Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

Domant phone numbers wanazogawiwa wateja wapya

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Hii kadhia huenda inawakuta wengi, nilikwenda ofisi ya 062 kupata line ya simu siku ya Ijumaa wiki iliyopita nikapewa na kuanza kuitumia, inavyoonekana hii namba ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine huko nyuma akaitelekeza, kinachonikuta hadi sasa ni wanawake 11 wananitumia meseji na kupiga simu tuhuma nyingi tu.
  1. Ati nimetelekeza mimba
  2. Nimetelekeza watoto
  3. Nadaiwa ada za watoto
  4. Nakwepa kulipa kodi ya chumba
  5. Na meseji za mahusiano mapya nyingi
  6. Wanaume nao wananishambulia kuwa niachane na wapenzi wao wengine wananisaka
Kwa mtindo huu wapo wanaouziwa matatizo na mitandao ya simu kwa kugawa namba hizo kwa wateja wapya, imagine mtu anaambiwa atasakwa awe dead au live.
 
Back
Top Bottom