DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji, Rais Samia umekosea sana

DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji, Rais Samia umekosea sana

Huyu SSH sasa naanza kuamini maneno ya Lissu kwamba ni "malikia mwenye kauri tamu'

Ishu ya wazee wa Dar na Benz la Mwinyi, haijaisha, Swala la Mechi ya Simba na yanga kuailishwa Ili Mwinyi auze kitabu haijaisha, amefanya utoporo mwingine.

Huyu mama naona anaturembulia macho tu, Wala hafai, huko mbele ni Giza tu.
 
Sielewi kinachopingwa hapa! DPP aliyetangulia kabla ya huyu ni Eliezer Feleshi ambaye pia aliteuliwa na JK kuwa jaji wa mahakama kuu akitokea katika nafasi hiyohiyo. What's the difference? Kwanini uteuzi wa Jaji Feleshi haukupingwa?

Hata George Masaju alipoondolewa kwenye nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliteuliwa kuwa Jaji, na sikusikia aliyepinga kuwa mtu anateuliwaje kutoka mhimili wa serikali kwenda mhimili wa mahakama.
 
Uhuru bila mipaka ni Vurugu.

yaani watanzania sasa wamekuwa huru kuzungumza hadi wanavuka mipaka!!!!

yaaani wamefikia hatua sasa ya kumpangia Rais nini cha kufanya!!!!

Duh!!! hili sasa limezidi na endapo Kiongozi wetu ataendekeza kupelekeshwa na majungu basi hii nchi haiwezi kwenda mbele.

Tena ingekuwa mimi basi huyo mnaye mpiga fitina na majungu ningemteua kuwa Jaji Mkuu kabisaa, hamna maaana kabisa nyie watu, mmekosa aibu kabisa.

huyo mnaye mpiga fitina hajaokotwa barabarani alikuwa DPP na aliteuliwa na mamlaka.
 
Kwa hiyo unapendekeza afunguliwe Mashitaka ya Kutakatisha Fedha?

Kuna madai kuwa amekuwa akiweka fedha zinazolipwa na "Watuhumiwa" kwenye Akaunti yake, DPP, kule Benki Kuu, badala ya Akaunti ya Msajili wa Hazina, kana Sheria inavyoelekeza.

Tuliona huko nyuma, jinsi fedha zinavyoweza kuondolewa kirahisi kutoka kwenye Akaunti za Benki Kuu baada ya Mamlaka ya Bandari kuziondoa na kuzihamishia kwenye Akaunti ya Matumizi ya kawaida kwenye Benki za Biashara!

Hakuna Jinai hapo?

Biswalo Mganga mahali pake sahihi ni Mahabusu.
 
Teuzi zake za wasiwasi zimekuwa kielelezo cha utawala wake, kuanzia yule mkurugenzi wa TPDC aliemteua na baadae kutengua uteuzi wake within 24 hrs mpaka leo bado anayumba tu...
Nchi sasa iko mikono salama na ya matumaini, hayo mengine hayana maana kwa sasa.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Hajakosea chochote ni upuuzi wako na watu wenye akili fupi kama zako ndio mnawaza hivyo.
 
Ndama mtoto wa ng'ombe kama fisadi wengi ameaminishwa enzi ya Magufuli imeisha sasa mambo yanakua mema kwao. Ndio maana hataki tena kutumia fursa ya sheria ya kukiri kwa dpp. Watu aina yake wanaamini katika kununua haki kuepa mkono wa sheria.

Kwa mfano ile kesi ya iptl imekua ikizunguka mduara bila mwisho kila round nchi ikipigwa upya mahela na mafisadi wakitumia mahakama kuifanya kutafsiri sheria kwa namna ya kulidhulumu taifa.

Magufuli hakuruhusu upuuzi wa wanasheria fisadi wenye kutumikia mafisadi. Sheria aliyokua anatekeleza dpp sio yeye aliyoitunga ila ni bunge la taifa. Kumchukia biswalo ni kazi bure. Wengi waliyotiwa kibano na sheria na wamejaa lupango ni fisadi dhulumati wa wananchi wala hakuna uvunjaji wa haki zao wapo lupango kisheria.

Biswalo kupandishwa wadhifa kua jaji bila shaka ni kutambua kufanya wajibu wake kwa bidii na kwa weledi. Bila shaka dpp mpya ataendelea pale alipoachia biswalo.
 
Huna akili. Wewe ni goigoi usiefuatilia masuala.Unaelewa kuwa kuna sheria ambayo inazuia DPP kuondolewa kwenye nafasi hiyo labda awe anaumwa na kushindwa majakumu yake au labda awe amefanya serious crime?

