Dondoo muhimu 10 kuelekea uzinduzi wa filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania ya Royal Tour

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
DONDOO MUHIMU 10 KUELEKEA UZINDUZI WA FILAMU YA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA YA ROYAL TOUR USIKU HUU.

Na Bwanku M Bwanku.

Usiku wa Leo Jumatatu Aprili 18, 2022 kuanzia Majira ya Saa 8 na nusu Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki, Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaweka historia kubwa kwenye Anga za Kimataifa katika safari ya Serikali ya Awamu ya 6 kupaisha Sekta ya Utalii na Uwekezaji kwa Kushuhudia Uzinduzi wa Royal Tour, Filamu Maalum ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Uzinduzi huu unaotarajia kufuatiliwa Duniani kote, utafanyika kwenye Jumba Mashuhuri la Makumbusho liitwalo Guggenheim Jijini New York na kuhudhuriwa na takribani watu 400 huku Mamilioni kwa Mamilioni ya watu kote Duniani wakifuatilia tukio hilo kupitia mitandao ya Kijamii, Televisheni na Redio.

Mapema leo Jumatatu, Rais Samia alikutana na Meya wa Jiji la New York Bwana Eric Adams kuelekea Uzinduzi wa Filamu hii ya Royal Tour.

Filamu hii ni Turufu muhimu sana kwenda kupaisha Utalii na Uwekezaji wa Nchi yetu na zaidi ya Televisheni 300 za Marekani ikiwemo za Online, za hapa nchini na nyingine nyingi zitarusha Live tukio hili la kihistoria linalokwenda kupaisha Sekta ya Utalii nchini kwa Kutangaza vivutio vyote vya Utalii nchini na maeneo yenye fursa za Uwekezaji kwa ajili ya Uchumi na Maendeleo ya Taifa Tanzania.

Taasisi kubwa za Kibiashara za Kimataifa, Waongoza Utalii wa Kimataifa, Viongozi wa Kisiasa wakubwa, Mashirika ya Kimataifa, Waandishi wa Habari wakubwa na wa Kimataifa na Watanzania waishio Marekani watahudhuria Uzinduzi wa Filamu hii ya Royal Tour.

Dunia nzima itasimama wakati Filamu hii Maalum ya kutangaza Utalii wetu wa Tanzania ikizinduliwa pale New York ambapo Mkuu wa Nchi, Rais Samia Suluhu Hassan ni Mhusika Mkuu (Tour Guider) kwenye Filamu hii inayokwenda kueleza kila Vivutio vya Utalii na Uwekezaji vilivyopo nchini ili kuwavuta Watalii na Wawekezaji wengi zaidi Ulimwenguni kuja nchini ili tupate fedha nyingi zaidi kupitia Utalii na Uwekezaji ili tuzipeleke kwenye Uchumi na Maendeleo yetu.

Kwa Mujibu wa Dkt. Hassan Abbasi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais Samia ya Kuratibu Mpango wa Kuitangaza Tanzania Kimataifa amesema Filamu hii ya Royal Tour inatarajia kuwafikia watu Bilioni 1 katika mwaka mmoja wa kusambaza kwake.

Pia, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mikakati mbalimbali imewekwa ya kusambaza Filamu hiyo itakayozinduliwa kwa mara ya kwanza leo Jijini New York na Aprili 21 Los Angeles, Marekani kisha Dar es Salaaam Aprili 28 na Zanzibar Mei 07, 2022.

Amesema pia kuwa Filamu itaoneshwa kwenye kumbi za sinema, kwenye ndege, mitandao ya kijamii na yote hayo ikilenga kuwafikia watu wa makundi mbalimbali na kuongeza kwamba, akiwa ziarani nchini Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan atakutana na makundi mbalimbali ya wasanii na wafanyabiashara ambao watapata wasaa wa kutazama Filamu hiyo inayoonesha fursa za uwekezaji na utalii nchini.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana amesema vivutio vingi vya utalii nchini havijulikani, lakini kupitia filamu hiyo vitajulikana na watalii wengi zaidi watafika Tanzania.

