Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Hii kadhia huenda inawakuta wengi, nilikwenda ofisi ya 062 kupata line ya simu siku ya Ijumaa wiki iliyopita nikapewa na kuanza kuitumia, inavyoonekana hii namba ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine huko nyuma akaitelekeza, kinachonikuta hadi sasa ni wanawake 11 wananitumia meseji na kupiga simu tuhuma nyingi tu.
- Ati nimetelekeza mimba
- Nimetelekeza watoto
- Nadaiwa ada za watoto
- Nakwepa kulipa kodi ya chumba
- Na meseji za mahusiano mapya nyingi
- Wanaume nao wananishambulia kuwa niachane na wapenzi wao wengine wananisaka