Jibu ni NDIYO
Maana ya jambo kama falsafa, mfumo au itikadi unaweza kuipata kwa
1. Kuambiwa
Hii ni ni kama tulivyoambiwa na kuaminishwa kupitia mifumo yan kisiasa na kielimu kuwa demokrasia ni nini
2. Kutengeneza maana binafsi
Hii unaipata kutokana na jinsi unavyokiona kitu husika kwa mfano, kuna anayeamni demokrasia ni mtego tu tuliowekewa na watu ili uwanufaishe wao kwa kupitia milango ya nyuma na hauna maana nzuri kwa hali halisi tuliyonayo waafrika.
3. Kitu kma kilivyo
Hii inaweza isiingie kwenye hiyo milengo mingine, kwa maana kwamba siyo kile unachoamabiwa au anachoshinikizwa kuamini au unachoamini wewe mwenyewe lakini ndo uhalisia wa mambo
KUHUSU AFRICA, SI TU KWAMBA TUNA MAANA YETU YA DEMOKRASIA BALI TUNAPASWA TUWE NA MAANA YETU JUU YA JAMBO HILI MTAMBUKA.
Demokrasia tuliyoletewa na hao wageni ina maambo mengi lakini kwa haraka haraka makubwa ni kama vile
A. Uchaguzi huru na haki
B. Uchaguzi kufanyika kila baada ya kipindi filani
C. Mfumo wa vyama vingi
D. Uhuru wa kusema/ uhuru wa maoni
E. Kuheshimu haki za binadamu
Sasa the issue is hayo mambo yote pengine ni mazuri, lakini wanaotetea demokrasia bila kuangalia kwa undani wanayachukua yalivyo (they take ghem for granted)
Mfano mzuri, demokrsaia inataka vyama vingi lakini kuna tija gani kuwa na utitiri wa vyama vya siasa? Vyama vipo vingi ni sawa lakini, je ni vyote vina nguvu? Jibu ni hapana mfano hai kwa mazingira yetu vyama vya upinzani ni vingi vidogo vidogo kiasi kwamba havina nguvu ya kutoshana ubavu na chama tawala, kwa hiyo hapo takwa la demkokrasia limetimizwa lakini halina tija
Kuna uhuru wa kusema ni jambo jema, lakini ni vipi huo uhuru unapopitiliza mipaka? Kuna wapinzani wao wanachojua ni kusema al mradi wapinge tu. Mwanagenzi mmoja humu aliwahi kusema upinzani ni kama imani hivyo hata serikali ifanye mazuri vipi, ukiwa mpinzani kazi yako ni kupinga. Hili pia ni tatizo, kitu kikiwa kizuri kinaonekana na mpinzani anayepinga kila kitu ataonekana hafai, ukienda mbali kwenye hili, inafikia mahali mpinzani anapinga hadi anafikia hatua ya kuhatarisha uwepo wa mambo mazuri. Chukulia mpinzani anayeshabikia mali za nchi/ umma kusikiliwa na wadeni al mradi aonekane yuko tofauti unamchukuliaje, hapo uzalendo uko wapi? Mtu kama huyo akipewa mpango mbaya kuihujumu serikali ili ionekane haifai atasita kuutekeleza? Na serikali inapohujumiwa hasara ni kwa nani, kama sio kwa umma?Ni vizuri uwepo uhuru wa kusema lakini kuwe na mipaka fulani sio kusema sema tu hata kama unaharibu.
Bila kuficha haya mambo tunapandikiziwa ili yatuvuruge tu, Afrika inahitaji kuwa namna yake ya demokrasia sio kuiga au kufuata tu tunayoaminishwa na jumuiya za kimataifa kwani hata wao kuna vitu vikifikia hatua fulani demokrasia yao hiyo hiyo wanaiweka pembeni mfano mzuri Marekani na Umoja wa Ulaya ziliilaumu sana Libya wakati wa maandamano yaliyopelekea machafuko na kisha kupinduliwa Ghadaffi kwamba serikali ya Libya ilkuwa inavunja haki za binadamu kwa kutumia nguvu kuzuia maandamano hadi ikafikia kupeleka majeshi ya NATO na wakafanikiwa kuung'oa utawala uliokuwepo lakini juzi hapa Marekani yenyewe imefanya vitendo vilevile dhidi ya waandamanaji na hali ni kimyaaa hakuna anayekohoa dhidi ya huyo baba na mtetezi maahuhuri wa demokrasia. Sasa hapo kama una akili pima uone,wao wakifanya hakuna shida sisi tukifanya tunaambiwa ni kinyume na demokrasia.
Kuna takwa la viongozi kupokezana madaraka, ni zuri tena sana lakini demokrasia hiyo hyo inasema sauti ya wengi ndiyo iamue, kwa mafano katiba zinaeleza mihula ya urais lakini demokrasia hiyohiyo inasema hata hiyo katiba inaweza kubadilishwa kwa sauti za wengi. Ni sawa kuna mihula ya urahisi inayoruhusiwa kikatiba lakini katiba ni yetu ipo kutusaidia na sisi ndo tunaoitengeneza vilevile sisi ndio wenye nguvu ya kusema kifungu fulani hapa tusikitumie na tuakakibadilisha kwa kufuata taratibu zote, tukikubaliana ni sawa maana sauti ya wengi ndiyo mwamuzi. Ajabu sauti ya engi kwenye hili jambo wenzetu hawapendi kulisikia, mi nadhani ni sahihi tu rais kama anakubalika na watu wake na wamekubali kutengeneza katiba yao hivyo, akae tu bila kujali ni muda gani ali mradi katiba imetengenezwa na wanachi na imefuata utaratibu halali. Mfano wa hili juzi tu hapa wananchi wa Urusi wameridhia mabadiliko ya katiba ya kumruhusu Putin kuongoza hadi 2036 ikiwa aataendelea kugombea na kushinda, lakini kwa sababu ni Ulaya hutasikia chokochoko, tatizo ni Afrika tukiamua mambo kama hivyo lazima tukosolewe, wanasiasa wetu wachochewe upuuzi na wao bila kujitambua wanafuata tu bila kujua kuwa wanacheza mdundo wa mabeberu ambao daima wanataka loopholes kama hizo za kubadili badili viongoli ili wapenyeze viongozi "wazuri kwao."
Pamoja na yote hayo simaanishi kuwa hawapo viongozi wa kiafrika au serikali za kiafrika zinazoharibu au zinazoenda kinyume na ustawi mzuri wa wananchi wao, zipo kabisa na hao kweli wanapaswa kurekebisha ili hii demokrasi inayotetewa sana iwasaidie.
Itoshe tu kusema Afrika tunahitaji demokrasia ya kipekee kwa ajili yetu, tusiingiliwe ingiliwe tu na watu wenye malengo yao binafsi dhidi yetu kwa kisingiziao cha demokrasia. Demokrasia ni nzuri kwa mambo mengi lakini tuwe na demokrasia ya kikwetu kwetu isiwe demokrasia inayoamriwa Washington na Brussels
Sent using
Jamii Forums mobile app