Inawezekana pia ikawa sababu kumbuka hapo kati Kuna mikopo mingi tumeomba inawezekana ndo pesa imeingia
Yeah.
Tatizo serikali haina uwazi hatujui kwa uhakika.
Kuna siku wakati wa Covid kulikuwa na mkopo wa IMF, mimi na rafiki zangu wachambuzi tukawa tunatafuta habari za ule mkopo, terms zake, duration etc.
Kuna watu walikuwa wanasema serikali inakopa sana (Ndugai camp) na kuna watu walikuwa wanasema kukopa si tatizo, tatizo ni matumizi ya mkopo na terms zake. Tukawa tunatafuta terms za mkopo, hata press release kutoka serikalini.
Serikali haikuwa imetoa tamko lolote kuhusu ule mkopo. Kila kitu siri.
Ilibidi tupate taarifa za mkopo kutoka tovuti ya IMF.
Kitu cha kuchekesha ni kwamba, terms za ule mkopo hazikuwa mbaya, ulikuwa wa grace period nzuri bila interest, kama msaada fulani. Yani serikali inaficha hata taarifa ambazo zingekuwa zinaweza kusaidia watetezi wa serikali kuutetea mkopo.
Kwa sababu kuna utamaduni wa kufichaficha kila kitu tu.
Kama hapa inawezekana serikali imefanya mambo fulani mazuri ya kuongeza dollar supply na kushusha bei ya dollar, lakini hata rais akisema anasema juu kwa juu kama alivyosema kwenye msiba wa Mafuru hupati detail wamefanya nini.
Na labda unaweza kusema rais tunamuonea yeye si mchumi na anaweza kujaribu kuelezea akaharibu mambo, it's Samia after all, she does not know evacuation from eviction.
Lakini vipi BOT? Vipi wizara ya fedha?
Mbona inaonekana kama wamefanya kazi nzuri kudhibiti supply na bei ya dollar lakini hatuwasikii wakisema wamefanya nini?
Au ndiyo wamefanya tatuzi za muda mfupi kama kukopa wakati tatizo la muda mrefu la balance of trade lipo pale pale?
Kwa sababu, kama hatuna exports za kutosha, tunapambana na dollar supply kwa kukopakopa tu, dollar itapanda tena muda si mrefu.