Donald Trump Pamoja na kupigwa Risasi na Kujeruhiwa lakini hapiti kwenye vyombo vya habari kuichafua Marekani kama alivyofanya Lissu kwa Tanzania

Ndugu zangu Watanzania,

Tuna mengi sana ya kujifunza katika tukio la kupigwa Risasi na Kujeruhiwa kwa Mheshimiwa Donald Trump,Rais Mstaafu wa Marekani na mgombea Urais kupitia chama cha Republican mwishoni mwa Mwaka huu.

Imeonyesha namna wenzetu walivyo wazalendo kwa nchi zao,kukomaa kiakili,Imani kwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama,kutanguliza mbele maslahi ya Taifa lao,kujizuia kuzungumza hovyo hovyo bila breki. Tumeona Trump akiwa mtulivu,mwenye subira na kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake na hatimaye kutoa ripoti.

Pamoja na kuwa ananyukana vikali sana na Joe Biden Rais wa sasa wa Marekani katika kuelekea katika kinyang'anyiro cha Urais, lakini hakuna mahali popote pale ambapo Trump ametoa Maneno ya kumshutumu Joe Biden na serikali yake.hakuna alipotoa maneno ya kusema joe Bideni anahusika na jaribio la kutaka kumuua ili kujitengenezea ushindi wa Urais .Hakuna mahali popote pale alipotumia tukio hilo kupata huruma ya wa Marekani au kutaka kuonyesha anataka kura za huruma.

Zaidi tumeona akiwa Bize kupanga mipango yake na mikakati yake kisera na ki ajenda pamoja na kuteua mgombea Mwenza wake anayeamini ni mtu sahihi katika Maono aliyonayo kisera juu ya Marekani mpya na yenye kuleta matumaini kwa wamarekani.

Lakini alipopigwa Risasi Lissu na watu wasiojulikana na baadaye kupata unafuu alianza kuzunguka Dunia nzima kama Jua kuichafua Nchi yetu,kuipaka matope,kutaka kila mtu Duniani aitenge Tanzania na asiipatie Msaada wa aina yoyote ile.Tuliona akihangaika usiku na mchana kutafuta vyombo vya habari kuanzia Ulaya hadi Amerika kumwaga sumu ya kuliangamiza Taifa letu na kutaka iwekewe vikwazo vya kiuchumi ili tufe wote..

Alisahau kwamba watakaoathirika ni ndugu zake na watanzania kwa mamilioni yao.alisahau kuwa Nchi na Taifa letu ni kubwa kuliko mtu yeyote yule na Maslahi yake,alisahau kuwa watu hupita na sote tunapita lakini Taifa letu litaendelea kubakia vizazi kwa vizazi.Alisahau kuwa ni Rahisi kulibomoa Taifa kuliko kulijenga,alisahau kuwa heshima ya Tanzania ilijengwa kwa miaka mingi na kwa akili kubwa na jasho lakini yeye akataka aharibu sifa hiyo ya Taifa letu ndani ya muda mfupi kwa Mdomo wake..

Kwa hakika Lissu na wapinzani alinifanya nimchukie mpaka Kesho na kutokumpenda kabisa .kwa sababu niliona ni mtu asiye mzalendo,mtu wa visasi ,chuki,roho mbaya ,tamaa ya madaraka hata kwa njia ya Damu. Niliona Lissu hana upendo wala hisia za upendo kwa Taifa letu na watanzania kwa ujumla wake.

Tabia hii ya kukosa uzalendo kwa Taifa letu imekuwa ikifanywa sana na viongozi wa CHADEMA mara kwa mara kuichafua nchi yetu kimataifa,kwa kuandika vibarua vyenye kujaa maneno ya uzushi , uongo, uchonganishi na umbeya tu.kuna kipindi upinzani hao hao waliandika vibarua vya kutaka kuzuia pesa ambazo zilipaswa kuja kuwekezwa katika miradi ya Elimu.Kwa hakika ulikuwa ni ujuha na ujinga wa kiwango cha juu sana.

Kwa sababu waliokuwa wanakwenda kuteseka na kuathirika ni watoto wa maskini na wa kipato cha chini.hawa ndio waliokuwa wanakwenda kuwa wahanga wakubwa.

Tujifunze kuwa wazalendo kwa Taifa letu.Tuache tabia ya kulichafua Taifa letu kimataifa.tujifunze kutatua migogoro yetu katika meza ya mazungumzo,tuache kupeleka mambo yetu nje ya nyumba yetu tukifikiri ndio jibu. Sasa Mbona Trump hajakwenda kuishtaki Marekani na kutaka iwekewe vikwazo vya kiuchumi? Kwanini hajafanya hivyo?

