Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Sababu HAWANA PESA km Wakandarasi wa NJE Wakandarasi wa Ndani wanategemea wapewe Pesa NDIO wafanye kazi km Pesa hakuna Kazi inadoda Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
Sidhani, lakini daima kumbuka kwamba mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya Watu kuwa masikini au mafukara wa kutupwa ni kutokana na KUKOSEKANA KWA NIDHAMU YA HALI YA JUU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA.
 
Njia 8 amejenga Mchina? Kwanza hamuwalipi mnawakopa unadhani watakua vipi? Zipo kampuni kibao za ndani Zenye uwezo ila hazipewi kazi.
CCM hao na sera yao (isiyoandikwa) ya kula kwa urefu wa kamba. Wanataka makandarasi wazawa nao β€œwajiongeze”!πŸ˜•
 
Stow,

Miradi mingapi mkandarasi wa nje alipewa halafu mradi pesa zikachelewa yeye akachukua pesa za kampuni ili ku-run mradi? Unazo baadhi ya takwimu?

Ili tuone utofauti wa wazawa wa ndani na wa nje sababu ni wao kuweza ku finance miradi pale serikali inapochelewesha au kuna sababu zaidi ya hizo?
 
Nchi inafilisika hii ...hata tusitafute mchawi ni nani...uzalendo kuanzia viongozi mpaka wananchi wake umeisha...kila mtu yupo kimaslahi binafsi na familia yake...kama na wewe unaweza nenda na speed ya nchi...inavyoeenda..Magu alijaribu sana sana lakin ndio hivyo
 
Wakandarasi wazawa ni tatizo kwenye swala la kiwango, wanapopewa mradi wajitahidi kuufanya kwa kiwango cha juu. Wengi wao wanalalamika kutopewa miradi wakipewa wanazingua.
 
Mfano mdogo ni hilo Daraja la Tanzanite
 
Ni kweli tourism, madini na crop export vinatuingizia pesa za kigeni yaani dollar. Ila ukweli ni kwamba kuna low seasonal inflows kutoka kwenye hizo sekta 3 mwisho wa siku tunakuwa na uhaba wa dollar.
Mzee,
Nimependa hoja yako, lakini sababu ya kupungukiwa ni sababu ya low seasonal inflow kutoka katika sekta hizo au kuna la zaidi?

Hivi inawezekana nchi ikawa na high inflow throughout the year?
Kwa kifupi tunapata dollar kidogo sana kupitia utalii, madini na export crops na huku tuna uhitaji mkubwa wa dollar ili kuimport bidhaa nje, kinachotokea ni uhaba wa dollar
Mzee,

Si kwamba tuna export zaidi ya tunavyo-import hivyo pesa inaishia nje?
 
2
namba 2 na 3 imemaliza kila kitu. Namba moja ni relative, kuna miradi wakandarasi wa ndani ndio wanaiweza mingine wa nje ndio wanaiweza, as for now si kila mradi mkandaras wa ndani anaweza

Ni kwlei siasa za kijamaa karne hii hazifanyi kazi tena, even china wameachana nazo
 
Mfano mdogo ni hilo Daraja la Tanzanite
Stow,

Mfano wa daraja la Tanzanite na mfano wa mkandarasi mzawa wa kampuni X uoni bado hakuna utofauti kati ya mzawa na mgeni kipindi pesa inapochelewa na wote wanaweza ku- run miradi hiyo?

Kwani kule makutupora Na Mturuki ni nini kiltokea?
Ujafikiri labda kuna sababu ya zaidi?
 
Unadhani wanaweza Kwa sababu zipi? Umemsikiliza Bashungwa?

Ile miradi ambayo pengine itakuwa spesho saaana ndio itafanywa Kwa ubia na wazawa Ili kufanya knowledge transfer na sio vinginevyo
 
Unadhani wanaweza Kwa sababu zipi? Umemsikiliza Bashungwa?

Ile miradi ambayo pengine itakuwa spesho saaana ndio itafanywa Kwa ubia na wazawa Ili kufanya knowledge transfer na sio vinginevyo
Inategemea na time frame, not miradi yote tunaweza fanya kwa style hiyo.
Although ninwazo zuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…