Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Hivi tuseme Marekani ina demokrasia imara ama demokrasia isiyo na uhalisia?

Yaani mamilooni ya wananchi wanapiga kura kumchagua Rais wamtakaye halafu kura zao zinakuwa useless hazitumiki kuamua nani awe Rais bali kura za watu wachache (Electoral Collage) ndizo zinaamua Rais.

Hii haina maana kwamba maamuzi ya wananchi yanapuuzwa?
Mkuu ipo hivi. Majimbo ya marekani (states) zimepewa idadi fulani ya electoral college kulingana na uwingi wa watu. Mfano carlifonia ina electoral collage 54. North Carolina 16, etc.

Mhombea anayeshinda jimbo husika kwa kura za wananchi pia anashinda hizo electoral college. Mfano kamala kashinda califonia ina maana pia kapata electoral college za carlifonia.

Kwa hivyo ni wananchi ndo huamua mshindi na sio hao wajumbe 538 wa electoral college.

Umeelewa?
 
Hivi Trump ataweza kugombea tena 2028? Au USA hamna wanasiasa kama wa kwetu wa kutafsiri katiba wanavyotaka?
term ni mbili tu. kama utaweza zipata, hii inakua term yake ya pili kwisha kazi
 
Electoral votes, popular votes, majimbo...sijawahi kuelewa namna hawa jamaa wanavyohesabu kura.
Mgombea akishinda jimbo fulani (yaani popular votes kwenye jimbo hilo), basi anapata pia electoral votes kwenye jimbo hilo.

Kwa mfano, Kamala Harris wa California akishinda jimboni kwake, anaondoka na electoral votes 54 (ambazo ni kura za jimbo lake tu). Ndivyo inakuwa kwa majimbo yote, hadi afikishe jumla ya kura 270+

Ni wazi kwamba bila popular votes huwezi kupata electoral votes. Hizi zinategemeana kabisa.
 
1730877029040.png
 
Wamarekani ni wabaguzi sana hasa Hawa weusi,si ajabu ndo mana wamarekani weusi wanabaguliwa mpaka Dunia ya Leo ya mwangaza.

Wamempiga chini Kamala kwa sababu ya uanamke wake na ngozi yake yenye uweusi ndani yake.Naamini wale manguli weupe kama Trump,Elon musk bado wanaamini wao ndo Wana haki na Taifa Hilo,na hata kwa Obama nafikiri walimchagua ili kujarbu kubalance ubaguzi ila hata Leo nafikiri ni doa kubwa kwao.

I hope wanafuraha Sasa mzungu pure ndo kashinda.Suala la Vita na mambo mengine hayatobadilika hata chembe,walichojarbu kuzuia TU ni taifa lao Kua na Mtu mweusi Tena Mwanamke.Tuendelee kuamini hiki kizazi cha hawa weupe ambao waliwahi kututawala,kutubagua,kurunyanyasa na kutupora kua ni Mitume ktk zama hizi
 
Back
Top Bottom