Dollar yaanza kushuka kwa kasi

Dollar yaanza kushuka kwa kasi

Hapo ukichanganya na mauzo ya nje kwa bidhaa kadha wa kadha
Bongo uwe makini na taarifa hasa za media. Toa mwenyewe kwa taasisi husika, japo napo Kuna muda inaweza kuwa ndivyo sivyo kulingana na mazingira.

Hii taarifa ya citizen ya mwezi uliopita msome waziri wa madini uone anachosema ulinganishe na hiko
 
Ipaste mkuu sijalipia citizen.
 
Hiyo ni moja ya sababu lakini ishu kubwa ya kuweza kustabilize currency ni kuuza sana nje, ndo maana tunasema labda ya mauzo ya bidhaa njee hasa kwa kuanzia oktoba mpaka sasa yamepelekea kupatikana kwa usd. Mauzo ya njee ni pamoja na hiyo dhahabu kumbuka kama walifanikiwa kununua 20 ya manunuzi ina maana Kuna dhahabu ya usd 370,000,000 na watu binafsi Sasa ukiweka na bidhaa nyinginezo bado unakuta Kuna mzigo wa dollar umeingia tu
Mkuu hayo mauzo ya nje tulijadili kila mwaka yanaongezeka kwa nn dollar haikushuka? Hili ndio swali

Pia kuipata dhahabu kutoka oktoba hadi sasa kwa hiyo 20% sio rahisi. Na pia kuiuza na kuleta matokeo leo ndani ya mwezi haiwezekani.
 
Mimi ni reflect kulingana na hiyo taarifa kuwa kama manunuzi yalifikia kg 800 basi Kuna asilimia 80 ya 100 imeuzwa njee ambayo ndo unakuja kupata 370mil.
Mpaka sasa hatujapata jibu kwanini
 
Inawezekana pia ikawa sababu kumbuka hapo kati Kuna mikopo mingi tumeomba inawezekana ndo pesa imeingia
Yeah.

Tatizo serikali haina uwazi hatujui kwa uhakika.

Kuna siku wakati wa Covid kulikuwa na mkopo wa IMF, mimi na rafiki zangu wachambuzi tukawa tunatafuta habari za ule mkopo, terms zake, duration etc.

Kuna watu walikuwa wanasema serikali inakopa sana (Ndugai camp) na kuna watu walikuwa wanasema kukopa si tatizo, tatizo ni matumizi ya mkopo na terms zake. Tukawa tunatafuta terms za mkopo, hata press release kutoka serikalini.

Serikali haikuwa imetoa tamko lolote kuhusu ule mkopo. Kila kitu siri.

Ilibidi tupate taarifa za mkopo kutoka tovuti ya IMF.

Kitu cha kuchekesha ni kwamba, terms za ule mkopo hazikuwa mbaya, ulikuwa wa grace period nzuri bila interest, kama msaada fulani. Yani serikali inaficha hata taarifa ambazo zingekuwa zinaweza kusaidia watetezi wa serikali kuutetea mkopo.

Kwa sababu kuna utamaduni wa kufichaficha kila kitu tu.

Kama hapa inawezekana serikali imefanya mambo fulani mazuri ya kuongeza dollar supply na kushusha bei ya dollar, lakini hata rais akisema anasema juu kwa juu kama alivyosema kwenye msiba wa Mafuru hupati detail wamefanya nini.

Na labda unaweza kusema rais tunamuonea yeye si mchumi na anaweza kujaribu kuelezea akaharibu mambo, it's Samia after all, she does not know evacuation from eviction.

Lakini vipi BOT? Vipi wizara ya fedha?

Mbona inaonekana kama wamefanya kazi nzuri kudhibiti supply na bei ya dollar lakini hatuwasikii wakisema wamefanya nini?

Au ndiyo wamefanya tatuzi za muda mfupi kama kukopa wakati tatizo la muda mrefu la balance of trade lipo pale pale?

Kwa sababu, kama hatuna exports za kutosha, tunapambana na dollar supply kwa kukopakopa tu, dollar itapanda tena muda si mrefu.
 
Mimi ni reflect kulingana na hiyo taarifa kuwa kama manunuzi yalifikia kg 800 basi Kuna asilimia 80 ya 100 imeuzwa njee ambayo ndo unakuja kupata 370mil.
Mpaka sasa hatujapata jibu kwanini
Bata ingekuwa kweli. Kg800 za dhahabu haiwezi kuwa $370mil. $370mil ni kama bilioni 900+. Haiwezekani

Pia nakusisitiza mabadiliko hayawezi kuwa ndani ya mwezi. Kila mwaka tunapata $3.3bilion unahisi kwa nn haikushusha dollar? Alafu ine ishushwe na hiki kiasi kidogo mno?
 
Mkuu hayo mauzo ya nje tulijadili kila mwaka yanaongezeka kwa nn dollar haikushuka? Hili ndio swali

Pia kuipata dhahabu kutoka oktoba hadi sasa kwa hiyo 20% sio rahisi. Na pia kuiuza na kuleta matokeo leo ndani ya mwezi haiwezekani.
Kila mwaka mauzo yakuwa lakini ilikuwa ngumu kuyatrack mfano nimekupa wa dhahabu Sasa hivi unalazimishwa kuuzia kwenye masoko yanayojulikana kwa hiyo hata traceability inakuwepo.
Lakini ukija kwenye export mwaka huu huwezi linganisha na mwaka jana mfano tu cashewnut 2023 export ilikuwa 250,000tonne Lakin kwa mwaka huu mauzo yashafika 338,000 tones na bado minada inaendelea, vile kwenye mazao kama ufuta na mbaazi .
Chukulia tu kwa minada mpaka November dhamani ya korosho iliyouzwa minadani ilikuwa imefika Zaid usd 400mil wakati mwaka jana export jumla ilikuwa usd 225.607594mil huoni kama Kuna gap kubwa sana
 
