Mkuu moto usikie tu yaan kuna pori moja nilienda kulima huko machakani basi nikalima pakubwa ikafika muda nimechoka sana na natakiwa kumaliza siku hio hio sasa kumbe kuna kitu nilisahau kule wenyewe hua hawachomi moto mchana kuelekea jioni yaani kuanzia saa 7 kuelekea 11 jioni hukuti mtu anachoma moto kwa sababu ya upepo mkali hada 12 kuelekea saa 1 ndio utakuta watu wanachoma moto
Basi nikaingia pori fanya yangu imefika saa 7 kwenda 8 nimechoka nikasema ngoja nichome hauendi mbali huu, ebanaeee moto unatembea na nyasi na kinyasi kidogo tu kikirukia upande wa pili kinawezaa kuunguza pori zima na ukiwa peke yako hata ufanye nini huwezi kuzima moto unaowaka kila upande
Nikatia kiberiti basi nikaanza kuzuia huku na huku ili moto usihame huwezi amini upepo ulipoongezeka kidogo tu moto ukahama ukahamia pori la pili uzuri kuna Mama yeye mwenyeji wa hilo eneo akaniambia usipokua makini utachoma pori zima hili utaunguza miti yote hii akaanza kunisaidia kuzima kuna sehemu akaniambia niwahi usivuke yaan kumbe kuna sehemu mbele walichimba kanjia akasema ukivuka kale kanjia ndio basi huo moto hauupati, kadadek nikawahi kale kanjia nikakuta ndio umekaribia kuvuka nilipambana ule moto balaa ingawa na mimi uliniunguza ila haukuvuka kale kanjia huku yule mama anasaidia kuzima upande mwingine ningekua peke yangu mngesikia tu kuna pori limeungua huko