DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

DP World anapewa kazi ya kupakua na kupakia Makontena tu, sio Bandari yote ya Dar wala si nje ya Dar

Ni zaidi ya Happ. Ndio maana imebidi nchi mbili ziingie makubaliano. Ingekuwa kuchukua nafasi wala wasingehitaji nchi mbili kukaa.
Mkuu huwezi kuamini lakini ukweli ni kwamba wanachukua sehemu ya bandari ya Dar tu. Sehemu nyingine ambayo wanafanya ushirikiano ni Teknolojia, Ujenzi wa chuo cha bandari upanuzi wa bandari pale Kurasini eneo la EPZA ambalo sasa ni Pori tu. Mambo ni mengi. Lakini kuhudu pale Bandarini wanachukua nafasi ya TICTS.
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 97%

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Hebu tupe sehemu ya mkataba wa makubaliano ya miaka mitano tuione.
 
Wengi wanoikataa DP World ni wale waliozoea Upigaji na wanajua wakija hawana chao.

Waliozoea hela za ICD na minada ya Bandari na kubambikizia kodi ili wapate Rushwa, hawapendi kuona DPW inakuja bongo.

Watatumia kila njia kupinga hata kupotosha Raia.
Wengi hawakatai DP kuwekeza ktk bandari zetu kama unavyosema, tatizo liko kwenye baadhi ya vifungu vya msingi wa mkataba uliopitishwa.
 
Hivi Dp wakiingia bandarini hizi kampuni za wazalendo za Clearing and forwarding si basi hazina kazi tena
Ndo zitafanya kazi sasa usiku na mchana. Wao wanahusika na kupakua makontena meli ikija na kupakia Makontena tu kama ilivyokuwa TICTS. TPA, TRA, TASAC, Polisi, Uhamiaji, Jeshi ataendelea na kazi kama kawaida. Sababu pale ni mpakani mtu anaweza kuingia nchi au kutoka.

DPW hawahusiki na mambo ya Clearing and forwarding. Sema wanarahisishiwa kazi. Mzigo analipia kabla haujafika. Ukifika tu na kuchukua na kuondoka siku hiyo hiyo.
 
Hii ngoma inafanya kila mmoja atoke pangoni kuja kutetea kwa kila namna!! Na ukishaona sintofahamu kama hii, jua tu kuna something wrong!!
Mimi nimekuja kuelezea ukweli ninao ufahamu. Hata wewe kama unaona Tanzania tunapigwa, andika na uelezee tunapigwa vipi mapema kabla ya Mikataba kuanza kusainiwa ili tusijilaumu Mikataba ikiwa ishasainiwa. Huu muda wa maazimio ndo wa kufunguka. Je, ni wapi tumepigwa? Usisubiri Watu waingiemkataba. Sema sasa hivi
 
Hata kwenye gesi mlisema hivyo kipindi Cha kikwete leo yako wapi? Mnaleta matazamio ya uongo wakati uhalisia bado.
Je, Makubaliano au maazimio kuhusu Gesi uliyaona? Si watu walikuwa wakihoji wanapigwa virungu na Polisi? Au umesehau jeshi lilivyo mwagwa Mtwara?

Rais Samia ameona hiyo sio njia nzuri wape wabunge wasome azimio, wape wananchi wasome azimip kama kuna tatizo lirekebishwe kabla ya kuanza kusaini Mikataba sababu Bandari ni ya Watanzania wana haki ya kujua nini kinaenda kusainiwa. Baadala ya kutukana na kupotosha huu ndo muda wa kuonesha penye mapungufu parekebishwe mapema. Tumepewa miezi 12 kupitia haya maazimio na kutoa maoni ya Ushirikiano. Watanzania hawajazoea haya mambo. Rais Samia kareta uwazi. Namshukuru kwa hilo.
 
Km Rais Samia ameshindwa kubuni vyanzo vya mapato aondoke ofisini waingie wenye uwezo

Kuuuza bandari kwa waarabu kwa visingizio visivyokuwa maana haikubaliki
Sasa hivi Nchi zote zinazojielewa duniani zimetoa kazi kwa private sector. Hata Marekani na Uingereza bandari zani zinaendeshwa na Private Sectors huyo huyo DP World. Kwanini sisi tukatae?
 
Kwa hiyo waziri wa Ujenzi na Uchukuzi alikuwa hajui hicho unachotuambia sasa? Mpaka akashindwa kukielezea kama unavyokielezea wewe??? Tumemsikiliza vizuri sana pale Bungeni, hakusema hicho unachokisema wewe. Kama angesema hicho, angeeleweka kirahisi sana. Usitutoe kwenye reli Mkuu..
 
Kapewa Bandari ngapi Tanganyika? Kapewa Bandari ngapi Zanzibar? Mkataba ni wa miaka mingapi?
Hakuna bandari hata moja amepewa si Tanganyika wala Zanzibar. Na hata hiyo bandari atakapewa sehemu ya bandari ya Dar tu pale TICTS alipokuwa kama haya maazimio bunge limepitisha yatakubalika.