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ndugu yangu kumbuka scenario ya kupigwa risasi Trump na Lissu ni mbili tofauti.

Aliyempiga risasi Trump alidhibitiwa muda ule ule na alijulikana fasta tu kwahiyo Trump atalaumu nani wakati mhusika alipatikana na alipigwa risasi akauawa?

Lissu alipigwa risasi mchana kweupe kwenye eneo la makazi ya wabunge na mawaziri tena kwenye eneo lenye ulinzi na hakuna uchunguzi wala taarifa zozote za kupatikana washukiwa.

Licha ya Lissu kuomba uchunguzi huru ufanyike hakuna aliyekuwa tayari kufanya uchunguzi. Katika mazingira kama haya akiilalamikia serikali atakuwa amekosea?
 
Kuna tofauti kubwa sana ktk haya matukio mawili.

. Lisu alipigwa risasi kwa maagizo ya rais wa nchi (dikteta jiwe), wakati Trump kapigwa risasi na mhuni tu.
 
Wewe ungeweza ? Yaani umebaki na kasikio kamoja Kama bundi alafu uanze kulandalanda kwenye korido za TV sijui redio eti kuituhumu serikali ?

Huu muda yupo chimbo wanasayansi wanaangalia namna ya kuunganisha kale kasikio kalikodondoka alafu wakaunge vizuri ndiyo atoke nje kuanza kelele 🙊
 
Kuna tofauti kubwa sana ktk haya matukio mawili.

. Lisu alipigwa risasi kwa maagizo ya rais wa nchi (dikteta jiwe), wakati Trump kapigwa risasi na mhuni tu.
Acha kuropoka.weka ushahidi wa maneno na kauli yako.
 
Una ushahidi dola inahusika .?
Yule kichaa jiwe:-
1. Alikataza wanaccm wenzake kwenda kumuona Lisu hospitali.
2. Alipiga marufuku kumchangia damu.
3. Kama kiongozi wa nchi, hakutoa pole kwa Lisu wala kutoa kauli ya kulaani tukio lile.
4. Alizuia uchunguzi kufanyika.
5. Alimvua ubunge.

Ndiyo maana kafa!
 
Bora ukae kimya unakaza fuvu ndiyo unadhihirisha ukilaza wako. Wewe elimu yako ya MEMKWA inatosha kuwasifia Mama Abdul,Makonda na Kafulila.
Akili yangu huwezi kuifikia hata kwa robo tu.mimi na wewe ni kama Mlima na kichuguu .wewe ni kichuguu tu kwangu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Tuna mengi sana ya kujifunza katika tukio la kupigwa Risasi na Kujeruhiwa kwa Mheshimiwa Donald Trump,Rais Mstaafu wa Marekani na mgombea Urais kupitia chama cha Republican mwishoni mwa Mwaka huu.

Imeonyesha namna wenzetu walivyo wazalendo kwa nchi zao,kukomaa kiakili,Imani kwa vyombo vyao vya ulinzi na usalama,kutanguliza mbele maslahi ya Taifa lao,kujizuia kuzungumza hovyo hovyo bila breki. Tumeona Trump akiwa mtulivu,mwenye subira na kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake na hatimaye kutoa ripoti.

Pamoja na kuwa ananyukana vikali sana na Joe Biden Rais wa sasa wa Marekani katika kuelekea katika kinyang'anyiro cha Urais, lakini hakuna mahali popote pale ambapo Trump ametoa Maneno ya kumshutumu Joe Biden na serikali yake.hakuna alipotoa maneno ya kusema joe Bideni anahusika na jaribio la kutaka kumuua ili kujitengenezea ushindi wa Urais .Hakuna mahali popote pale alipotumia tukio hilo kupata huruma ya wa Marekani au kutaka kuonyesha anataka kura za huruma.

Zaidi tumeona akiwa Bize kupanga mipango yake na mikakati yake kisera na ki ajenda pamoja na kuteua mgombea Mwenza wake anayeamini ni mtu sahihi katika Maono aliyonayo kisera juu ya Marekani mpya na yenye kuleta matumaini kwa wamarekani.

Lakini alipopigwa Risasi Lissu na watu wasiojulikana na baadaye kupata unafuu alianza kuzunguka Dunia nzima kama Jua kuichafua Nchi yetu,kuipaka matope,kutaka kila mtu Duniani aitenge Tanzania na asiipatie Msaada wa aina yoyote ile.Tuliona akihangaika usiku na mchana kutafuta vyombo vya habari kuanzia Ulaya hadi Amerika kumwaga sumu ya kuliangamiza Taifa letu na kutaka iwekewe vikwazo vya kiuchumi ili tufe wote..

