Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

Kwani ni lazima MAHOJIANO yawe ya kushambuliana kiasi hicho ?!!!

Kwa hiyo ni lazima mwandishi wa habari awe kama Tim Sebastian na Christian Amanpour kila wakati katika MAHOJIANO?!!!

Ninajiuliza je kila MAHOJIANO aliyoyafanya mathalani Tim Sebastian na Christian Amanpour kwa viongozi yalikuwa YANAFANANA KWA MTIRIRIKO ULEULE?!!

Kumbe mwandishi wa habari aliyebobea hupewa sifa pale ANAPOKUWA na MAHOJIANO ya "tug of war" na viongozi wakuu wa nchi ili mwishowe ionekane kiongozi huyo wa nchi AMEBANWA NA KUSHINDWA KUJIBU MASWALI.....kweli uliberali kazi.......🤣

Huko katika nchi zilizoendelea mfano Trump alikuwa ANAWAKATAA waandishi wa habari wa CNN (kaliba ya Christian Amanpour)....tukaambiwa na wapinzani wake kuwa ni kwa sababu Trump ni "dikteta"....Trump hana "ufahamu mkubwa" 🤣
 
Salimu kikeke ana uwezo mdogo sana. Hii ya kujificha nyuma ya mahojiano kufanyika ikulu haina maaana. Ikisikiliza vizuri utagundua mama alikuwa akijibu anavyotaka na hakukua na maswali fikirishi na yakuibua majibu lengwa.

Ni makosa makubwa Sana mwanzo mwisho wa interview hakuna lejea. Nafikiri hii ilikuwa press conference iliyoandaliwa na ikulu. Tafadhali Sana BBC mnaharibu bland yenu. Huyu jamaa anachemka interview karibu zote. Zuhura anajitahidi na nafikiri anaijui na kuimudu kazi yake.
 
Nilishawahi kubishana na mtu kuwa Zuhura ni bora kuliko kikeke kwenye kuhoji kimkakati ila watu hawachambui maswali ya kimkakati kutoka kwa waandishi. Angehojiwa na Zuhura bila woga ndo tungeona uwezo wa mama.
 
Salimu kikeke ana uwezo mdogo sana. Hii ya kujificha nyuma ya mahojiano kufanyika ikulu haina maaana. Ikisikiliza vizuri utagundua mama alikuwa akijibu anavyotaka na hakukua na maswali fikirishi na yakuibua majibu lengwa.

Ni makosa makubwa Sana mwanzo mwisho wa interview hakuna lejea. Nafikiri hii ilikuwa press conference iliyoandaliwa na ikulu. Tafadhali Sana BBC mnaharibu bland yenu. Huyu jamaa anachemka interview karibu zote. Zuhura anajitahidi na nafikiri anaijui na kuimudu kazi yake.
Uko sahihi, Zuhura ni kichwa kwenye kuuliza maswali ya kimkakati
 
Lazima tuelewe mahojiano yale ni baada ya Raisi kama Taasisi kukubali kufanya mahojiano, ili akubali ni lazima aonyeshwe au aelezwe anaenda kuulizwa nini na hapo ndipo tatizo linapoanzia. Kunakuwa na editing ya maswali.

Kikeke hakuwa na uwezo wa kuuliza hayo uliyashauri sababu everything there was pre-planned, publicity stunt.
Hata kama kuna editing ya maswali,alichokisema Bulendu ni kwamba hata kwa maswali hayohayo 'yaliyoruhusiwa' kuulizwa yalikosa backup ya rejea kutoka kwenye sheria, Mfano raisi aliposema baada ya Uchaguzi hakuna mikutano ya kisiasa alipaswa amuulize kwa sheria ipi? au aliposema kuna watu wamehukumiwa kwa Ugaidi angeuliza ni kina nani hao? Maana rekodi zinaonyesha bado wapo mahabusu hata kesi haijaanza.
 
Kikeke Atakuwa anawinda teuzi kwa Mama.Kuna Uzi nilisoma humu Mkataba wake na BBC uko ukingoni na Yuko mbioni Kurudi Tanzania,nyumbani.
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge.
@@@@@@
Honera sana kwa uchambuzi makini na summary murua kabisa.
Bulendu umetisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kilichofanywa na BBC kupitia Salim Kikeke jana hakipaswi kuitwa mahojiano bali ni mazungumzo tu ya kawaida kabisa baina ya bibi na mjukuu wake wa darasa la pili.

