Waarabu watuletee maendeleo ndio mnavyofikiri kweli? Jamii zote alizoshukia mwarabu Tanzania zipo nyuma kimaendeleo na sasa anarudi kunyonya tena kama zamani.Unamtazama kwa uoga tu, unaona mama Samia na kubwabwaja na kuhororoja kwenu kote hana habari. yeye anaupiga mwingi tu, kitaifa na kimataifa.
Naona wewe na anayejiita FRANCIS DA DON mmekuja na wimbo mmoja lakini chorus tofauti. Ni mawakala wa shetani yupi nyinyi?
Maana mkataba huu hapa mbele ya uso wenu hamuoneshi una tatizo lipi? Tatizo lenu mkataba au Waarabu wanaokuja kutuletea maendeleo tuliyoshindwa kujiletea zaidi ya miaka 60 ya uhuru sasa?