Mhe. Rais Samia kwasasa ni Mwanamke anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa zaidi Barani Afrika na Duniani kwa Mujibu wa Majarida ya Avance Media la Ghana na Jarida la Ulimwengu la Forbes, hivyo uamuzi huu wa Rais Samia kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii wetu kama Mhusika Mkuu ni turufu ya Kimkakati sana na itafanya Ulimwengu mzima kutazama na kufuatilia Filamu hii na kujionea uzuri wa Tanzania na kumiminika kwa wingi kuja nchini.

Watanzania wote Mabibi na Mabwana tuiunge mkono Filamu hii, inakwenda kutusaidia kupandisha idadi ya Watalii kutoka chini ya Milioni 2 wasasa mpaka kufikia Milioni 5 kufikia mwaka 2025 kama ilivyo Mipango yetu ya Ilani ya CCM, Chama kinachoongoza Taifa letu inayotekelezwa na Taifa na Mipango yetu. Ni wakati wa Tanzania Kimataifa sasa.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com.

IMG-20220418-WA0161.jpg


IMG-20220418-WA0128.jpg

IMG-20220418-WA0130.jpg


IMG-20220418-WA0129.jpg


20220418_222418.jpg
 
Wale washamba watakuja hapa na hoja zao za kitoto….Kuwa mshamba ni mzigo mzito kwa taifa
 
Lengo la hiyo filamu ni kushawishi wazungu waje Tanzania.

Kutumia muda mwingi kuwaambia Watanzania mama anazindua filamu yake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

It’s a promotional film kwa ajili ya foreign audience kwa lengo la kuitangaza Tanzania. So ideal mgetumia hizo hela za propaganda kuwalipa Netflix, Apple TV or whatever media platforms which will be showing the film to promote it watu huko mnapolenga waitazame wawe interested nayo.

Bogus people kweli kweli sasa mkishatuambia sisi walalahoi mama anazindua filamu yake leo au mkienda airport kuvizia ndege za watalii baada ya hapo ndio mnataka tuende mbugani wakati bei ya mafuta ya kupikia na unga wa ngano tu mtihani kwetu.
 
Tuwe tuu wakweli mama anahangaika sana japo tupige hatua chanya. Tumtie moyo kwa kumpa sapoti!
 
Lengo la hiyo filamu ni kushawishi wazungu waje Tanzania.

Kutumia muda mwingi kuwaambia watanzania mama anazindua filamu yake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu...
utaumia sana brother.na bado rais wetu anaenda kufanya makubwa zaidi.na maendeleo

umepaniki brother
 
ahhhh uta

utaumia sana brother.na bado rais wetu anaenda kufanya makubwa zaidi.na maendeleo


umepaniki brother
Sasa hapo ni panic kitu gani, hivi wakitumia nguvu kutujulisha uzinduzi wa hiyo filamu sisi ndio target audience au wakienda kuwalazimisha wachonga vinyago mtaani sinema ina faida kwao ndio italeta watalii.

Ni sawa na kutangaza biashara ya bucha maeneo ya baniani kazi bure tu na upotevu wa hela.

Hizo promotional efforts si wangepeleka kwenye communication channels za targeted audience.

Hata communication strategy ya kufanya promotion shida halafu wanajiita wasomi.

Washauri wa mama ni watu ambao ukiwauliza what are the usefulness and differences of ‘above and below’ promotional tactics in reaching the audience; sidhani kama watakujibu. Kwa kuangalia tu huu upuuzi unaoendelea kuelekea uzinduzi wa filamu yake inaonyesha hawajui ata wanachokifanya.
 
Sasa hapo ni panic kitu gani, hivi wakitumia nguvu kutujulisha uzinduzi wa hiyo filamu sisi ndio target audience au wakienda kuwalazimisha wachonga vinyago mtaani sinema ina faida kwao ndio italeta watalii...

Unataka kusema watanzania hawana haki ya kupewa taarifa kuhusiana na hiyo filamu? Mbona roho mbaya zitawaua
 
Unataka kusema watanzania hawana haki ya kupewa taarifa kuhusiana na hiyo filamu? Mbona roho mbaya zitawaua

Mnatabia ya kujitekenya na kucheka wenyewe; nimekuwekea link upitie average promotional budget ya filamu mpya Hollywood ili watu waitazame ni kama $35 million sio ajabu kabisa kutumia zaidi ya $50+ million kwenye promotional tu (achilia mbali mamillioni ya kuitengeneza filamu yenyewe).

