DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

DPP, TAKUKURU na Polisi: Wasikilizeni CHADEMA. Kuna jinai kubwa imetendeka

kaba ya jin
Kuna jinai kubwa imetendeka.

Kuna uvunjaji mkubwa wa Katiba na Sheria za nchi umetokea. Mhusika lazima abainishwe na achukuliwe hatua kali za kisheria. Mambo yako hivi: CHADEMA wamesema na wanaendelea kusema kuwa hawakuwasilisha Orodha ya Wabunge wa Viti Maalum NEC. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ndiye mhusika wa kupeleka majina na mjazaji wa Fomu za kisheria.

Katiba imevunjwa, sheria zimevunjwa. Orodha haikupelekwa. Orodha aliyopewa Spika, kuiamini na kuwaapisha jana ameitoa wapi? Anzeni na Spika. Kama ameipata Orodha kutokea NEC, NEC wamepewa na nani? Nendeni na NEC. Halafu, wote 19 walioapishwa jana wahojiwe na waeleze, pamoja na mambo mengine, waliambiwa na nani kuwa wameteuliwa kuwa wabunge. Waseme waliambiwa kwa njia gani.

Hapa kuna mambo ya pesa za umma. Kuna mambo ya katiba na sheria. Hapa kuna mambo ya jinai kubwa. DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania. Lindeni pesa zao, katiba yao na sheria zao. Mtaheshimiwa na kuthaminiwa. Wakati ni huu!

Mwaka 2020 kulikuwa na uchafuzi mkuu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
kabla ya jinai kwanza wajitathimini wao ndani ya chama na aina ya uongozi wa chama chao, jinai isubiri.
 
Mnataka iweje? je mnafikiri bila sihasa watakula wapi?
Kwani wanaoishi kwa mshahara wa laki moja unusu wanaishije?? Sembuse hao wengine wenye kiinua mgongo cha 240+mil walichochukua hata miezi mitatu haijaisha?
 
Kesi ya mchawi anapewa Shetani, unafikiri kuna kitu hapo
 
Chadema porojo tu kama wako serious wawachukulie hatua wao kwanza ndipo waite DPP wasitumie DPP kama kichaka cha kujificha mleta Mada usirukie kwa DPP
 
Mnyika ametoa ufafanuzi mzuri sana.

Hapo kwenye form no. 8(d) inayotakiwa kuwasilishwa bungeni ikiwa na jina la mhusika na Mnyika amesema bado anazo form zote, hii pekee inaonesha nchi inavyoendeshwa kiajabu siku hizi.

Taasisi zote hazifuati sheria tena, wanafanya mambo ya ajabu.
Mnyika aache porojo hapo kasema ana fomu anazo original au photocopy? Hajasema

Wameapa hadharani waziwazi kama wamekiuka so chama kiwachukulie hatua

Hakuwa hata na haja ya kuitisha Press conference anatafuta pa kujisafishia mnafiki mkubwa

Ohhh fomu ninazo sasa kama unazo chukua hatua basi
Chadema wasanii wanachoogopa kuchukua hatua nini?

Wanataka kusukumia zigo sijui NEC sijui bunge utapeli mtupu

Kama wamekiuka toeni Tamko la kuwafukuza chama mbona midomo inakwepa kutamka

Mnyika msanii
 
Jinai kubwa ni kutopeleka majina ya viti maalumu na kuwanyima wawakilishi wa wananchi fursa
Mkiwa katika juhudi za kuendeleza uchafuzi, mtaokoteza vineno mpaka mtaugua. Sio siri tena kuwa mwaigwaya sana CHADEMA.
 
Mshapigwa changa la macho na bado mtasikia TL kateuliwa yaani mtatembelea nyongo.

Game la siasa waachie kina mbowe wengine mnajichafulia CV tu
 
Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya hao wabunge waliokwenda kuapa bungeni.
Mdee na wenzie...

Hivi hao wabunge wasingekwenda hata hyo karatasi inayoeleza majina ya wateuli viti maalum isingekuwa na maana yeyote kwa NEC..

Swali la kujiuliza..

-- ni akina nani waliopeleka barua NEC.

-- Je iweje halima mdee amshukuru
mbowe hadharani kwa kuwapa baraka zote za chama?

Kama mbowe hahusiki kwa hilo kwann
mdee amuhusishe?