Huyo DPP ameondolewa kwa mujibu wa sheria hiyo?Wewe ni ngumbaru sawa na aliemuondoa DPP kwenye nafasi yake bila ya kuzingatia sheria.Tanzania karibia kila mtu ni goigoi kuanzia wananchi wa kawaida hadi viongozi wakubwa. What a shame!

9876uy.jpg
0987654nb.jpg
 
Mother Theresa bhana, mziki unaopigwa ni singeli yeye anacheza reggae akija shtuka ili acheze style ya mziki, ndo dullah makabila anamalizia "imetoshaaaa" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Ifike mahala sasa, tusikubali viongozi wetu ambao wanajitoa kufanya kazi kwa moyo mmoja wachafuliwe kirahisi rahisi hivi.

tumeshuhudia tabia hii imeshamiri kwa kasi kubwa sana mara baada ya hayati JPM kuaga dunia!! hili halikubaliki na wala lisifumbiwe macho, tumeona maneno na kashifa nyingi zikitolewa kwa viongozi wetu wajuu, tuhuma za kizushi, majungu na fitina, hii si sawa.

mamlaka zinazo husika chukueni hatua, kwa nini mnaachilia watu wanachafuliwa tu, kutokana na chuki binafsi!!

kazi aliyo ifanya DPP ni ngumu sana ambayo hata angekuwa mtu yoyote yule lazima upate maadui wengi tu, ni sawa na kazi ya Ujaji au Uhakimu kamwe huwezi kupendwa na watu wote lazima wapo wengi watakuchukia kutokana na aina ya kazi yako kuwa huwezi kuwaridhisha watu wote na haswa kama unamsimamo na unasimamia sheria kikamilifu.

Biswalo ni mtu alitolea kufanya kazi zake kwa uaminifu wa hali ya juu na kutokana na uadilifu wake wapo ambao walitaka kumtoa kwenye msimamo na walishindwa, sasa nadhani ndio wakati wao wa kupiga majungu na kumfitini ilimradi achafuke ili wapate ushindi.

kamwe Rais wetu asiingie kwenye mtengo na kuwasikiliza watu wenye chuki zao binafsi.
 
Sheria zimekuwa zikikanyagwa toka mwendazake lakini ulikuwa kimya sasa mama ameshika kijiti unaleta ujuaji., Nchi yenu haihitaji majaji kufanyiwa vetting, majaji wanahukumu kesi kwa maelekezo tu., No justice at all -
Mwacheni mama wa kizanzibari naye awaongoze mlifkiri mzanzibari haitawezekana tena kuongoza Ikulu ya magogoni
Ilishajengeka dhana kwamba mzanzibari wa mwisho kuongoza nchi ni mzee Mwinyi. Ni ule ule ubinafsi na uchoyo.

Watakaojaribu kumfanya Mama atetereke kiuongozi kuelekea 2025 ni watu wanaosumbuliwa na hiyo dhana potofu ambayo ni ya ubaguzi unaofichwa kwa kutumia hoja za mijadala ya JF na huko facebook na twitter.
 
Ifike mahala sasa, tusikubali viongozi wetu ambao wanajitoa kufanya kazi kwa moyo mmoja wachafuliwe kirahisi rahisi hivi.

tumeshuhudia tabia hii imeshamiri kwa kasi kubwa sana mara baada ya hayati JPM kuaga dunia!! hili halikubaliki na wala lisifumbiwe macho, tumeona maneno na kashifa nyingi zikitolewa kwa viongozi wetu wajuu, tuhuma za kizushi, majungu na fitina, hii si sawa.

mamlaka zinazo husika chukueni hatua, kwa nini mnaachilia watu wanachafuliwa tu, kutokana na chuki binafsi!!

kazi aliyo ifanya DPP ni ngumu sana ambayo hata angekuwa mtu yoyote yule lazima upate maadui wengi tu, ni sawa na kazi ya Ujaji au Uhakimu kamwe huwezi kupendwa na watu wote lazima wapo wengi watakuchukia kutokana na aina ya kazi yako kuwa huwezi kuwaridhisha watu wote na haswa kama unamsimamo na unasimamia sheria kikamilifu.

Biswalo ni mtu alijitolea kufanya kazi zake kwa uaminifu wa hali ya juu na kutokana na uadilifu wake wapo ambao walitaka kumtoa kwenye msimamo na walishindwa, sasa nadhani ndio wakati wao wa kupiga majungu na kumfitini ilimradi achafuke ili wapate ushindi.

kamwe Rais wetu asiingie kwenye mtengo na kuwasikiliza watu wenye chuki zao binafsi.
 
Acha mbwembwe zako za kiharakati hapa, hiyo tume ya utumishi wa mahakama ndio imekupa taarifa hizo kwamba hakupendekezwa popote?

Umewasiliana na Jaji mkuu kuhusu uteuzi huo ukamhoji uzingatiwaji wa taratibu na kakuambia hazikuzingatiwa?

