ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 664
Miaka kadhaa iliyopita mtoto (wa kiume) wa shemeji yangu , aliacha chuo akiwa ameshamaliza mwaka wa pili eti anataka kufanya biashara ya forex. (Kipindi hicho hata sielewi ndio wanafanyaje).
Ni kwamba, dogo alipotakiwa kwenda chuo hakwenda, nyumbani walipomuuliza akasema chuo amesimamishwa kwa miaka 3 halafu ndio ataendelea. Alipoulizwa kwanini kasimamishwa chuo akasema hakufanya project ndio maana amesimamishwa. Kwa hiyo akasema mpango wake kwa miaka hiyo mitatu atafanya biashara ya forex.
Bahati nzuri mimi nikawa nimetembelea chuoni kwake Mbeya huko. Nikaongea na uongozi nikawaambia kuna kijana wetu amesimamishwa chuo kwa miaka mitatu, imekuwaje? Walimu wakasema matokeo hayajatoka bado, huyo kijana amejuaje kuwa amesimamishwa chuo?
Lakini wakakubali kuwa ni kweli kijana hakufanya project, na usipofanya project unakuwa umedisco na hauruhusiwi kuomba tena chuo upya (Kuanza mwaka wa kwanza) mpaka baada ya miaka mitatu.
Na wakasema usipofanya project kama una sababu za msingi unareport tu kwa mwalimu wa somo unarudia, kama umekosa hela za mahitaji (vitendea kazi) ya project, na ikathibitika hauna uwezo, unaweza kuomba wakakusamehe kulipa ukafanya project kwa kutumia vifaa ambavyo huwa vinabaki kwa wenzio.
WALIMU WAKAKUBALIANA KWA PAMOJA KUWA KIJANA WETU HATAKI KUENDELEA TU NA CHUO, KADANGANYIKA NA STORI ZA MITANDAONI ZA BIASHARA YA FOREX.
Basi nikamrudishia jibu mama yake. Ndugu wakamuuliza kijana mtaji wa biashara ya forex anao? Akasema anaomba ndugu zake wamchangie milioni mbili (2,000,000) apate mtaji. Ndugu wakaona dogo anafanya mzaha. Kwani kufanya biashara ya forex ni lazima uache chuo?
Mama yake singo maza kamlea kwa shida toka mdogo. Baba yake yupo hai ila hajawahi kuishi nae. Anavoenda kuanza chuo mama yake alihaso sana kupata hiyo hela ya kuanzia, mpaka aliwekwa na ndani (lockup) kwa kushindwa kulipa mkopo ambao ndio alimpa dogo akaanze chuo (Mkopo wa HESLB huwa unachelewa kutoka, lazima uwe na pesa ya mahitaji muhimu mwanzo).
Basi ndugu wakakubaliana dogo apewe kishamba (ni wachaga) alime ili apate hizo milioni mbili akafanye hiyo biashara ya forex. Basi wakamtafuta baba yake (Ambaye naye alishakatiwaga kishamba na baba yake) wakamwambia amgawie mwanae sehemu yake ya ardhi alime apate mtaji wa biashara.
Dogo akapewa kishamba chake. Kwani alilima sasa!? 😀😀😀😀. Akaona life gumu akaenda Dar, amejaribu vibarua kibao mpaka saidia fundi kwenye ujenzi, kachemka.
Sasa hivi anaomba asaidiwe arudi chuo akaanze mwaka wa kwanza! Aliacha chuo akiwa anaingia mwaka wa tatu na akiwa anapata mkopo kwa asilimia 100.