Hadi sasa tumepewa miezi 1w kujadili maazimio kabla ya kuyasiani ili Mkataba wa kuendesha bandari usainiwe. Huo Mkataba sasa ndo watasema tutakuwa tunarenew baada ya Muda gani? Miaka 2,10,20 au mongapi? Hivyo vinakaa kwenye Mkataba sio Maazimio ya Nchi na Nchi ya Ushirikiano kwenye Uendelezaji wa Uchukuzi majini.
 
Nadhani Uungwana ulitakiwa ulete hoja yako au useme wapi nimedanganya ndo unitukane ili kufurahisha nafsi yako. Mengine unajishushia heshima Mkongwe kama wewe kushindwa kujadiliana kwa hoja.
Onyesha huo mkataba!
La sivyo, hizi ni post za kulaghai 'wadanganyika, kufifisha mjadala
 
Hilo ndo tulilotarajia, hao walitakiwa wapewe tender ya kufanya operations kama ilivyo TICTS na siyo kumilikishwa bandari, hilo haliwezekani.
 
Salaam Wakuu,

Wote tunaijua Bandari ya Dar Es Salaam.

Watu walidanganya eti kuanzia Geti namba moja hadi namba 8 anapewa DP World kumbe uongo. DP World anapewa kazi ya kupakia na kupakua Makasha kama ilivyokuwa kwa TICTS si kwamba anapewa bandari yote ya Dar, anapewa kijisehemu tu.

Kwahiyo TPA ataendelea na kazi ya kupakua Magari, Mafuta nk.

Pili DP World anakuja na Teknolojia ambayo itawezesha Mifumo ya TRA, TASAC, TPA isomane. Yaani mzigo wako ukifika unachukua hapo hapo hamna mambo Storage wala gharama zimezidi.

Hawa wanaopiga kelele ni watu waliokuwa wanategemea hela za storage hawa wenye bandari kavu. DP World yeye kwenye hatakuwa na mambo ya storage sababu hadi mzigo unafika unakuwa ushalipia kila kitu.

Nimefafanuliwa na Mwanasheria wa bandari baada ya kumtwanga swali.

Nimewapenda bure DP World.

Sasa hawa wanaopotosha wana dhamira gani?

Sema kuna wengine wanapinga sababu walishalishwa matango pori ukizingatia haya makubaliano ya awali yapo kwa lugha ya Kimombo.

Ukweli ni kwamba hadi sasa hakuna Mkataba umesainiwa wala hakina kitu kilicho chukuliwa. Hata huu Mkataba wa Mashirikiano ya Nchi kwa Nchi ambayo wanataka yawe na Ukomo nayo hayajatiwa saini.

Wanasiasa nao washapata sehemu ya kupepetea mdomo.

Natamani kuona Watanzania tukishikamana kwa manufaa ya Watoto wetu. Tuache kuishi kama zamani.

Sasa hivi TPA inapakua Kontena laki 6 kwa Mwaka. Ila DP World watapakua Makontena Mil 2 kwa Mwaka.

Sasa hivi baandali inachnagia pato la taifa kwa 35% lakini DP World wakianza Bandari ya taifa itachangia 97%

Hii itafanya Watanzania wapumue na mambo ya tozo. Nchi inatoza tozo hadi kwenye Miamala sababu hakuna vyanzo vya mapato vya kueleweka na Nchi lazima iendelee.

Ajabu ni kwamba Wanaoongoza kwa kuiponga DP World mitandaoni ni Wakenya sababu wanajua hii ni vita ya Kiuchumi. DP World wakianza bandari za Kenya hawana chao. Hata waliokuwa wanapinga bomba la Mafuta Mafuta Uganda kuja Tanzania ni Wakenya hadi wakaandamana Ulaya huko eti litaharibu Mazingira.

Watanzania tujitafakari na tujielewe.

Kila kitu kina mazuri na Mabaya, kwanini Wakenya wanaona Ubaya wa DP World tu?

Bila uzalendo tutaishia hapa hapa kulaumiana. Sasa hvi Mwarabu ndo mwenye hela ndo maana hata timu za Mpira za Uingereza anapewa Mwarabu. Hata Bandari zao wamempa Mwarabu lakini sisi wabongo Bandari tunataka eti tumpe Singa singa na Kanjibhai.

Tujaribu Waarabu japo miaka 5 tuone.

Nipeni basi hiyo connection ya kumpigania mama na mwarabu mteja wakuu!! Nasikia inalipa hatari!
 
Mazuzu kama Msukuma, Lusinde n.k wanaotuuza kama kwa wageni kama mafungu ya nyanya ngongwe
Mkuu, tuliza presha utueleze wanawauzaje? Pia jifunze kusikiliza pande zote kabla hujahukumu. Kipi kimeuzwa?
 
Km Rais Samia ameshindwa kubuni vyanzo vya mapato aondoke ofisini waingie wenye uwezo

Kuuuza bandari kwa waarabu kwa visingizio visivyokuwa maana haikubaliki
Wenye uwezo ni kina nani

Hao

Ova
 
Tanzania maboga mengi.. watu wanahadaika na Hoja zilizojaa siasa na kufungamana na manufaa ya chama. Hii ya DP inechambuliwa na watu kisiasa sana kuliko kiuchumi.. imetumika kikampeni
Mkuu watu wanasema kuhudu DPW? Tutonye na sisi tujue aisee. Kuna nini huko kwenye huo uchambuzi? Tuwekee hapa tuuone.
 
Back
Top Bottom