DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji, Rais Samia umekosea sana

Mwendazake alishaaharibu watu wakafikiri ukiwa na madaraka unaweza kuteua kama utakavyo. Yeye akifanikiwa kwa hilo sasa mama asifikiri kuwa itakuwa rahisi kwake kuifanyia mambo kama Mwendazake.

Tatizo la Mama kuna watu kibao anataka kuwatoa ila hajui namna ya kuwaondoa.
 
Sheria zimekuwa zikikanyagwa toka mwendazake lakini ulikuwa kimya sasa mama ameshika kijiti unaleta ujuaji., Nchi yenu haihitaji majaji kufanyiwa vetting, majaji wanahukumu kesi kwa maelekezo tu., No justice at all -
Mwacheni mama wa kizanzibari naye awaongoze mlifkiri mzanzibari haitawezekana tena kuongoza Ikulu ya magogoni
 
Kaingizwa cha kike tena kama Richard Mwanafunzi wa Udom, waziri wa UDASO na Mwanasheria wa MTAKATIFU YOHANA[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mirembe ww kwenu hawafi huchoki kumsema marehemu
 
Tulia wewe usi-mu-undermine mama, ata uchukie vipi yeye ndo rais wa jamhuri mwache apigiwe vishoka, hao ndio washateuliwa kama una kundi la kuweza kwenda kuzuia kuapishwa kwao go ahead.,
 
Punguza chuki binafsi mkuu,
kwa nini unamchukia binaadamu mwenzio kiasi hicho?!.
huna hoja zaidi ni chuki binafsi, fitina na roho ya choyo.
 
Hiyo ndio njia pekee ya kumtoa pale jamaa....Mama katumia fimbo ya kisiasa kumchapa kama alivyomchapa Bashiru.... unampromote kumtoa usiyempenda huko umakompeleka unakwenda kumtelekeza kimyakimya.... Mama sasa yuko huru kufanya uteuzi wa DPP....
 
Biswalo anatakiwa kuwa jela ananyea ndoo, zile hela za Kabendera zinaniuma hadi leo.

Tusubirie na Jambazi mwingine Ole Sabaya atakapopewa uRC.
 
Awatoe aweke wakina faru John na genge lake au sio. Mwache mama afanye kazi yake.
 

Unajua Jaji kiongozi wa sasa alikua DPP prior?

Kwani Maganga kaanza lini kuwa DPP? If anything, JPM aligoma kumpa Maganga ujaji hata baada ya jina lake kupendekezwa.
 
Pendekezo la jana kuwa na sifa za kuwa jaji halina maana linaweza kutumika leo kuwa jaji. Kwanini? Sifa za mtu hubadilika kutokana na nafasi aliyonayo, nyakati tuliyopo na mwenendo wake.
 
Dah, mama kazungukwa na manyang'au...
Hawaja elewa kwamba hapakuwa na njia nyingine ya kumtoa hapo bila kumpsndisha cheo
Na sio yeye tuu katolewa, bali hata naibu wake.
Kumtoa ni tiba zaidi kwa Taifa kuliko kumuacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…