BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
DONDOO MUHIMU 10 KUELEKEA UZINDUZI WA FILAMU YA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA YA ROYAL TOUR USIKU HUU.
Na Bwanku M Bwanku.
Usiku wa Leo Jumatatu Aprili 18, 2022 kuanzia Majira ya Saa 8 na nusu Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki, Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaweka historia kubwa kwenye Anga za Kimataifa katika safari ya Serikali ya Awamu ya 6 kupaisha Sekta ya Utalii na Uwekezaji kwa Kushuhudia Uzinduzi wa Royal Tour, Filamu Maalum ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Uzinduzi huu unaotarajia kufuatiliwa Duniani kote, utafanyika kwenye Jumba Mashuhuri la Makumbusho liitwalo Guggenheim Jijini New York na kuhudhuriwa na takribani watu 400 huku Mamilioni kwa Mamilioni ya watu kote Duniani wakifuatilia tukio hilo kupitia mitandao ya Kijamii, Televisheni na Redio.
Mapema leo Jumatatu, Rais Samia alikutana na Meya wa Jiji la New York Bwana Eric Adams kuelekea Uzinduzi wa Filamu hii ya Royal Tour.
Filamu hii ni Turufu muhimu sana kwenda kupaisha Utalii na Uwekezaji wa Nchi yetu na zaidi ya Televisheni 300 za Marekani ikiwemo za Online, za hapa nchini na nyingine nyingi zitarusha Live tukio hili la kihistoria linalokwenda kupaisha Sekta ya Utalii nchini kwa Kutangaza vivutio vyote vya Utalii nchini na maeneo yenye fursa za Uwekezaji kwa ajili ya Uchumi na Maendeleo ya Taifa Tanzania.
Taasisi kubwa za Kibiashara za Kimataifa, Waongoza Utalii wa Kimataifa, Viongozi wa Kisiasa wakubwa, Mashirika ya Kimataifa, Waandishi wa Habari wakubwa na wa Kimataifa na Watanzania waishio Marekani watahudhuria Uzinduzi wa Filamu hii ya Royal Tour.
Dunia nzima itasimama wakati Filamu hii Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York ambapo Mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu.
Kwa Mujibu wa Dkt. Hassan Abbasi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais Samia ya Kuratibu Mpango wa Kuitangaza Tanzania Kimataifa amesema Filamu hii ya Royal Tour inatarajia kuwafikia watu Bilioni 1 katika mwaka mmoja wa kusambaza kwake.
Pia, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ya kusambaza Filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza leo Jijini New York na Aprili 21 Los Angeles, Marekani kisha Dar es Salaaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.
Amesema pia kuwa Filamu itaoneshwa kwenye kumbi za sinema, kwenye ndege, mitandao ya kijamii na yote hayo ikilenga kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kuongeza kwamba, akiwa ziarani nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na makundi mbalimbali ya wasanii na wafanyabiashara ambao watapata wasaa wa kutazama Filamu hiyo inayoonesha fursa za uwekezaji na utalii nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema vivutio vingi vya utalii nchini havijulikani, lakini kupitia filamu hiyo vitajulikana na watalii wengi zaidi watafika Tanzania.
Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Ulimwengu la Forbes, hivyo uamuzi huu wa Rais Samia kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu kama Mhusika Mkuu ni turufu ya Kimkakati sana na itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini.
Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Ni wakati wa Tanzania Kimataifa sasa.
Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.