Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Methali 26:4-12​

Usimjibu mpumbavu kipumbavu, usije ukafanana naye. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.
 
zaburi 23:4
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
 
Umekurupuka kujibu hapo awali ulikuwa unabishana na member mwingine na si mimi ikanibidi nikuulize hilo swali , sasa naona jibu lako limeni point mimi moja kwa moja .
 
Ayubu ananipa karaha sana he remainds me of my late mother and father 🥹🥹🥹
 
Ukisoma kitabu cha Ayubu usome kwa uangalifu sana maana Ayubu aliyasema hayo alipokuwa hamjui Mungu ( alikuwa anasikia sikia tu habari za Mungu , akamtumikia kwa habari alizosikia)


Alipomjua Mungu akaomba msamaha kwa yote aliyoyasema kwanza ,tena akasema wazi kuwa alikuwa anasikia sikia tu ila sasa amemjua


Ayubu 42:1,5-6
[1]Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema.
[5]Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio;
Bali sasa jicho langu linakuona.
[6]Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu
Katika mavumbi na majivu.
 
Yakobo 2:8

Avunjaye amri moja basi amevunja zote
Kwa maana aliye sema usizini ndo aliyesema usiibe [emoji120]
 
🤣🤣🤣Umeamua kutembelea humohumo
Nilifunza mengi sana hasa ukikutana na watu wapenda Pombe..kama hauko imara ni watu wanajua Biblia sijawahi ona..kwa upande wa Ukristo.

Ukikaa vibaya imani yako inaweza ondoka mchana kweupe.

Tuna mengi ya kujifunza na kuisha maisha matamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…