Unadhani studios huko hollywood wanatengeneza tu filamu na watu wanafurika kwenda kuangalia theatres (labda afternoon martinee) aimed for stay at home mums.

Ndugu there is a lot of money spent in above the line campaign in order to raise awareness kwenye filamu mpya.

Sasa wewe unatengeneza filamu kwa sababu ya wazungu halafu unatumia hela nyingi kuwaambia watanzania mama anaupiga mwingi; badala ya kutumia muda huo kuhakikisha hiyo filamu inaangaliwa na walengwa wengi as much as possible waje Tanzania.

Sisemi tutumie budget za Hollywood au promotional tactics zao kwa hiko ki-documentary cha ‘bi-tozo’ lakini hiki kinachoendelea sasa is more than pathetic unajiuliza what’s the point ya hizo campaign zisizo na faida kwa filamu yenyewe and it’s intentions.
 
Wakati inazinduliwa SAFARI CHANNEL kipindi cha Hayati Magufuli nilikosoa sana channel hiyo ambayo haitasaidia kukuza utalii, na sababu nilizotoa ni mbili
i) Channel hiyo itashindwa kuutangaza utalii nje ya mipaka ya Tanzania.
ii) Ulimwengu umebadilika kutoka kutazama vipingi vya runinga mpaka kutazama movies

Badala yake nikashauri itengenezwe filamu katika mfumo wa CD na hizo CD zisambazwe kwa mabalozi wetu wote dunia nzima ambao nao watazimbaza kwa sehemu mbalimbali walipo hii itasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka.

Nikiri kusema Rais Samia kakiri kunifurahisha
 
Kama chuki huumiza moyo na kuleta hadi mauti, basi kuna hadi kufika 2025 kuna watu wengi sana watakuwa wamejiua kwa chuki zao dhidi ya huyu mama.....haki ya nani bila Mungu Mkuu, wangekuwa wameshafika ikulu na kumnyofoa roho yake kwa jinsi wasivyompenda kwa sababu tu ya kuwazidi.
 
Izo zote ni mbinu za kula pesa za wananchi hamna jipya nyie iyo Royal tour wamefanya nchi kibao mbona wao awajaweka mbwembwe zote izo acheni wizi wa Kodi za Watanzania
 
UCHAMBUZI- DONDOO MUHIMU KUHUSU FILAMU MAALUM YA KUTANGAZA UTALII NA UWEKEZAJI WA NCHI YETU YA ROYAL TOUR.

Na Bwanku M Bwanku.

Kuelekea kesho Alhamisi kwenye Uzinduzi wa pili wa Filamu ya Royal Tour ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Nchi yetu Tanzania Kimataifa kule Los Angeles, Marekani, Leo Jumatano Aprili 20, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua Dondoo muhimu zote kuhusu Filamu hii ya Royal Tour.

Mpango wa Taifa kwasasa kufikia mwaka 2025 ni kuhakikisha Watalii wanafikia Milioni 5 kwa Mwaka kutoka chini ya Milioni 2 wasasa na ndiyo maana Rais Samia Suluhu Hassan ameweka nguvu kubwa sana kwenye Sekta hii muhimu sana kwa Taifa ili kuhakikisha tunafikia malengo na kulipatia Taifa Uchumi na Fedha nyingi zaidi, na ndiyo maana akaamua kujitoa mwenyewe kama Mkuu wa Nchi kurekodi Filamu hii ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wetu Kimataifa kama Mhusika Mkuu ili ikasaidie hilo. Pata Nakala sasa ya Gazeti lako pendwa la TANZANIA LEO uone umuhimu wa Filamu hii na Dondoo zake zote kuihusu na namna inavyokwenda kulipaisha Taifa Kiuchumi na Uwekezaji.

@

IMG-20220420-WA0044.jpg


IMG-20220420-WA0042.jpg
 
Nashindwa kuelewa hii nchi ina tatizo gani.

Tumeandaa film kwa mabilioni ya shilingi ili kutangaza utalii ili wazungu waje kuona vivutio ikiwa pamoja na wanyama lakini cha ajabu waziri wa Maliasili anatangaza kuruhusu kusafirisha nje ya nchi wanyama hao hao ambao wazungu wangekuja kuwaona na kuliingizia taifa mapato kwa matinki umuhimu wa Royal Tour ni upi?
 
Back
Top Bottom