Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Dola zimeadimika kwasababu wageni wanavuna fedha za miradi kuliko wazawa

Sababu HAWANA PESA km Wakandarasi wa NJE Wakandarasi wa Ndani wanategemea wapewe Pesa NDIO wafanye kazi km Pesa hakuna Kazi inadoda Ila wa NJE hata km Pesa haijaingia wanatumia za KWAO huku wakisubiria Pesa iingie ilimradi mradi usiishie NJIANI
Sidhani, lakini daima kumbuka kwamba mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya Watu kuwa masikini au mafukara wa kutupwa ni kutokana na KUKOSEKANA KWA NIDHAMU YA HALI YA JUU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA.
 
Njia 8 amejenga Mchina? Kwanza hamuwalipi mnawakopa unadhani watakua vipi? Zipo kampuni kibao za ndani Zenye uwezo ila hazipewi kazi.
CCM hao na sera yao (isiyoandikwa) ya kula kwa urefu wa kamba. Wanataka makandarasi wazawa nao “wajiongeze”!😕
 
Nitatoa mfano:

Kuna Mkandarasi X wa Mradi wa Umeme au Maji I think mojawapo kati hizo Ila nahisi ni Mradi wa Maji Mkoa fulani, Mkandarasi X ni Mkandarasi mzawa, alipewa tenda kwenye HUO Mradi Ila mradi Pesa ilichelewa kwa HIO ukakwama alichofanya alichukua Pesa yake akaongezea kwenye Mradi ili mradi uishe usisimame na NDIO wanavyofanya ni Pesa za Kampuni SIO Pesa za mtu binafsi, sasa SIO Wakandarasi wote wanaoweza kufanya HIVYO wengi wakikosa Pesa Mradi unafeli

Nahisi hapo nitakua nimeeleweka
Stow,

Miradi mingapi mkandarasi wa nje alipewa halafu mradi pesa zikachelewa yeye akachukua pesa za kampuni ili ku-run mradi? Unazo baadhi ya takwimu?

Ili tuone utofauti wa wazawa wa ndani na wa nje sababu ni wao kuweza ku finance miradi pale serikali inapochelewesha au kuna sababu zaidi ya hizo?
 
Nchi inafilisika hii ...hata tusitafute mchawi ni nani...uzalendo kuanzia viongozi mpaka wananchi wake umeisha...kila mtu yupo kimaslahi binafsi na familia yake...kama na wewe unaweza nenda na speed ya nchi...inavyoeenda..Magu alijaribu sana sana lakin ndio hivyo
 
Wakandarasi wazawa ni tatizo kwenye swala la kiwango, wanapopewa mradi wajitahidi kuufanya kwa kiwango cha juu. Wengi wao wanalalamika kutopewa miradi wakipewa wanazingua.
 
Stow,

Miradi mingapi mkandarasi wa nje alipewa halafu mradi pesa zikachelewa yeye akachukua pesa za kampuni ili ku-run mradi? Unazo baadhi ya takwimu?

Ili tuone utofauti wa wazawa wa ndani na wa nje sababu ni wao kuweza ku finance miradi pale serikali inapochelewesha au kuna sababu zaidi ya hizo?
Mfano mdogo ni hilo Daraja la Tanzanite
 
Ni kweli tourism, madini na crop export vinatuingizia pesa za kigeni yaani dollar. Ila ukweli ni kwamba kuna low seasonal inflows kutoka kwenye hizo sekta 3 mwisho wa siku tunakuwa na uhaba wa dollar.
Mzee,
Nimependa hoja yako, lakini sababu ya kupungukiwa ni sababu ya low seasonal inflow kutoka katika sekta hizo au kuna la zaidi?

Hivi inawezekana nchi ikawa na high inflow throughout the year?
Kwa kifupi tunapata dollar kidogo sana kupitia utalii, madini na export crops na huku tuna uhitaji mkubwa wa dollar ili kuimport bidhaa nje, kinachotokea ni uhaba wa dollar
Mzee,

Si kwamba tuna export zaidi ya tunavyo-import hivyo pesa inaishia nje?
 
Twende kazi..😅
 

Attachments

  • A405E4D0-EE4D-4FC2-8109-5BAA022DC594.jpeg
    A405E4D0-EE4D-4FC2-8109-5BAA022DC594.jpeg
    157.6 KB · Views: 3
2
Kila siku tunalia kuhusu kuadikika Kwa Dola licha ya juhudi za kukuza Uchumi lakini hakuna ambae anajadili jambo Hilo Kwa kuangalia sababu za msingi.

