Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 10,860
- 18,819
Trump amesema assasin wa Charlie Kirk ameshikwa tayari na amependekeza anyongwe kwa mujibu wa sheria.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Charles Kirk inaaminika yuko mikononi mwa FBI baada ya kukamatwa karibu na kitongoji cha Orem ulioko karibu na jiji la Salt Lake maili 200 kutoka jiji la Utah.
Sehemu hiyo alokamatwa ni masaa manne kwa mtu anesafiri kwa gari na yaaminika kuwa ni nyumbani kwa familia yake.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa ni kwamba mtuhumiwa huyo amekiri kwa baba yake kwamba ni yeye ndiye aliemlenga risasi Charles Kirk alipokuwa akifanya mhadhara na wanafunzi wa chuo kikuu cha Utah.
Raisi Donald Trump amesema katika mtandao wake kwamba ana imani kuwa FBI wanae mtu aliemuua Charles Kirk.
FBI watarajiwa kutoa taarifa muda si mrefu.