Mtuhumiwa wa mauaji ya Charles Kirk inaaminika yuko mikononi mwa FBI baada ya kukamatwa karibu na kitongoji cha Orem ulioko karibu na jiji la Salt Lake maili 200 kutoka jiji la Utah.
Sehemu hiyo alokamatwa ni masaa manne kwa mtu anesafiri kwa gari na yaaminika kuwa ni nyumbani kwa familia yake.
Habari ambazo bado hazijathibitishwa ni kwamba mtuhumiwa huyo amekiri kwa baba yake kwamba ni yeye ndiye aliemlenga risasi Charles Kirk alipokuwa akifanya mhadhara na wanafunzi wa chuo kikuu cha Utah.
Raisi Donald Trump amesema katika mtandao wake kwamba ana imani kuwa FBI wanae mtu aliemuua Charles Kirk.
FBI watarajiwa kutoa taarifa muda si mrefu.
Zoazoa ingeanza palepale kwenye eneo la tukio, yaani mngesombwa balaa 😂😂Ingekuwa ile nchi nyingine sasa!!
Kama aliyeuwawa ni mshirika wa karibu wa Rais basi hadi sasa wangeshashikiliwa watu baki zaidi ya 10 wanahojiwa ni kipigo kama siyo nunda unajikuta unakiri kosa yaishe.
Mkuu ondoa shaka.Jamaa Wajitahidi kudhibiti hali ya usalama huko Vinginevyo nitashindwa kwenda World Cup nikihofia kudunguliwa
Kapiga tukio lakini ndio anaenda kunyongwa hivooYaani muda ule na maliza elimu ya msingi ndio anazaliwa huyu mwamba ila amesha fanya kubwa dunia nzima inamzungumza hali mimi nipo nipo tu!
Mimi ndio niko form three wakati dogo anazaliwa. Ndio hivyo mkuu keshajulikana dunia nzima, sisi tuendelee na ukombozi wa Tanganyika yetu. Labda kuna jambo tunaweza fanya tukaja kukumbukwa na vizazi vijavyo kwenye ardhi yetu.Yaani muda ule na maliza elimu ya msingi ndio anazaliwa huyu mwamba ila amesha fanya kubwa dunia nzima inamzungumza hali mimi nipo nipo tu!
FBI waliahidi kutoa dola 100,000 hivyo utaona jinsi baba yake huyo dogo alivyokuwa hataki masihara.Dogo amekamatwa na Baba yake mzazi baada ya kuwapigia simu FBI waje kumkamView attachment 3470523ata
Ukisoma comments nyingi kwenye social media za US
Dogo kafundishwa na Mzee wake kulenga shabaha Toka akiwa na miaka 11, hawa wenzetu wazungu sometimes ni wajinga haswa.FBI waliahidi kutoa dola 100,000 hivyo utaona jinsi baba yake huyo dogo alivyokuwa hataki masihara.
Hivyo mzee atakunja dola 100,000 na kipigwa tax atabakia na kiasi cha kutosha.