Alisahau kwamba watakaoathirika ni ndugu zake na watanzania kwa mamilioni yao.alisahau kuwa Nchi na Taifa letu ni kubwa kuliko mtu yeyote yule na Maslahi yake,alisahau kuwa watu hupita na sote tunapita lakini Taifa letu litaendelea kubakia vizazi kwa vizazi.Alisahau kuwa ni Rahisi kulibomoa Taifa kuliko kulijenga,alisahau kuwa heshima ya Tanzania ilijengwa kwa miaka mingi na kwa akili kubwa na jasho lakini yeye akataka aharibu sifa hiyo ya Taifa letu ndani ya muda mfupi kwa Mdomo wake..

Kwa hakika Lissu na wapinzani alinifanya nimchukie mpaka Kesho na kutokumpenda kabisa .kwa sababu niliona ni mtu asiye mzalendo,mtu wa visasi ,chuki,roho mbaya ,tamaa ya madaraka hata kwa njia ya Damu. Niliona Lissu hana upendo wala hisia za upendo kwa Taifa letu na watanzania kwa ujumla wake.

Tabia hii ya kukosa uzalendo kwa Taifa letu imekuwa ikifanywa sana na viongozi wa CHADEMA mara kwa mara kuichafua nchi yetu kimataifa,kwa kuandika vibarua vyenye kujaa maneno ya uzushi , uongo, uchonganishi na umbeya tu.kuna kipindi upinzani hao hao waliandika vibarua vya kutaka kuzuia pesa ambazo zilipaswa kuja kuwekezwa katika miradi ya Elimu.Kwa hakika ulikuwa ni ujuha na ujinga wa kiwango cha juu sana.

Kwa sababu waliokuwa wanakwenda kuteseka na kuathirika ni watoto wa maskini na wa kipato cha chini.hawa ndio waliokuwa wanakwenda kuwa wahanga wakubwa.

Tujifunze kuwa wazalendo kwa Taifa letu.Tuache tabia ya kulichafua Taifa letu kimataifa.tujifunze kutatua migogoro yetu katika meza ya mazungumzo,tuache kupeleka mambo yetu nje ya nyumba yetu tukifikiri ndio jibu. Sasa Mbona Trump hajakwenda kuishtaki Marekani na kutaka iwekewe vikwazo vya kiuchumi? Kwanini hajafanya hivyo?

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
TRUMP NI MNYAMWEZI OG , LISSU NI MTU YA SINGIDA ....

KINGINE KAMA TAIFA LA TANZANIA , TUMUUNGE MKONO MHE. RAISI wetu SAMIA SULUHU HASSAN , nae ni kiongozi mwenye upendo wa dhati . Kiongozi bora ni yule mpenda watu kuanzia jamii yake paka ya jirani . Mungu bariki viongozi wetu wa Afrika . Mungu ibariki Tanzania
 
Yule kichaa jiwe:-
1. Alikataza wanaccm wenzake kwenda kumuona Lisu hospitali.
2. Alipiga marufuku kumchangia damu.
3. Kama kiongozi wa nchi, hakutoa pole kwa Lisu wala kutoa kauli ya kulaani tukio lile.
4. Alizuia uchunguzi kufanyika.
5. Alimvua ubunge.

Ndiyo maana kafa!
Hakuna hoja yenye mashiko ambayo inathibitisha maneno yako. Wewe ndiye kichaa.
 
Lissu hakuwai kuichafua Tanzania kama nchi, bali aliichafua SERIKALI ya Tanzania ya CCM chini ya Magufuli , pili neno kusema kweli si kuchafua bali alikuwa anaeleza yaliyo wazi,

Sera za Trump ni dhid ya SERIKALI ya Marekani chini ya Biden wala si dhidi ya Nchi ya Marekani,

1. Anakataa Ushoga
2. Sera mbovu ya mambo ya nje na Ushirikiano kimataifa
3. Matumizi mabovu ya walipa kodi wa Marekani kuendelea kutumika kufadhili Mapigano sehemu mbali mbali za dunia
4. Uhamiaji holela ambao haudhibitiwi vema! Na hii Biden amelegeza sana watu wanahamia hamia na kupewa Pesa na Marekani kwamba wanatafta asylum, wakati wananchi baadhi wana shida kibao

Britanicca
 
Back
Top Bottom