Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Imetangazwa dakika chache zilizopita na vyombo vya Habari

=====

Rais wa zamani Donald Trump kutoka chama cha Republican, ameshinda Uchaguzi wa Marekani.
View attachment 3144969
Chanzo: Spectator Index

Donald Trump ameoa mara tatu, Ivana na Marla Maples, mke wa kwanza na wa pili mtawalia ambao wote ametalikiana nao. Mke wake wa sasa ni Bi Melania.

Bwana Trump ana watoto watoto watano, watatu wa kiume Donald Trump Jr, Eric, Barron na watoto wawili wa kike Ivanka na Tiffany.

Rais huyo wa Zamani wa Marekani alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita.

Babake Fred alikuwa tajiri aliyemilki majumba na babu zake Trump walikua wahamiaji kutoka Ujerumani.

Mamake Mary alikuwa mzaliwa wa Scotland.
View attachment 3144983
Tangu utotoni, Trump alikuwa mtundu na wazazi wake walimpeleka shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi mjini New York.

Baadaye alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, kitivo cha elimu ya biashara mwaka wa 1968.

Alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha kadiri, viungani mwa New York.

Hata hivyo Donald Trump alikuwa na ndoto ya kufanya biashara nje ya makaazi ya Queens na Brooklyn.

Aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyowekwa na utawala wa Reagan miaka wa 1980.

Yapo mahoteli, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai nembo yake ikiwa ni Trump.

Ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking'aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, "The Apprentice," katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.
Wahooo!
Furaha sana kwangu asubuhi ya leo.
 
Chombo gani wewe hapo BBC,CNN na aljazeera wanasema ameshinda majimbo mawili makubwa bado mengine wewe jamaa muongo sana

USSR

Kuna wenzako msibani huku:

IMG_20241106_100316.jpg
 
Wamnadi muda mwingi wakati ndio alikuwa VP kwa miaka 4?
Kamala Harris hakuwa Mgombea sahihi kwa kiti cha uRais wa Marekani kwa kushindana na Trump. Democrats wangejifunza kupitia kwa Hilary Clinton kwenye Uchaguzi wa mwaka 2016. Uchaguzi huo ungekuwa kama Pilot Project kwa Democrats ili kuweza kumteua mtu sahihi wa kushindana na Trump.
Narudia tena kusema kwamba Democrats walipiga mahesabu vibaya kwenye Uchaguzi huu.
 
Kamala Harris hakuwa Mgombea sahihi kwa kiti cha uRais wa Marekani kwa kushindana na Trump. Democrats wangejifunza kupitia kwa Hilary Clinton kwenye Uchaguzi wa mwaka 2016. Uchaguzi huo ungekuwa kama Pilot Project kwa Democrats ili kuweza kumteua mtu sahihi wa kushindana na Trump.
Narudia tena kusema kwamba Democrats walipiga mahesabu vibaya kwenye Uchaguzi huu.
Biden pamoja na uzee wake nadhani angekuwa competitive kushinda Kamala.
 
Rais wa Marekabni sio Magufuli mlipa kisasi😂
Aaah, subiri uone na endelea kuamini hawalipi kisasi.

Nadhani ulikuwa mtoto wakati George W. Bush alipoivamia Iraq kulipa kisasi cha baba yake George Bush aliyekuwa rais kabla ya Clinton kutaka kuuliwa na Iraq. Ulitengenezwa uongo wote mpaka ikapatikana sababu ya kumpiga Sadam Hussein.
 
Trump sio Kamala na Biden, hii ni namba nyingine kabisa iliyowafanya Iran wanywee kipindi chake akiwa Rais kabla ya Biden.

Vyuma vilikaza sana Iran, Walisimamiwa ukucha kwenye vikwazo vya kuwabana wasiuze mafute, Hawakuwa na jeuri waliyonayo sasa ya kuuza mapipa milioni kila siku, Biden anawachekea.

Trump kushika Madaraka ni "Mguse Israel uone cha mtemakuni" hajivungi kuonesha mapenzi yake ya wazi kwa Israel kuanzia alipotambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na kuwasaidia Israel kulichukua eneo la Golan Heights, Isis mfupa uliomshinda Obama ilipotezwa mazima kipindi chake.
 
Back
Top Bottom