Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%

Aaah, subiri uone na endelea kuamini hawalipi kisasi.

Nadhani ulikuwa mtoto wakati George W. Bush alipoivamia Iraq kulipa kisasi cha baba yake George Bush aliyekuwa rais kabla ya Clinton kutaka kuuliwa na Iraq. Ulitengenezwa uongo wote mpaka ikapatikana sababu ya kumpiga Sadam Hussein.
Hiyo si vita ya juzi tu?
 
Viva Trump, 2020 haikuwa wakati sahihi, ilibidi kina Biden washinde wamarekani wajue kwamba Democrats ni chama kisichojali wamarekani,

Kashinda kwasabau chama cha Harris / Democrats

  • Wanaingiza wanaume waliobadili jinsia kwenye michezo na vyoo vya kike
  • Gharama za maisha zilipanda sana / Mfumuko wa bei
  • Kuingiza maharamia milioni 20 ambao Trump kaahidi kuwatimua
  • Kuruhusu watoto wabadili jinsia bila ridhaa ya wazazi
  • kutoa mimba iliyokomaa miezi 9
  • kuwapuuza Israel, Kamala kawapa support ya wazi Hamas
Yaani Hao democrats wange tawala miaka 4 mingine dunia ingekuwa inashuhudia laana kubwa Sana ambazo hazijawahi kutokea
 
Trump sio Kamala na Biden, hii ni namba nyingine kabisa iliyowafanya Iran wanywee kipindi chake akiwa Rais kabla ya Biden.

Vyuma vilikaza sana Iran, Walisimamiwa ukucha kwenye vikwazo vya kuwabana wasiuze mafute, Hawakuwa na jeuri waliyonayo sasa ya kuuza mapipa milioni kila siku, Biden anawachekea.

Trump kushika Madaraka ni "Mguse Israel uone cha mtemakuni" hajivungi kuonesha mapenzi yake ya wazi kwa Israel kuanzia alipotambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na kuwasaidia Israel kulichukua eneo la Golan Heights, Isis mfupa uliomshinda Obama ilipotezwa mazima kipindi chake.
Hujui kitu
 
No, Biden pia angeshindwa.

Biden alipaswa atangaze mapema zaidi nia yake ya kutogombea tena kiti cha uRais ili kutoa nafasi kwa Watu wengine ambao ni wagombea sahihi & competitive ndani ya chama chake cha Democrats kuweza kuonyesha nia zao za kugombea.
Kile kitendo chake cha kuanza kampeni ndicho kimewagharimu sana Democrats. Inaonesha hawakuwa na uhakika na wanachokifanya - wabahatishaji hata kwenye mambo ya msingi kama urais wa nchi!

Hebu fikiria kama Joe Biden angeshinda tena!

Hilo ndilo limewafanya wafuasi wao wengi wapoteze imani na chama. Halafu, Kamala hakuwa na muda mrefu wa kujiandaa. Miezi mitatu tu ya kampeni halisi, wakati Trump tayari alikuwa mkongwe majukwaani?

Ndiyo maana siku JB anaachia ngazi na Kamala akatangazwa kuwa mgombea rasmi, Trump alidai angeshinda asubuhi na mapema. Akawashukuru JB na Democrats kwa kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho.
 
Wamarekani ni wabaguzi sana hasa Hawa weusi,si ajabu ndo mana wamarekani weusi wanabaguliwa mpaka Dunia ya Leo ya mwangaza.

Wamempiga chini Kamala kwa sababu ya uanamke wake na ngozi yake yenye uweusi ndani yake.Naamini wale manguli weupe kama Trump,Elon musk bado wanaamini wao ndo Wana haki na Taifa Hilo,na hata kwa Obama nafikiri walimchagua ili kujarbu kubalance ubaguzi ila hata Leo nafikiri ni doa kubwa kwao.

I hope wanafuraha Sasa mzungu pure ndo kashinda.Suala la Vita na mambo mengine hayatobadilika hata chembe,walichojarbu kuzuia TU ni taifa lao Kua na Mtu mweusi Tena Mwanamke.Tuendelee kuamini hiki kizazi cha hawa weupe ambao waliwahi kututawala,kutubagua,kurunyanyasa na kutupora kua ni Mitume ktk zama hizi
Hujui kuwa yule Mama ni Mhindi
 
Sio makelele tu Trump kashinda Trump kashinda tuige vitu vya msingi matokeo ya urais yatangazwe siku hio hio ndani ya masaa 24. Kwani tunashindwa vipi kuweka mifumo ya kura kama hio? Tumeweza kununua ndege iweje tushindwe kuweka mifumo thabiti ya uchaguzi? Kumbukeni bila viongozi wa maana tutaendelea kufukuza upepo tu na mark time bila kusogea
 
Sio makelele tu Trump kashinda Trump kashinda tuige vitu vya msingi matokeo ya urais yatangazwe siku hio hio ndani ya masaa 24. Kwani tunashindwa vipi kuweka mifumo ya kura kama hio? Tumeweza kununua ndege iweje tushindwe kuweka mifumo thabiti ya uchaguzi? Kumbukeni bila viongozi wa maana tutaendelea kufukuza upepo tu na mark time bila kusogea
Ngumu sana mkuu! Msimamizi wa Uchaguzi ndo mkwe wa mgombea unadhani kitatokea nini!? Unataka Wanu aombe talaka ehh!?
 
Back
Top Bottom