Doto magari na wasomi, mamlaka kuweni makini

Doto magari na wasomi, mamlaka kuweni makini

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Salaam wakuu!

Najua huwa anafanya ki utani utani tu na huwa hamaanishi ila sijajua tunajenga kizazi cha namna gani, Amekuwa akipata endorsement kubwa nyingi kutoka makampuni mengi sana na kupata hela ambazo yeye anaona amekuwa Tajiri na kudharau wasomi.

Kuna namna baadhi ya vitu anatakiwa kukemewa ili ku balance mambo haswa kwenye hiki kizazi ambacho vijana wengi wadogo sana wanashika simu na kutwa kushinda Instagram.

Sawa mimi nimejiajiri kama legal and business consultant, Hapa katikati zilitoka nafasi nyingi sana za walimu na baadhi ya kada mbali mbali serikalini nilikuwa na wasaidia hasa kwenye kuhakiki vyeti na shughuli nyingine za kisheria; Kwa kweli mtaani ni pagumu sana, tena sana ila bado tunaona serikali inataka wataalamu katika kila nyanja.

Wasomi bado wanahitajika sana katika kila nyanja za private na public.
 
Hawa wahuni wanapuuza wasomi na elimu,
Maisha ni kutegemeana.
Huyo Dotto akiumwa ataenda kutibiwa na msomi daktari
Atamtegemea wakili, walimu, wahasibu, rubani, wanajeshi n.k
Siyo busara kubeza taaluma za watu
 
Nadhani wewe ndio umenielewa nasemea kwa vijana wadogo ambao hawajui ku reason vizuri wataona kwamba mtu kama dotto ndio kioo cha jamii so wataacha kusoma na kufuata ambayo anasema dotto
 
Salaam wakuu!

Najua huwa anafanya ki utani utani tu na huwa hamaanishi ila sijajua tunajenga kizazi cha namna gani, Amekuwa akipata endorsement kubwa nyingi kutoka makampuni mengi sana na kupata hela ambazo yeye anaona amekuwa Tajiri na kudharau wasom....
Sijakuelewa wewe msomi wa kitanzani point yako ni ipi?
 
Kama kitu gani aangaliwe,mbona haujakitaja hapo?
Dhihaka, Dharau, na namna anavyosema vibaya juu ya wasomi, inawezekana kabisa atakuwa na nia nzuri sana ila namna ujumbe wake anavyopeleka kwa wasomi. Tunajenga vipi vijana wetu wa kizazi kijacho kwa hawa wanaoitwa influences
 
Salaam wakuu!

Najua huwa anafanya ki utani utani tu na huwa hamaanishi ila sijajua tunajenga kizazi cha namna gani, Amekuwa akipata endorsement kubwa nyingi kutoka makampuni mengi sana na kupata hela ambazo yeye anaona amekuwa Tajiri na kudharau wasomi.

Kuna namna baadhi ya vitu anatakiwa kukemewa ili ku balance mambo haswa kwenye hiki kizazi ambacho vijana wengi wadogo sana wanashika simu na kutwa kushinda Instagram.

Sawa mimi nimejiajiri kama legal and business consultant, Hapa katikati zilitoka nafasi nyingi sana za walimu na baadhi ya kada mbali mbali serikalini nilikuwa na wasaidia hasa kwenye kuhakiki nyeti na shughuri nyingine za kisheria; Kwa kweli mtaani ni pagumu sana, tena sana ila bado tunaona serikali inataka wataalamu katika kila nyanja.

Wasomi bado wanahitajika sana katika kila nyanja za private na public.
Acha Doto Magari atunyooshe Wasomi wa Tanzania na tena namuunga mkono 100% kwa jinsi anavyotudharau na namuomba asichoke Kutudharau Kwake. Eti kabisa nawe Unaumia...!!

Kama Msomi kamaliza Chuo Kikuu lakini hawezi hata tu kubuni Wazo la Biashara lakini Yeye ( Doto Magari ) asiye na hata Elimu kaweza kuwa Mbunifu akitudharau anatukosea?
 
Sijakuelewa wewe msomi wa kitanzani point yako ni ipi?
Boss mimi sio msomi, ila point yangu ni namna dhihaka, Dharau, kejeli juu ya wasomi. Unajua inawezekana akawa ana point nzuri sana lakini namna anavyowasilisha kwenye jamii kuhusu wasomi ikawa sio sawa haswa kwa vijana wetu wadogo, inawezekana wakaja kudharau kusoma na kuona maisha ni kama anavyoishi dotto, kwa maana ya kushika pesa tu ndio mwisho wa maisha pasipo kusoma
 
Back
Top Bottom