VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kuna jinai kubwa imetendeka.
Kuna uvunjaji mkubwa wa Katiba na Sheria za nchi umetokea. Mhusika lazima abainishwe na achukuliwe hatua kali za kisheria. Mambo yako hivi: CHADEMA wamesema na wanaendelea kusema kuwa hawakuwasilisha Orodha ya Wabunge wa Viti Maalum NEC. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ndiye mhusika wa kupeleka majina na mjazaji wa Fomu za kisheria.
Katiba imevunjwa, sheria zimevunjwa. Orodha haikupelekwa. Orodha aliyopewa Spika, kuiamini na kuwaapisha jana ameitoa wapi? Anzeni na Spika. Kama ameipata Orodha kutokea NEC, NEC wamepewa na nani? Nendeni na NEC. Halafu, wote 19 walioapishwa jana wahojiwe na waeleze, pamoja na mambo mengine, waliambiwa na nani kuwa wameteuliwa kuwa wabunge. Waseme waliambiwa kwa njia gani.
Hapa kuna mambo ya pesa za umma. Kuna mambo ya katiba na sheria. Hapa kuna mambo ya jinai kubwa. DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania. Lindeni pesa zao, katiba yao na sheria zao. Mtaheshimiwa na kuthaminiwa. Wakati ni huu!
Mwaka 2020 kulikuwa na uchafuzi mkuu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam.