Habari iliyopo kwa sasa ni kwamba nyumba ya mbunge mheshimiwa Polepole mkoani Dodoma imevamiwa na watu wasiojulikana wameharibu mali za thamani na kuacha ujumbe mzito wa kuwa aache kuichafua serikali ya sasa
View attachment 2041847
=====
WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA NYUMBANI KWA MBUNGE HUMPHREY POLEPOLE,
Watu wasiojulikana wamevamia nyumbani kwa mbunge Humphrey Polepole (Dodoma) wakati akiwa safarini, na hii ndio hali ya nyumbani kwake palivyo kwa sasa kama video inavyoonesha
Mbunge Polepole amethibitisha kuwa nyumbani kwake jijini Dodoma, pamevunjwa na watu wasiojulikana na kuibiwa Television pamoja na kuharibiwa vitu mbalimbali siku ya Desemba 12, 2021 akiwa safarini Manyara ambapo amerejea usiku huu na kukuta hali hiyo
"Hali nilivyoikuta nyumbani kwangu Dodoma muda huu, Nakwenda kuripoti Polisi. Yeyote aliyefanya haya Mungu atanilipia" amesema Humphrey Polepole.
View attachment 2042259