Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga majiani kumsalimia na kumsindikiza.
Read your messages brother!
 
Neno zuri kabisa. Chadema waongeze watumishi katika kitengo cha habari cha chama kwa kuweka vijana mahiri na wazoefu.
Watoe hata fursa za kujitolea (mradi wawape posho ya kujikimu) kwa vijana wengi kadri iwezekenavyo maana wapo vijana wengi wapenzi wa Chadema mtaani ambao awamu hii imewakatili ajira.
Kipindi hiki idara ya habari no muhimu sana hasa kwa vile vyombo vya habari vina maelekezo ya kuwabania. Na tovuti iongezewe uchangamfu kuwa vibe

Kunywa chochote hapo kwa mangi nakuja kulipa. Big up sana.
 
Police bado hawajatoa tamko kwamba wagombea waende peke yao sababu ya corona?

Pia saa nane nane ofisi zisije zikafungwa kusingizia kwamba ni Jmosi nusu siku ama ni public holiday.

Maana nchi hii kila hila yawezekana.

Go Lissu goooo...Rais wa wanyonge
Tahadhari zote zimechukuliwa
 
Amsha popo
FB_IMG_1596778126258.jpeg
 
Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga majiani kumsalimia na kumsindikiza.
Sasa hayo kasema Lissu?
Kumbe #1 akiwa na uwezo mdogo wa kuelewa basi hata wanaomuunga mkono lazima wawe kama yeye?
 
Binafsi sioni dhambi vyama vyote kumuunga mkono Magufuli amalize kipindi chake. Otherwise ni kupoteza fedha na rasilimali. Uchaguzi si vita, bali mchezo wa hesabu. Namba zilishagoma kwingine.
 
Mkuu hv una mwamini kweli huyo mtu?? Huyo ni bia yangu ujue ..ratiba iko hvyo wala hiyo sikukuu haiwezi kuvuluga ratiba za NEC ...mpuuze tu huyo bia yangu

Ni kweli usemayo, ila kesho ni siku kuu kweli, na ifahamike kuwa cdm ni mtoto wa kambo. Ndio maana nimeomba Molemo atuhakikishie kuwepo kwa zoezi hilo, bila kuathiriwa na hiyo public holiday.
 
Lissu hawezi kushinda na kamwe hatakuwa rais wa Tanzania labda jua libadili uelekeo,kwa lipi lissu kaifanyia Tanzania na watanzania hadi wampe heshima ya kiongoza nchi yetu?

Lissu ni mtu hatari sana kwa mstakabari wa taifa letu kwani ni selfish person, ni mtu mwenye jazba,hana nidhamu,amejaaa chuki,na anatumika na nchi za magharibi ili kuvuruga mstakari na umoja wa taifa letu,huyu bwana hafai lazima apingwe kwa kila namna .

Harafu mtu anaposema lissu atakuwa rais ni kujidanganya sana,ataongoza serikali ipi ikiwa chama chake hakina uhakika wa kupata japo wabunge watano,hii ni ndoto

Mwambie lissu kuwa amejidanganya na kama anamatumaini ya kuiongoza Tanzania basi kapotea,

Eti mtetezi wa wanyonge,wanyonge wepi hao anaowatetea ?
Endelea kulala wewe!
IMG_20200623_122420.jpg
 
Tunashukuru Molemo kwa kuleta hii habari. Kuna uzito fulani kwenye kitengo cha habari cha cdm, kiasi kwamba kuna uzi humu jukwaani unaohimiza kitengo cha habari kuamka. Kuna ushauri pia kuhusu Tundu Lisu jinsi ya kufanya siasa zake bila kupoteza credibility yake. Ni vyema kama chama mkakaa na Lisu na kumfunda. Kuna baadhi ya maneno anaongea yanampotezea haiba yake.
Mfano suala la corona. Aachane nalo kabisa lakini namna anavyoli address litampoteza.
 
Lissu hawezi kushinda na kamwe hatakuwa rais wa Tanzania labda jua libadili uelekeo,kwa lipi lissu kaifanyia Tanzania na watanzania hadi wampe heshima ya kiongoza nchi yetu?

Lissu ni mtu hatari sana kwa mstakabari wa taifa letu kwani ni selfish person, ni mtu mwenye jazba,hana nidhamu,amejaaa chuki,na anatumika na nchi za magharibi ili kuvuruga mstakari na umoja wa taifa letu,huyu bwana hafai lazima apingwe kwa kila namna .

Harafu mtu anaposema lissu atakuwa rais ni kujidanganya sana,ataongoza serikali ipi ikiwa chama chake hakina uhakika wa kupata japo wabunge watano,hii ni ndoto

Mwambie lissu kuwa amejidanganya na kama anamatumaini ya kuiongoza Tanzania basi kapotea,

Eti mtetezi wa wanyonge,wanyonge wepi hao anaowatetea ?
Jiwe lenu mwaka huu, ndo Basi tena
 
Binafsi sioni dhambi vyama vyote kumuunga mkono Magufuli amalize kipindi chake. Otherwise ni kupoteza fedha na rasilimali. Uchaguzi si vita, bali mchezo wa hesabu. Namba zilishagoma kwingine.

Ukimuunga mkono Magufuli kupita leo bila kupingwa, ujiandae yeye kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Magufuli sio masiha, hivyo hana uhalali wowote wa kuachwa apite bila kupingwa.
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.
Mbarikiwa anaingia Yesrusalem
 
Ni kweli usemayo, ila kesho ni siku kuu kweli, na ifahamike kuwa cdm ni mtoto wa kambo. Ndio maana nimeomba Molemo atuhakikishie kuwepo kwa zoezi hilo, bila kuathiriwa na hiyo public holiday.
Ondoa shaka mkuu ...ikifika kipindi hk NEC huwa haina J2 wala ckukuu ..na kesho ndo ratiba yetu hvyo bc Kama kungekuwa na sikukuu bc wangetupa tarehe nyingine
 
Mzee wenu Jiwe anavyocharuka Ziarani ninyi mnamuona Lissu tu .Na apunguze maneno
Mikutano yake imebaki ni ya vichekesho tu badala awamibie wananchi amewafanyia nini cha maana kwa miaka 5
 
Back
Top Bottom