Kwanini Jaji mkuu kama mhimili unaojitegemea asikatae kwa mamlaka aliyokuwa nayo?

Hapa inadhihirisha umetumwa na watu wenye makosa ambao kwa kubanwa kwao ndio maana unaropoka ovyo tu hapa jukwaani?

Wewe una weledi upi wa kuhoji maadili ya Biswalo Mganga kama sio chuki binafsi zinazokusumbua?

Kwa maoni yangu baada ya Mh Rais kuwapeni upenyo wa kukosoa sasa mnajiokotea hata takataka huku mkijinasibu mna weledi wa sheria wakati mufilisi tupu

Peleka pingamizi mahakamani ili upewe tafsiri sahihi kuliko kulindima kisiasa jukwaani hapa
 
Jifunze kutokuwa na wivu mkuu, ukiona mtu kateuliwa usisononeke wewe piga kazi hayo mambo huwa anapanga Mungu.
Nashukuru kumwambia jamaa aache wivu na achape kazi, nami nakuambia acha kumsingizia Mungu kwamba amepanga, wakati ni mipango ya wana-mboga mboga tu!
 
Ww ni mtu

Ww ni MTU wa ajabu sana.Tena mjinga na mpumbavu.Kila MTU ana nafasi yake.Kakojoe huko ,ulale.
Huyu siyo Mtu wa ajabu, mjinga wala mpumbavu, labda kama na wewe ni hivyo ama zaidi yake!
 
Mkuu

Mh Rais ndio katoa upenyo huo ambao ndio utakuja kumwadhibu hatasahau kwamba Watanzania hawatabiriki katika maamuzi. Kelele zote unazozisikia zina baraka ili ionekane mbwa wa kijakazi ndio anabweka kumbe sivyo, fikiri kwa kina jawabu utalipata sawia.

Nakumbuka miaka ya 1990 Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi alidhalilishwa sana na jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu hapo mlimani DSM kwa kuchorwa na jukwaa la kijamii lililoitwa 'Punch' akivunjiwa heshima.

Kiongozi wa nchi ukisharuhusu tu kwamba ni 'rukhusa' basi tambua kwamba utaingizwa hata wewe mwenyewe 'postmortem' utapasuliwa viungo vyako vyote nje kisha wataanika hadharani-ndio si umeruhusu kukosoa ndio matunda yasiyofaa kwa kiongozi kuwa 'democratic' taswira yake ni udhaifu.

Kiongozi wa nchi ni sharti awe mchanganyiko wa-Democratic (wewe unaonaje hapa?)+autocratic (fanya kama ninavyosema)+authoritative (nifuate mimi)+pacesetting (fanya kama ninavyofanya mie)+coaching which is commonly effective (tafakari kuhusiana na hili na uwe makini)+affiliative (hudumia watu wengine kwanza)+laissez-faire-which is rarely effective (hobela hobela bila mpangilio na udhibiti, kila mmoja anafanya anavyoona inafaa au kuweza) hapo ndipo+strategic which is commonly effective+transformative (sometimes effective)+bureaucratic (rarely effective)+transactional (sometimes effective).

Tamatisho
Kujua ni mitindo gani ya uongozi inafanya kazi vizuri kwako ni sehemu ya kuwa kiongozi mzuri. Kuendeleza mtindo wa utambulisho wako na uwezo wa kunyoosha katika mitindo mingine kwani hali inaweza kusaidia kuongeza ufanisi wako wa uongozi. Mitindo ya uongozi wa mseto inahitaji kuunganishwa na mbinu mpya sambamba na jinsi uongozi unavyofafanuliwa kwa karne ya 21. Mazingira ya shughuli mbalimbali za leo yanakumbushwa na changamoto kutokana na kubadilika kwa idadi ya watu na matarajio ya wananchi mbalimbali. Hii inaweza kuitisha uzalishaji mpya wa kiongozi ambaye ni kiunganishi wa mitindo mikubwa ya uongozi. Inashauriwa kufahamu kwa undani ‘repertoire’ (hazina ya ujuzi au aina ya tabia ambayo mtu hutumia) ya mitindo ya uongozi ambayo inaweza kufanya kazi vizuri kwa hali fulani

Kiongozi unatakiwa kuwa na uhalisia na mbinu yoyote unayotumia. Kubadilika kutoka mtindo mkubwa wa uongozi hadi mwingine tofauti inaweza kuwa changamoto mwanzoni. Fanya mazoezi ya tabia mpya ambayo umeshaipima na kushuhudiwa na wanufaika wake mpaka ziwe za asili. Kwa maneno mengine, usitumie mtindo tofauti wa uongozi kama njia ya kudandia kufika mahali kirahisi na endapo utafanya hivyo watu wanaweza kunusa kuvaa mtindo bandia wa uongozi bila kustahili.
 
Back
Top Bottom