kuiba kura na hakuna namna ya kumtoa. Kama polisi inachukuliwa kama kikundi cha wahalifu. Kama matapeli, wezi na mafisadi ndiyo wanaosifiwa kuwa wajanja. Kama ukitapeliwa huna pa kwenda na ukienda kwenye sheria ndiyo utatapeliwa na hao uliowapelekea kesi. Kama makanisa yanageuzwa vijiwe vya kuendeshea utapeli na uhalifu. Nk. Hapo lazima watu wamalizane wenyewe kwa wenyewe.

Kama mifumo ya upatikanaji haki ingekuwa inaheshimiwa katika ngazi zote, haya mambo yasingesikika.

Lakini baba wa matatizo yote ya nchi hii anafahamika. Na yampasa atokomezwe mapema.
 
Watu waelimishwe tu, hamna cha maombi hapo, kitafutwe chanzo cha mauaji, tatizo mnachagua aina ya ukatili na watu wanaofanyiwa, mf. Ukatili unasemwa dhidi ya wanasiasa hamkemei wala hamna maombi, kumbe ndio mnapanda mbegu ya chuki na ukatili!
Kwa hiyo unataka kusema Samia ndio kawaua?

Sio kila kitu ni politics wadau, kuna mambo mengine ni maadili ya kifamilia na hofu ya Mungu watu imewatoka
 
Maovu yameletwa na viongozi wa nchi wanaoamini katika wizi, uporaji na kupuuza sheria.

Kama kiongozi anapata mamlaka kwa kuiba kura na hakuna namna ya kumtoa. Kama polisi inachukuliwa kama kikundi cha wahalifu. Kama matapeli, wezi na mafisadi ndiyo wanaosifiwa kuwa wajanja...

Hapa umenena sawa kabisa, mifumo ya kutoa haki imefubaa, watu wanafanya watakavyo. Hii ni kansa iliyopandwa na viongozi wanaoingia madarakani kwa matambiko na uporaji. Hayo maagano yao machafu ndio matokeo yake haya.
 
Maovu yameletwa na viongozi wa nchi wanaoamini katika wizi, uporaji na kupuuza sheria.

Kama kiongozi anapata mamlaka kwa kuiba kura na hakuna namna ya kumtoa. Kama polisi inachukuliwa kama kikundi cha wahalifu. Kama matapeli, wezi na mafisadi ndiyo wanaosifiwa kuwa wajanja...
Duh,nimesoma hapa imenijia picha ya Bw Ramadhani Ntuzwe...ni karibia mwaka wa tano huu anahangaikia haki yake na mpaka wa leo wanampiga chenga tu.

Cha kusikitisha ni kwamba hata aliyekuwa na dhamana ya Fedha wakati ule ambaye sasa ni Mkuu namba mbili wa Nchi naye yupo kimya tu wala hana habari...hivi leo ikitokea Bw Ramadhani ameuwawa kuna Kiongozi atathubutu kumlilia?.
 
Huyu kuna siku atasema ijengwe ikulu ya raisi wa machifu.mikoa miwili sasa amaimaliza.nasikia mkoa unaofata ni kagera
#chifu hangaya
#chifu chui jike manka.

Bukoba naskia watamuita ,
#chifu kokubanza
Kichwa kikishavurugwa na 2025, ndiyo matokeo yake haya. Badala ya kupambana na mfumuko wa bei, kuimarisha na kuboresha sekta ya kilimo, ajira, viwanda, biashara, nk.

Yeye yuko busy na mambo mepesi mepesi tu. Kazi tunayo.
 
Nina muda sanaa sijawah kuskia tembo,simba au chuii kaua mtu zaid kwa sasa ni kuskia auawa au wauwa..na wanaohusika ni binadamu...hii inaonesha ni namna gani binadamu tumekuwa hatar zaid ya wanyama
 
Nina muda sanaa sijawah kuskia tembo,simba au chuii kaua mtu zaid kwa sasa ni kuskia auawa au wauwa..na wanaohusika ni binadamu...hii inaonesha ni namna gani binadamu tumekuwa hatar zaid ya wanyama
Binadamu ni hatari zaidi wanyama tangu zamani sana ndio maana ya kuwekwa katiba na sheria.
 
Mbona mauaji na kupotea kwa watu kumeongezeka kwa kasi sana siku hizi au ndio biashara ya viungo vya watu imepamba moto
 
Mauaji yanazidi kwa kasi sana...ndugu zangu tumrudieni Mwenyezi Mungu ili tuwe na upendo. Kwa sasa upendo umekwisha baina yetu, bila Mungu hatuwezi kutatua hili swala!. Eeeh Mwenyezi Mungu tuokoe waja wako..
Mungu hajawahi kuokoa watu yy mwenyewe anakata watu wampiganie wamtete
 
Back
Top Bottom