Bata ingekuwa kweli. Kg800 za dhahabu haiwezi kuwa $370mil. $370mil ni kama bilioni 900+. Haiwezekani

Pia nakusisitiza mabadiliko hayawezi kuwa ndani ya mwezi. Kila mwaka tunapata $3.3bilion unahisi kwa nn haikushusha dollar? Alafu ine ishushwe na hiki kiasi kidogo mno?
Hapa ni assumption ila still yet mwenye data Kamil ni Bot
 
Bata ingekuwa kweli. Kg800 za dhahabu haiwezi kuwa $370mil. $370mil ni kama bilioni 900+. Haiwezekani

Pia nakusisitiza mabadiliko hayawezi kuwa ndani ya mwezi. Kila mwaka tunapata $3.3bilion unahisi kwa nn haikushusha dollar? Alafu ine ishushwe na hiki kiasi kidogo mno?
Sijamanianishq kg 800 namaanisha kama walinunua kg 800 inamaana Kuna kama kg 4000 zimeuzwa nje ambayo imepelekea kwenye 370mil
 
Kila mwaka mauzo yakuwa lakini ilikuwa ngumu kuyatrack mfano nimekupa wa dhahabu Sasa hivi unalazimishwa kuuzia kwenye masoko yanayojulikana kwa hiyo hata traceability inakuwepo.
Lakini ukija kwenye export mwaka huu huwezi linganisha na mwaka jana mfano tu cashewnut 2023 export ilikuwa 250,000tonne Lakin kwa mwaka huu mauzo yashafika 338,000 tones na bado minada inaendelea, vile kwenye mazao kama ufuta na mbaazi .
Chukulia tu kwa minada mpaka November dhamani ya korosho iliyouzwa minadani ilikuwa imefika Zaid usd 400mil wakati mwaka jana export jumla ilikuwa usd 225.607594mil huoni kama Kuna gap kubwa sana
Mauzo yalikua ngumu kuyatrack? Hapa nazungumzia mauzo rasmi hayo ambayo hayajulikani Wala hayapo kwenye reports za BOT. Mauzo rasmi ni $3.3bil kwa mwaka. Swali langu haya yalishindwa vipi kushusha dollar?

Export kila mwaka inaongezeka, swali langu kwako hayo maongezeko ya kila mwaka kwa nn hayakushusha dollar? Tulikua na export ya $5bil tukaenda Hadi 8 na 10, kwa nini hapo dollar haikushuka na kulikua na ongezeko kubwa la export value? Hilo ndio swali langu muda wote

Kuhusu korosho, hizo tani tumewahi kuzalisha zaidi ya hizo tani na tukaingiza zaidi ya hizo za mwaka huu. Kwa nn dollar haikushuka??

Au nibadilishe swali, kwa nn mwaka huu dollar ilipanda sana ikiwa export value haikuwahi kushuka? Nini kilifanya dollar ipande sana?
 
Kg 4000?? Huo utani sasa, tunaanza kujadili kwa kubahatisha.
Kama Bot walinunua kg 800 kwa oktoba ambayo ni 20% ya manunuzi inamaana Kuna 4000kg za dhahabu ziliuzwa nje ambayo ukiconvert 20% ya 4000 unapata kg 800kg kipi kigumu hapo
 
Kama Bot walinunua kg 800 kwa oktoba ambayo ni 20% ya manunuzi inamaana Kuna 4000kg za dhahabu ziliuzwa nje ambayo ukiconvert 20% ya 4000 unapata kg 800kg kipi kigumu hapo
Mkuu umekomalia kg 800., Kg 800 zinaweza vipi kushusha dollar haraka ndani ya mwezi?

Hata zikiwa kg4000 kwa mwaka bado haziwezi kushusha dollar. Ndio maana nilikuuliza export value ilikua $5bil ikapanda hadi $10bil. Kwa nn hapo dollar haikushuka Kama issue ni kuongezeka kwa exporr value?
 
Kwa kweli hali ya biashara imekuwa ngumu sana hasa sisi tunaotegemea kuuza bidhaa nje miez michache kabla serikali haijavamia biashara ya mahindi kwa kujifanya mnunuzi mkuu ili iwauzie zambia tulikuwa tunapeleka mahindi zambia wenyewe na ilitulipa sana maana kwacha ya zambia ilikua juu kulinganisha na shiling ya tanzania hivyo tulipendelea kuuza kwa kwacha then tunarudi tunduma kubadili tunapata sh. Za kutosha kwa sasa kwacha imeporomoka sana ukiuza ukapewa kwacha ukija kubadili upate tsh. Inakukata vibaya sana hii imepelekea kuliua soko la zambia kwa wafanya biashara wa tz imetulazimu tuiuzie serikali ambayo inatukopa kwa muda usiojulikana kwa kifupi serikali imeua export kabisa hasa ya mazao na bei hazipandi kabisa upande wa nchi jirani huku thamani ya pesa zao ikizidi kushuka dhidi ya pesa yetu kwa kweli serikali imetuumiza sana wafanya biashara
 
Sasa dola inashuka well lakini ktk exportation bado inaleta shida maana inashuka kila sehemu hivyo ukiuza bidhaa zako nje inabidi utumie hiyo hiyo tz sh. ambapo bei inakua bado ipo chini kwa kifupi inakua hailipi
 
Back
Top Bottom