Mojawapo ya vitu vinavyosababisha kuadikika Kwa Dola Nchini no hizo hapa 👇

1. Kuwapa kazi za Ujenzi wakandarasi wa kigeni badala ya wazawa Kwa visingizio vya hawana uwezo na uzoefu(wageni hulipwa Kwa Dola)

2. Kuagiza bidhaa nyingi ambazo tunaweza Kuzalisha wenyewe ndani ya mwaka eg maziwa,ngano,Mafuta ya kula,sabuni,vyakula vya mifugo,mbegu nk

3. Kukwamisha uwekezaji kutoka Nje kutokana na mitizamo ya siasa za ujamaa(kusema Nchi imeuzwa Kwa Waarabu,kuwa na sera ambazo hazitabiriki,Urasimu wa Kiserikali na Rushwa) eg miradi ya Lindi LNG na Liganga imekwama kutokana na siasa uchwara.

---
WAGENI WAVUNA FEDHA ZA MIRADI KULIKO WAZAWA

SERIKALI imesema asilimia kubwa ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inawanufaisha wageni kutoka nje ya nchi kuliko wazawa.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema bungeni Dodoma kuwa sababu kubwa inayochangia hali hiyo ni uwezo mdogo wa makandarasi wa ndani wa kifedha, mitambo na wataalamu hivyo inakuwa vigumu kwao kushindana kwenye zabuni za kazi na makandarasi kutoka nje hasa kampuni za Kichina.

Bashungwa amesema hayo akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni Dodoma jana. Alisema kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Usajili wa Makandarasi, kati ya miradi 36,839, wazawa walitekeleza miradi 35,351 sawa na asilimia 95.9 ya miradi hiyo.

Hata hivyo, Bashungwa amesema miradi iliyotekelezwa na wazawa ni midogomidogo yenye thamani ya Sh trilioni 23.749, sawa na asilimia 38.5 ya thamani ya miradi yote iliyosajiliwa na kutekelezwa katika kipindi hicho ambayo ni Sh trilioni 61.638.

“Hivyo, makandarasi wa nje ambao ni takribani asilimia 4.1 walitekeleza miradi michache yenye thamani kubwa (asilimia 61.5 ya thamani ya miradi yote),” amesema Bashungwa.

Kwa mujibu wake, kuna kampuni 14,800 za ndani za makandarasi, za ushauri wa wahandisi ni 252 na kampuni za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ni 461.

Chanzo: Habari Leo

My Take
Naunga mkono wazo la Bashungwa kuanza kuwaamini Wakandarasi Wazawa.Sheria hii isiishie Wizara ya Ujenzi pekee Bali Taasisi zote.Tanzania sio Mali ya Wachina pekee.
namba 2 na 3 imemaliza kila kitu. Namba moja ni relative, kuna miradi wakandarasi wa ndani ndio wanaiweza mingine wa nje ndio wanaiweza, as for now si kila mradi mkandaras wa ndani anaweza

Ni kwlei siasa za kijamaa karne hii hazifanyi kazi tena, even china wameachana nazo
 
Mfano mdogo ni hilo Daraja la Tanzanite
Stow,

Mfano wa daraja la Tanzanite na mfano wa mkandarasi mzawa wa kampuni X uoni bado hakuna utofauti kati ya mzawa na mgeni kipindi pesa inapochelewa na wote wanaweza ku- run miradi hiyo?

Kwani kule makutupora Na Mturuki ni nini kiltokea?
Ujafikiri labda kuna sababu ya zaidi?
 
2

namba 2 na 3 imemaliza kila kitu. Namba moja ni relative, kuna miradi wakandarasi wa ndani ndio wanaiweza mingine wa nje ndio wanaiweza, as for now si kila mradi mkandaras wa ndani anaweza

Ni kwlei siasa za kijamaa karne hii hazifanyi kazi tena, even china wameachana nazo
Unadhani wanaweza Kwa sababu zipi? Umemsikiliza Bashungwa?

Ile miradi ambayo pengine itakuwa spesho saaana ndio itafanywa Kwa ubia na wazawa Ili kufanya knowledge transfer na sio vinginevyo
 
Unadhani wanaweza Kwa sababu zipi? Umemsikiliza Bashungwa?

Ile miradi ambayo pengine itakuwa spesho saaana ndio itafanywa Kwa ubia na wazawa Ili kufanya knowledge transfer na sio vinginevyo
Inategemea na time frame, not miradi yote tunaweza fanya kwa style hiyo.
Although ninwazo zuri
 
Back
Top Bottom