Ishort jana Salim Kikeke alienda kutalii Ikulu na pia alienda kumfanya huyu mama adhalilike mbele ya dunia kwa maboko aliyotoa mubashara.
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge.
@@@@@@

BBC wamefanikiwa kuongeza umaarufu wao Kwa Siku ya jana Kwa Maana ya Idadi ya watu wanaowasikiliza na kuwatazama kupitia Vyombo vyao vya
Safi Sana bulendu umetufumbua macho yani mama anadanganya mchana kweupe jamani haya magari yalichomwa lini Moto?
 
Yaani akina sheikh farid na wenzake wake acquitted na ugaidi then mbowe ndie awe gaidi?

Bi mkora anafeli, ila ajue kwamba mdude anao wembe wake
Kwa hiyo kwa mtazamo wako sheikh Farid na wenzake ndio walistahiki tuhuma za Ugaidi..ila Mbowe hastahiki....kwa kuwa yeye ni msafi sana? au kwa sababu ya dini yake?
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
Binadamu ni shida. wanakushangilia punde wanakusurubu. Wale wale waliokuwa wanasema mama anaupiga mwingi ndo hao hao leo wanalalamika
 
Kikeke ni mtangazaji siyo mwandishi wa habari

Rais Samia alimuuliza swali muhimu sana kwa ajili ya afya ya mjadala ule!
Hivi unaweza kuwa Mtangazaji wa Redio au Tv lakini usiwe chini ya 'Academic Umbrella' ya Journalism and Mass Communication course?

Nani aliyekudanganya kuwa huwezi kuwa Mtangazaji na usiwe umepita katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano?

Nakupa 'assignment' ndogo tu tafadhali mtafute huyu unayemuita Mtangazaji kisha muombe Cheti chake cha Kitaaluma nina utakutana Kimeandikwa kuwa amemaliza Kozi ya Uandishi wa Habari isipokuwa huko katika Utangazi ni sehemu tu ndogo ya Ubobezi alipokuwa mwaka wa mwisho Chuoni.
 
Hata kama kuna editing ya maswali,alichokisema Bulendu ni kwamba hata kwa maswali hayohayo 'yaliyoruhusiwa' kuulizwa yalikosa backup ya rejea kutoka kwenye sheria,

Ni kweli, hapa tunakubaliana...
Mfano raisi aliposema baada ya Uchaguzi hakuna mikutano ya kisiasa alipaswa amuulize kwa sheria ipi?

Ni ngumu kuuliza direct kwa kiasi hiki...

Hili ni swali linalotakiwa liwe backed up na sheria. Kwa hiyo swali linapaswa kuwa na rejea ya sheria...

Mfano, ni vyema swali hili lingeanza na "kwa mujibu wa sheria......

## Swali hili na jibu lake, lilifunua udhaifu wa kwanza mkubwa wa Rais. KUTOJUA KATIBA NA SHERIA MBALIMBALI ZA NCHI ZINAZO GUIDE UTEKELEZAJI WA SPECIFIC MATTERS mf. haki za kiraia, haki za binadamu, uhuru wa raia nk KATIKA NCHI AMBAYO YEYE NI RAIS WAKE...!!
au aliposema kuna watu wamehukumiwa kwa Ugaidi angeuliza ni kina nani hao? Maana rekodi zinaonyesha bado wapo mahabusu hata kesi haijaanza.
Yes, hili halina shida. Liko direct na yeye Rais ndiye aliyepaswa kuweka jibu lake kwa uwazi zaidi...

##Hili swali lilifunua udhaifu wake mkubwa pili mkubwa wa KUTOKUWA NA TAARIFA SAHIHI JUU KILE ALICHOKUWA ANAJIBU. Na hii inaweza kuwa inatokana na kuwa fed wrong information na wasaidizi wake wanaopaswa kumpa taarifa za kila siku za nchi...
 
Back
Top Bottom