Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

October 2020 uchaguzi lakini mpaka sasa wanyanyembe hamjajipanga kwenye kitengo cha habari?
Mgombea wenu Lissu mpaka sasa hajajua aelekee wapi mpaka afundwe?
Hata ratiba za sikuu hamzijui?
Nyinyi hamna umakinifu hamuwezi kupewa nchi.
 
Inaweza tokea wakafunga siku hiyo. Wakaja sema mbona nchi nzima ni sikukuu nyie hamkujua??
Sawa watu watalala hapo mpaka j3 labda wafunge moja kwa moja,

Wakifanya hivyo ndo watadhihirisha kwamba siyo huru, na wanamwogopa lissu
 
Hatuhitaji aongee lugha ya kubembeleza, vinginevyo tungemtaka Nyalandu, tunataka azungumze mambo yatakayopandisha haiba yake, na sio yatakayomfanya awe easy target.
Hilo bado wengi hawaelewi, tumempendekeza Lissu kwa vile lugha yake ndio inawafaa hawa CCM wa sasa.
Lugha za kina Lowassa hazijawahi kutufaa zaidi ya kuifaa CCM na sie kuonekana mafala.
Na Lissu sio tuu kwa lugha yake Bali pia slogan ya "Hakuna kumuachia Mungu kupigania haki ya kura zetu".
 
Nikweli kabsa mfano ni suala la corona asiliongelee kabsaa aiache serikali ipambane nalo hivohivo, kwani hakuna mwananchi anayependa lockdown na ukiongelea lockdown lazima utachukiwa.
 
Wewe hujuelewi waliotufikisha hapa si hao maviccm mpaka tunakuwa maskini wakutupwa? Mambo aliyoyaahidi huyo rais wako ni asilimia ngapi ametimiza? Au unafikiri hatukumbuki mwaka 2015.
Mkuu umasikini wako haujaletwa na CCM Bali ni uzembe wako wa kufanya kazi,ulitaka ccm ije ikuamshe asubuhi uende shambani
 
Hii iko poa sana. Mitandao ya kijamii ni mingi mno inafikia watu wengi sana. Tulio kama hili liwafikie watanzania wote.

Kupitia audio, video, texts, photos

Kitengo cha habari msituangushe
 
hivi kati ya TL na Jiwe ambaye ni Rais, anayetaka kuwapanua watu na kumuoza mama ake kwa zawadi ya jogoo nani mropokaji?
Hivi huu upumbavu wa kupewaga ushauri na kusema mbona kule kuko hivi, huwa unatokana na nini?
 
Mzee wenu Jiwe anavyocharuka Ziarani ninyi mnamuona Lissu tu .Na apunguze maneno
Kumbe basi Lisu hana tofauti na jiwe!

Tutamchagua Magufuli maana wote kumbe ni walewale
 
Huyo ndo anatakiwa kwa Sasa
 
Kumbe basi Lisu hana tofauti na jiwe!

Tutamchagua Magufuli maana wote kumbe ni walewale
Mkuu kunatofauti kubwa,shida ya Lissu ni kuongea vitu vizito ambavyo watu wenye akili kidogo wanahitaji muda mrefu wa kuvitafakari na kuvielewa while mwingine analopaka tu imradi neno limekuja mdomoni.lakini tofauti nyingine ni kwamba utu na mtu ni muhimu sana kwa Lissu while Magu barabara inaweza kuwa muhimu kuliko mtu na utu wa mtu.Ndo maana haikuwa shida kwake kuelekeza rambi rambi kwenye miradi ya serikalini
 
I wish him every blessing from the same God that rescued him from death.
 
Mkuu siyo kwamba una mdescribe magufuli hapa? Hivi maji Yuko wapi kwani au mwananzila?
 
Kumbe basi Lisu hana tofauti na jiwe!

Tutamchagua Magufuli maana wote kumbe ni walewale
Nashangaa CCM mnamsema TL wakati mzee wenu Ndiye mropokaje mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…