-- kama kweli hawawatambui wabunge waliokwenda kuapa bungeni,,
wamewachukulia hatua gani kama chama?

Vinginevyo ni cinema ya kihindi..
 
"Natural justice".
 
Labda mimi ndo sielewi siasi, hao kina mdee walipewa taarifa na nani kwamba wameteuliwa na wanatakiwa kwenye kuapishwa bungeni? na kama ni NEC ndo ilipitisha tu majina yao na kuyapeleka kwa spika bila kushirikisha viongozi wa chadema je walipoitwa kwenda kuapishwa lilikuwa ni jambo la lazma kwamba wangekataa wangekufunguliwa mashitaka? Kama ilikuwa ni hiari ya kukubali au kukataa iweje lawama ziende kwingine?

Kiuhalisia wao ndo walipaswa kuwasiliana na chama chao ukizingatia wao kama chadema hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi, na mgombea wao ambae ni Lisu ameshatamka hadharani for the whole world to hear kwamba hawalitambui bunge wala hawatashiriki, sasa leo wafuasi wake wanaenda kuapa kwenye hilo hilo bunge ambalo wamesema hawalitambui, tena wakijua wazi kwamba viongozi wao hawana taarifa ya kuteuliewa kwao na hata kama wangepewa taarifa lazima wangepinga, but that ddnt stop them, imekaaje hiii? mleta uzi unazunguka mbuyu kutafuta mchawi wakati hii ishu ilitakiwa wahojiwe hao walioenda kuapa kwenye bunge wasilolitambua wamekubalije?
 
Kesi ya nyani unampelekea ngedele.😂😂
 
Mambo ya hivi ndiyo maana hata MABEBERU wanatudharau kabisa - yaani majina yamepelewa kwa spika 20th Nov, cha ajabu mmoja kati ya hao alikuwa gelezani miezi kadhaa na katolewa 23rd Nov... Sasa jiulize kwamba alifanikishaje zoezi la kuteuliwa kwake Ubunge akiwa gelezani ?

Mambo mengine jamani si ni ya aibu tu haya!!
 
Wote Wameoza Na Kupungukiwa Utukufu Wa Mungu

Sheria Ichukue Mkondo Wake
 
Behaviorist you are now crossing the red-line for posting this figurative cartoon which represents bashing, trolling and provocative, you may eventually pay the price for entertaining these kind of unacceptable ridicule. Your ID is on eavedrop track to account the assault
Empty tin pole sana. Hata wa chekechea watazimia kwa kukucheka.
 
Polisi hii hii iliyopewa mpaka namba ya gari ambalo lilikuwa linamfuatilia Lissu na hakuna ilichofanya.
Polisi hii hii iliyopewa mpaka namba ya simu ambayo ilikuwa inamtumia Ben Saanane vitisho na hkuna ilichofanya.
 
Kuna jinai kubwa imetendeka.

Kuna uvunjaji mkubwa wa Katiba na Sheria za nchi umetokea. Mhusika lazima abainishwe na achukuliwe hatua kali za kisheria. Mambo yako hivi: CHADEMA wamesema na wanaendelea kusema kuwa hawakuwasilisha Orodha ya Wabunge wa Viti Maalum NEC. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ndiye mhusika wa kupeleka majina na mjazaji wa Fomu za kisheria.

Katiba imevunjwa, sheria zimevunjwa. Orodha haikupelekwa. Orodha aliyopewa Spika, kuiamini na kuwaapisha jana ameitoa wapi? Anzeni na Spika. Kama ameipata Orodha kutokea NEC, NEC wamepewa na nani? Nendeni na NEC. Halafu, wote 19 walioapishwa jana wahojiwe na waeleze, pamoja na mambo mengine, waliambiwa na nani kuwa wameteuliwa kuwa wabunge. Waseme waliambiwa kwa njia gani.

Hapa kuna mambo ya pesa za umma. Kuna mambo ya katiba na sheria. Hapa kuna mambo ya jinai kubwa. DPP, TAKUKURU na Polisi, wasaidieni watanzania. Lindeni pesa zao, katiba yao na sheria zao. Mtaheshimiwa na kuthaminiwa. Wakati ni huu!

Mwaka 2020 kulikuwa na uchafuzi mkuu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Hao uliwataja ndiyo wahusika wa kubwa wa hii move
 
Back
Top Bottom